Msaada: Tatizo la ng'ombe kupepesuka na kutoa udenda anapolala

Msaada: Tatizo la ng'ombe kupepesuka na kutoa udenda anapolala

Shukrani kiongozi.. Nitakuja na mrejesho
Pole sana mkuu na changamoto ulizopitia na unazoendelea kupitia, baada ya hapo hebu twende pamoja ili tuweze kukusaidia

Kwanza kitu cha kujua ni kwamba uchunguzi sahihi hukupa dawa sahihi, na baada ya kupata dawa sahihi ndipo kupona kunakuja

Kwa dalili ambazo umesema Ng'ombe wako walikuwa nazo hasa hao wa Kwanza, hapo kuna uwezekano walikuwa na magonjwa yafatayo

1.Homa ya mapafu, ambapo mnyama anakuwa anapata shida ya kuhema,kuchoka sana,kutembea akiwa hana nguvu na mwisho kuwa anatoa mate mdomoni

Lakini pia hizo shida za kupumua huambatana na dalili za mafua na kifua, kwahiyo mnyama anaweza kuwa anatoa makamasi au anaweza kuwa anakohoa sana

na mnyama akichinjwa huwa anakuwa na maji mengi sana katika sehemu ya mbavu/kifuani na yanakuwa kama ya njano hivi

Matibabu yake ni kumchoma huyo mnyama dawa ambayo inatibu maradhi ya mfumo wa hewa, ambayo inaweza kuwa Tylosin 20%, Amoxicillin 15% au Enrofloxacin 10% hizi zote ziwe injection

Na hizo dawa zitatumika Kwa siku 3-5 inategemea na maelekezo ya dawa husika, lakini pia kama mnyama hana Mimba utachoma Dexamethasone ili kwenda kuondoa Athari za mapafu ambazo mara nyingi huwa ni kujaa Maji



2.Ugonjwa wa miguu na kwato, huu mnyama akiupata anakuwa anasumbuliwa na vidonda kwenye midomo pamoja na kwenye kwato, na mara chache kwenye kiwele

Hivo vidonda hupelekea mnyama kutoa mate mdomoni ambayo huning'inia lakini pia hukosa hamu ya Kula maana vidonda hushambulia ulimi pamoja na kinywa chote

na mwisho kabisa mnyama akipata vidonda vya kwenye miguu hufanya ashindwe kutembea au kusimama na ata akisimama/kutembea huwa anatembea upande upande

Haya yote utayajua endapo tu utachukua muda wako na kumchunguza vizuri mnayama wako, Kwa kuanzia katika kinywa hadi miguuni, ukikuta tu vidonda mdomoni unajua kuwa huu ugonjwa ni wa kinywa na kwato hivo unaangalia na kwato pia

Endapo kama shida ndio hiyo, basi unaanza Kwa kusugua na chumvi vidonda vya kwenye kinywa hadi Damu zitoke au viwe visafi kabisa na kisha unafatia kusugua pia vidonda vya kwenye kwato kama vipo

Baada ya hapo utamchoma mnyama wako dawa ya Penstrep 20% high dose au Gentamicin 10% high dose pia au sulfa high dose pia, ila kama utatumia sulfa inabidi uchome asubui na jioni Kwa siku 3 ila hizo zingine unachoma Kwa siku mara 1

Na ikibidi ununue na dawa ya vidonda ya kuspray (wound spray) baada ya kuwa umesafisha vidonda unapulizia hiyo Kwa ajili ya kutibu vidonda lakini pia kuzuia infections ambazo zinaweza kusababishwa na kidonda

Kwahiyo zingatia hizo dalili na uhakikishe kabla ya kutumia dawa uwe umejiridhisha na uchunguzi utakaoufanya. All the best
 
Back
Top Bottom