Habari zenu na pia heri ya Christmas, jaman ndugu yenu nafunga mwaka vibaya; naumwa vitu vinatembea mwilini na mwili unatikisika. Nitumie tiba gani nimehangaika hospital zote sioni tatizo.
Nimeenda kwenye maombi lakini bado kwa anaejua tiba anisaidie nipone. Halafu ajabu ni kuwa watu wengine wanatibiwa wanapona na Masheikh na Wachumgaji lakini mimi siponi sijui shida ni nini.
Au miujiza inachagua jamani, mbona sielewi?
Shukran.
Pole kwa kuumwa.
Ili kupata amani ya moyo, hii inaitwa TACTILE HALLUCINATIONS (FORMICATION). Ni matatizo yanayotokana na athari kwenye mfumo wa ubongo na afya yake. Ni tatizo mtambuka toka kwenye(ORGANIC VS INORGANIC) Maumbile vs Saikolojia vs Experience.
Unahitaji kutulia na kuhudumiwa na mtaalamu wa afya kwa kufuata mlolongo wa comprehesive managements. Huitaji kufanya vipimo hapa na pale (dedicate physician/daktari wa magonjwa ya ndani anaweza kukusaidia sana).
Mawazo ya kulogwa na.mengine ya kukutia hofu hufanya hali kuwa mbaya zaidi.
Hii huusisha:
1: Uchukuaji mzuri wa historia yako ya afya kwa ujumla.
2: Historia ya mapito yako ya zamani na sasa.
3: Saikolojia yako ya maisha na afya
4: Maisha yako kwa ujumla, kazi, familia, marafiki, dini au mahusiano na Muumba.
5: Maisha na maana yake. Malengo vs Mipango vs Ufanisi katika maisha.
6: Stress/matumizi ya pombe/matumizi ya dawa/ ulaji wa chakula ni sehemu muhimu hapa.
7: Kufanyiwa physical examination
8: Kufanyiwa vipimo kulingana na mwelekeo wa mtoa huduma nawe mtakavyokuwa mmelielewa tatizo.