Habari ndugu zangu!!
Ngoja niingie kwenye maada moja kwa moja, kwa muda sasa nimekuwa nikiwashwa sana sehem ya haja kubwa. Nimejaribu kutumia sabun tofaut lakn wapi, nmetumia dawa za minyoo nazo nkizan ni pinworms lakin bado tatizo halijaondoka, naomba mwenye kujua tiba sahihi ya tatizo hili aweze kunisaidia, na kusaidia wengine wenye tatizo kama hili.
Asanten Ndugu zangu, wote mtakao onyesha ushirikiano kwenye hili. [emoji120]
PRURITUS ANI
Muwasho kwenye njia ya haja kubwa, husababishwa na:
1: Fangasi
2: Bakteria
NB: Hapa unaweza kupata mchanganyiko wa vyote. Fangusi pamoja na bakteria. Njia rahisi huwa ni kutimia dawa yenye mchanganyiko wa dawa dhidi ya bakteria, fangus na muwasho. Unaweza kufanya hivyo kwa kunawa vyema na kupaka dawa.
3: Minyoo
Hapa suluhisho huwa ni kupata dawa ya minyoo. Kuna aina ya minyoo ambayo hutoka nje wakati wa usiku ili kutaga mayai, huwa ni chanzo kikubwa cha muwasho.
4: Michubuko vs kuchanika/fissures:
Hii inaweza kusababishwa na choo kigumu au kujikuna mwenyewe baada ya kupata muwasho.
Suluhisho:
Kuhakikisha unapata choo laini na kupata dawa ya muwasho. Choo laini hupatikana kwa kunywa naji ya kutosha kulinhana na uzito, kazi na hali ya hewa uliyopo, kula matunda kwa wingi pamoja na mbogamboga.
5: Aina ya vyakula
Ukishapata madhira maeneo husika, vyakula vifuatavyo vyenye kuleta muwashawasha huongezea tatizo: pilipili, kahawa, tangawizi, chocolate nk.
Hivyo, ni vyema kujizuia na vyakula husika.