Habari wakuu,
Mimi ni mfugaji wa naombe nilipata changamoto wa ngombe wangu kufa kwa tatizo la kutokula na kutoa udenda pia anapepesuka akitembea. Baada ya kufa alipasuliwa tumbo na kukutwa na maji tumboni na nyongo yake ni kubwa sana na nyeusi sana pia.
Baada ya siku tatu tatizo likaanza kwa ndama dume naye akafa.
Sasa ivi kwa siku 6 zilizopita tatizo limenza kwa mwingine na kuonyesha dalili za wengine kama mwanzo la kutokula majani pia amedhohofika sana na akitembea anapepesuka sana pia anatoa udenda.
Nimemuita daktari wa mifugo kata ..kaja kampima na kumdunga shindano (kasema ya kushusha joto) akaondoka na hali ya ngombe imekua mbaya zaidi .. Naombeni msaada kwa madaktari dawa ya kutatua tatizo. Au namna na jinsi yoyote.
Asan
Pole sana mkuu na changamoto ulizopitia na unazoendelea kupitia, baada ya hapo hebu twende pamoja ili tuweze kukusaidia
Kwanza kitu cha kujua ni kwamba uchunguzi sahihi hukupa dawa sahihi, na baada ya kupata dawa sahihi ndipo kupona kunakuja
Kwa dalili ambazo umesema Ng'ombe wako walikuwa nazo hasa hao wa Kwanza, hapo kuna uwezekano walikuwa na magonjwa yafatayo
1.Homa ya mapafu, ambapo mnyama anakuwa anapata shida ya kuhema,kuchoka sana,kutembea akiwa hana nguvu na mwisho kuwa anatoa mate mdomoni
Lakini pia hizo shida za kupumua huambatana na dalili za mafua na kifua, kwahiyo mnyama anaweza kuwa anatoa makamasi au anaweza kuwa anakohoa sana
na mnyama akichinjwa huwa anakuwa na maji mengi sana katika sehemu ya mbavu/kifuani na yanakuwa kama ya njano hivi
Matibabu yake ni kumchoma huyo mnyama dawa ambayo inatibu maradhi ya mfumo wa hewa, ambayo inaweza kuwa Tylosin 20%, Amoxicillin 15% au Enrofloxacin 10% hizi zote ziwe injection
Na hizo dawa zitatumika Kwa siku 3-5 inategemea na maelekezo ya dawa husika, lakini pia kama mnyama hana Mimba utachoma Dexamethasone ili kwenda kuondoa Athari za mapafu ambazo mara nyingi huwa ni kujaa Maji
2.Ugonjwa wa miguu na kwato, huu mnyama akiupata anakuwa anasumbuliwa na vidonda kwenye midomo pamoja na kwenye kwato, na mara chache kwenye kiwele
Hivo vidonda hupelekea mnyama kutoa mate mdomoni ambayo huning'inia lakini pia hukosa hamu ya Kula maana vidonda hushambulia ulimi pamoja na kinywa chote
na mwisho kabisa mnyama akipata vidonda vya kwenye miguu hufanya ashindwe kutembea au kusimama na ata akisimama/kutembea huwa anatembea upande upande
Haya yote utayajua endapo tu utachukua muda wako na kumchunguza vizuri mnayama wako, Kwa kuanzia katika kinywa hadi miguuni, ukikuta tu vidonda mdomoni unajua kuwa huu ugonjwa ni wa kinywa na kwato hivo unaangalia na kwato pia
Endapo kama shida ndio hiyo, basi unaanza Kwa kusugua na chumvi vidonda vya kwenye kinywa hadi Damu zitoke au viwe visafi kabisa na kisha unafatia kusugua pia vidonda vya kwenye kwato kama vipo
Baada ya hapo utamchoma mnyama wako dawa ya Penstrep 20% high dose au Gentamicin 10% high dose pia au sulfa high dose pia, ila kama utatumia sulfa inabidi uchome asubui na jioni Kwa siku 3 ila hizo zingine unachoma Kwa siku mara 1
Na ikibidi ununue na dawa ya vidonda ya kuspray (wound spray) baada ya kuwa umesafisha vidonda unapulizia hiyo Kwa ajili ya kutibu vidonda lakini pia kuzuia infections ambazo zinaweza kusababishwa na kidonda
Kwahiyo zingatia hizo dalili na uhakikishe kabla ya kutumia dawa uwe umejiridhisha na uchunguzi utakaoufanya. All the best