Msaada: Taratibu za kugawana mirathi kisheria

Msaada: Taratibu za kugawana mirathi kisheria

kintakunte

Member
Joined
Apr 21, 2012
Posts
42
Reaction score
8
Mimi ni kijana wa familia, nina dada wawili baba yetu alipofariki aliacha urithi wa nyumba mbili na shamba la viwanja vidogo kama sita ukigawa) nje kidogo ya Dar es Salaam nafanyia kazi mikoani na siishi Dar ila dada zangu wamezaa hawajaolewa wanaishi nyumbani ndani ya hilo shamba kubwa na mama yangu mzazi.

Naomba utaratibu wa kisheria wa kugawana maana kila ninapozungumzia vita huanza baina yao na mimi nahitaji nijenge japo nyumba kati ya kiwanja cha mgao.
 
Ni nani msimamizi wa mirathi ya marehemu baba yenu, kimahakama.
 
kama unataka kujenga nunua kiwanja chako wewe.mtakuja toana roho bure kwa mali alizo acha baba yenu.ww mtoto wa kiume bana
 
Tafuta mali zako kijana hilo ni jasho la baba yako hivyo ni halali kabisa ukamuachia Mama. Yeye ndiye ataamua aidha agawe kwenu watoto au apige bei. Komaa wewe ushakuwa mtu mzima mbona baba yako aliweza? mwanaume unaanza vipi kupigania mali za urithi na dada zako???
 
Tafuta mali zako kijana hilo ni jasho la baba yako hivyo ni halali kabisa ukamuachia Mama. Yeye ndiye ataamua aidha agawe kwenu watoto au apige bei. Komaa wewe ushakuwa mtu mzima mbona baba yako aliweza? mwanaume unaanza vipi kupigania mali za urithi na dada zako???

kwani yeye siyo mnufaika wa mali za baba yake??
 
Mi nashangaaga kweli mitoto inayotoaga mawazo ya kugawana badala ya kutafuta tu.
 
Lazima mtoane roho..ata ukiwapelekea kitabu au katiba hawatakubali..ukiona binti anazalia kwao ujue..kuna tatizo..wanajiona wana mali..sasa hawatakubali uwavuruge wakati viwanja vinawapa kibri
 
kuna maswali mengi ya kujiuliza hapa,je kabla ya kufa baba hakuandika wosia?(dying intestate),kama Luna wosia je ni halali?(validity of will),kama hakukua na wosia kabisa je marehemu alifata itikadi gani/life style kati ya kimila,kiislam,kikristo or hakuna kabisa? he hakuna mnufaika au mtu yeyote aliyeomba usimamizi was mirathi? na je mzee wakat anakufa alifia wapi(jurisdictional purpose),mwisho je hakuacha madeni yoyote na iwapo aliacha ukiteuliwa kunufaika kama mrithi utakua tiyari kulipa madeni endapo madeni yatazid thamani ya Mali iloachwa(estate), hayo in baadhi tu,kikazi zaid tutafutane
 
Back
Top Bottom