Naomba mwenye Tangazo tajwa hapo juu lililotoka kwenye magazeti siku ya Jumatano(hii/wiki iliyopita sina hakika sana) atuwekee hapa kwa faida ya wengine!
Website ya wizara ipo katika matengenezo kwa hiyo ni ngumu kulipata online.
Tangazo kweli nimeambiwa limeshatoka lipo kwenye mbao za matangazo wizara ya elimu. Website yao ipo down hivo mwenye kuweza kufika pale wizarani tafadhali atusaidie alibandke hapa.
Lilitoka kwenye Mwananchi ya wiki iliyopita. Nililiona ila nimemisplace gazeti lenyewe.
Tangazo lilitaka waombaji waombe online kwenye website hii http://laihua.csc.edu.cn. Ukiingia humo utakutana na program nyingi lakini wao walitangaza scholaship za Masters na PhD kwenye Agriculture, Medicine, Nursing, Pharmacy, Engineering (sikumbuki specialization) na Rural Development.
Ila kwenye hiyo website unaweza kuomba scholarships kutoka Vyuo hadi vitano hasa kwenye MBA, International Relations, Public Administration, Educational Management n.k
Nimeliona hilo gazeti ni la tarehe 4/2/2015..Field of study;Pediatrics,Nursing, ICT,Electronic Engineering, Mechanical,Environmental Science,Pharmacy,Medicine, rural Development,Agriculture, Oil and Gas for Masters degree.
Qualifications; Age below 35 and GPA of not less than 3.5 at Undergraduate.
Mkuu asante kwa infor. Ila hio stage ya online hua ni ya pili ukishakua umechaguliwa na wizara. Kama umeingia ukacheki hio website kuna sehem kabisa ya kwanza unatakiwa kujaza Nominating agency number ambayo kwa case hii ni number wanayo wizara hua wanatoa kwa wale waliowapendekeza wao.
Kwa navojua mimi kwa sasa unatakiwa kuandika barua tu ya maombi pamoja na vyeti vyako then watachagua watu hao ndio watakaoomba ile online.
Hio naongea from experience na baada yakuona hilo tangazo. Ila nashauri kama kuna mtu yupo dar aende wizarani akaukizie vizuri tupate uhakika zaidi maana hicho nachosema ndio hua utaratibu wa miaka yote.
Tangazo linasema...Recommended candidates are required personally to conduct online applications. Utaingia kwenye links zilizopo hapo juu. Maana yake lazima uwe recommended na Wizara.