Kwa namna ulivyobainisha tarehe zako za mzunguko, inaonesha mzunguko wako una siku kati ya 28 na 29.
Kawaida siku ambayo yai hupevuka na kushuka kuelekea mji wa mimba "Ovulation" ni siku ya 14 kabla ya siku ya mwisho ya mzunguko wake.
Mathalani;
mtu mwenye jumla ya siku 28, basi ovulation kwake hutokea siku ya 28 kutoa siku 14 [ 28 - 14 = 14]
mtu mwenye jumla ya siku 29, basi ovulation kwake hutokea siku ya 29 kutoa siku 14 [ 29 - 14 = 15]
mtu mwenye jumla ya siku 30, basi ovulation kwake hutokea siku ya 30 kutoa siku 14 [ 30 - 14 = 16]
nakadhalika na kadhalika....
Sasa wakati mzuri wa kufanya mapenzi kwa wale watafutao mtoto, iwe ni siku tatu kabla ya ovulation, siku ya ovulation yenyewe na siku tatu baada ya ovulation.
Sasa kwa wewe
MadamG, jaribu kuchakarika kuanzia tarehe 26, 27, 28, 29, 30, 31 halafu endelea na tarehe 1,2 na 3.
Most likely, ovulation yako ikawa tarehe 29 au 30.