Jicho la tatu ninalo tangu nikiwa mtoto kwa hiyo sijui nani kalifungua maana nimezaliwa hivi
Kwa mganga nilipelekwa sio kwamba nilienda mwenyewe
Kuhusu kufanya tendo la ndoa sijumbuki ni lini ila ni muda umepita
Sijawahi kunena kwa lugha ila nikisali kwa imani sana huwa nalia
Pili naomba nikwambie kwenye maombi kuna nguvu nitakuelekeza jinsi ya kumuamsha roho mtakatifu ndani yako uweze kunena kwa lugha (ila usiache na kwenda kanisani)
Ukiwa kwenye kunena kwa lugha Mungu atakuelekeza nini chakufanya.
chukua karatasi lako andika majina 3 pili chini andika unachotaka chini andika andiko utakalosimamia (nimetuka picha chini)
tafuta muda mzuri kukiwa na utulivu,
Jinsi ya kumuamsha roho mtakatifu ndani yako, nakupa njia 2
ya Kwanza play kwenye simu yako wimbo wa kuabudu na uufuate ukiimba kwa Imani (mimi huwa natumia HAUFANANISHWI wa Boaz danken au Tafuta version ya kanisani ya NIGUSE (ukinigusa wewe nitakuwa salama) ya Clorious celebration)
Wakati ukiendelea kuimba katikati wewe sema tu asante Yesu mara nyingi uwezavyo (Asante Yesu, Asante Yesu, Asante Yesu) mara nyingi....utaona unashindwa kusema asante Yesu hapo utaanza Nena Kwa lugha
Njia ya pili search YouTube video ya mwakasege search (Video hii imenitoa machozi ndugu yangu)
Kwenye hiyo video fuatilia kukiwa na utulivu, alafu anapoanza kuomba wewe useme (asante Yesu mara nyingi) utaona unaanza kunena kwa lugha
Ukianza kunena kwa lugha weka hilo karatasi chini na picha katikati uendelee kunena kwa lugha huku unazunguka chumba chako na unazunguka hilo karatasi...
Baada ya muda piga magoti na endelea kuomba Kwa Imani ukiwa unanena Kwa lugha Mungu atakufunulia na kukujibu mahitaji yako..
Mimi nilifunga nilipanga kufunga siku 7, siku ya Kwanza na yapili nilinena Kwa lugha na nilioneshwa vitu vingi, ilikuwa shida kwamaana nilioneshwa nilikuwa natakiwa kufa... so katika maombi nikawa nafukuza hao wachawi baada ya muda nilipata uchungu mkubwa nililia karibu nusu saa kwamaana nilioneshwa hao wachawi wanapanga kurudi kuniua na wakirudi Mungu wangu hatawaruhusu waishi tena nililia Sana na kuomba Mungu awasamehe kwamaana nitaishi kwahatia.
2022 sina ninachomdai Mwneyezi Mungu.