Msaada tiketi ya basi inaweza kua ushahidi mahakani

Msaada tiketi ya basi inaweza kua ushahidi mahakani

dibless marco

Member
Joined
Jul 10, 2016
Posts
16
Reaction score
6
Naomba msaada sheria zinasemaje kuhusu tiketi kutumika kama ushahidi mahakaman. nimeshtaki nimemtishia mtu kumuua wakati tarehe aliyotaja kwenye maelezo yake mimi skuwepo mkoa anaodai nilimtishia yeye anadai nilimtishia tarehe 18 mwezi wa saba na mimi nimefka tar 20 mwezi wa saba tiketi pia ninayo je naweza kuitumia kama ushahid

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yes,ni ushaidi mkubwa sana huo na usiupoteze.
 
Akisema ulimtishia kupitia phone call je?

In any case it is his/her word against yours. Kama hakuna shahidi yeyote aliyekuwepo/kusikiliza vitisho vyako, itakuwa ngumu kuthibitisha. Kwa maana nyingine, hakuna kesi hapo.
 
Yeye anadai nilimtishia kwa panga maeneo ya majengo wakati mimi skuwepo huko pia anasema ana mashahidi ila mimi tar anayotaja nilikuwa sipo haya maeneo nilikuwa mkoa mwingine

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naomba msaada sheria zinasemaje kuhusu tiketi kutumika kama ushahidi mahakaman. nimeshtaki nimemtishia mtu kumuua wakati tarehe aliyotaja kwenye maelezo yake mimi skuwepo mkoa anaodai nilimtishia yeye anadai nilimtishia tarehe 18 mwezi wa saba na mimi nimefka tar 20 mwezi wa saba tiketi pia ninayo je naweza kuitumia kama ushahid

Sent using Jamii Forums mobile app
nenda kwenye kampuni ya basi ulokata tiketi ile siku..waombe wakusaidie ushahidi..kwani kwenyw vitabu vuao wakikata tiketi chini kunabaki maandishi..au konda wa basi ile siku unasafiri awe shaodi ako..
usikubali kuonewa.
chukua hata mdugu wa karibu waliojua kuhusu safar yako waksseme ukweli mahaksmani
 
Pole sana na pia pongezi kwa wote mliotoa msaada na ushauri. Ila hapo unachokizungumza mleta mada kwenye sheria inaitwa defense ya alibi (inasomeka alabai au alibi hivyohivyo). Hii ni defense kuonesha kuwa siku ya tukio hukuwepo eneo la tukio, ili itumike mahakamani ni lazima uutaarifu mapema (kwa maandishi) upande wa pili kuwa unakusudia kutumia hiyo defense ya alibi..
Sababu kuu ya kuwataarifu ni hii; tofauti na wengi walivyosema kuwa ukaombe manifest kwenye kampuni ya basi nk kuthibitisha kutokuwepo kwako, kisheria upande wa pili ndio wanaotakiwa kuthibitisha kuwa ulikuwepo eneo la tukio wakati tukio likifanyika na sio wewe kuthibitisha kuwa hukuwepo eneo hilo.. Hivyo unawapa taarifa ili wajiandae kuthibitisha kuwa ulikuwepo eneo la tukio.. Ni muhimu lakini kuwa na tiketi na vielelezo vingine (kama hiyo manifest nk)
 
Wakati wa kujitetea ndio useme hukuwapo. Achana na kusema hukuwapo kabla haijafika zamu yako ya kujitetea. Watauhujumu utetezi wako.

Sent using Jamii Forums mobile app
upo sawa mkuu, acha kwanza wajieleze wao mpaka mahakama itakapotoa uamuzi kwamba una kesi ya kujibu au la...ukiambiwa una kesi ya kujibu na hivyo ujiandae kujitetea ndipo utakapotoa hilo wazo kuwa utatumia defense ya alibi, kwa hiyo bado una muda wa kutosha tu
 
Nashukuru sana kwa wote walionipa msaada wa kisheria. Lakini pia naomba kujua je ni maswali gani ninayopaswa kuwauliza mashahidi watakaoletwa mahakamani ktk kesi hiyo????

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nashukuru sana kwa wote walionipa msaada wa kisheria. Lakini pia naomba kujua je ni maswali gani ninayopaswa kuwauliza mashahidi watakaoletwa mahakamani ktk kesi hiyo????

Sent using Jamii Forums mobile app
Ushahidi wa kuona ni ushahudi mzuri. Utamuuliza shahidi hilo panga uliloshikilia ukimtisha mlalamikaji ulikuwa unelishika mkono gani wa kulia ama kushoto? Atajibu......

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kisha utamuuliza wakati anakuona alitumia darubini? Maana kumwona mtu aliyeko Mwanza akimtishia kumkata mtu panga wa Dar wakati mtkataji panga 6 akiwa Mwanza yataka uwe na darubini. Na hilo panga yaelekea ni aiba ya kombora maana panga kutoka Mwanza mpaka Dar ili liweze kumkata mtu linahitaji mtambo wa kurushia kombora.

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji3][emoji3]
 
Nashukuru Mr Malyenge, umenipatia jibu zuri sana anbalo naweza kulitumia siku ya kesi. Pia naomba maswali zaid ninayoweza kuuliza siku hiyo. Pia nilipanga kuuliza mashahidi kama wananifahamu na ni kwa muda gani wananifahamu na wananifahamu kama nani, je niswali sahihi la kuuliza???

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni ushahidi very strong, Inaitwa Kisheria "DEFENSE OF ALIBI"
 
Back
Top Bottom