Pole sana Mkuu, ngoja nikutafsirie kidogo.
-Kwanza kabisa Mkuu wewe huwa unachukuliwa usiku na unapelekwa sehemu za kichawi ila kuanza kukutumikisha moja kwa moja hapo sijajua.
- Pili, anayekupeleka huko sio mdogo wako kama wengi walivyosema. Siraha kubwa kwa uchawi ni usiri. Anayekuchezea hawezi akaleta sura yake ili umjue, ukimtambua ile nguvu yake hupungua kwa kasi sana. Kuonesha kwamba upo na mdogo wako inakuashiria kwamba ni mtu wako wa karibu kama mzazi, jirani, ndugu, jamaa n.k
-Umesema kwamba umetupiwa mikaa mitatu, baada ya kutupiwa ulipata maumivu au kujeruhika sehemu yoyote?
- Kuna mtu wako wa karibu anataka akuunganishe na Uchawi. Na hizo process zimeshaanza na hivyo ulivyotupiwa ni uchawi dhahiri, na ulipoambiwa usiseme ni kama upo ktk training ya kichawi kwamba usiwe mtoaji siri kwa yote yanayotendeka huko.
Wachawi wanapoanza kumtumikisha mtu ktk uchawi wanaanzaga na ndoto kisha ndo wanakuja kukudhihirisha moja kwa moja.
TAFSIRI YA PILI
-Tafsiri ya pili ya hii ndoto yaweza kuwa kwamba kuna sehemu mtu wako wa karibu atafanya jambo ila wewe ndo utahusishwa kama mtendaji wa hilo kosa.
Kuwa makini!