Msaada: Tofauti ya maneno haya,

Msaada: Tofauti ya maneno haya,

Chemiker

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2013
Posts
506
Reaction score
108
Usifikiri kila anayekuangalia anakutazama tu.

Je, kuna tofauti gani kati ya kuangalia na kutazama?
 
Najaribu....
Kuangalia = To scan (kuchunguza,kulinda)
kutazama = To look (nadhra,mtupio,)

kama unajibu nitafurahi kutujuza hapo.
 
usifikiri kila anayekuangalia anakutazama tu.

Je, kuna tofauti gani kati ya kuangalia na kutazama?

usifikiri kuwa anayekuangalia anishia kukuangalia tu, hapana anafanya kitu kingine cha zaidi ya kukuangalia.
 
kwanza kuna 'kuangali' ,'kutazama', na kuona. Tendo la kwanza ni kuona, ukishaona ndio unaangali! Vile vile unaweza 'kuona' lakini 'usiangalie' kwa mfano unapita ukaona vijana wanacheza mpira lakini usiangalie. Pia unaweza kuangalia lakini usione! Kwa mfano, mpo wa3, mnaangalia mwezi ulioandama wenzako wakaangalia wakaona na wewe ukaangalia lakini hukuona. Kutazama (watch) ni tendo la kutulia na kuangalia ama mpira,hata Tv.
 
Ndugu Ziroseventytwo Nakupa kongole kwa maelezo yako murua.
 
Usifikiri kila anayekuangalia anakutazama tu.

Je, kuna tofauti gani kati ya kuangalia na kutazama?

Kuangalia ni kukitazama kitu na kukitilia maanani mfano mtu anakuambia naomba nisaidie kuangalia begi langu.
Kutazama ni hali ya kuona kuelekea mbele , nyuma kwenye kitu n.k
 
kutazama ni kuangalia kwa makini. kuangalia ni kuelekezea kitu macho kwa lengo la kukiona. Kutazama ni kuona kitu katika mazingira yake na kumakinika na uwepo wacho.
 
kwanza kuna 'kuangali' ,'kutazama', na kuona. Tendo la kwanza ni kuona, ukishaona ndio unaangali! Vile vile unaweza 'kuona' lakini 'usiangalie' kwa mfano unapita ukaona vijana wanacheza mpira lakini usiangalie. Pia unaweza kuangalia lakini usione! Kwa mfano, mpo wa3, mnaangalia mwezi ulioandama wenzako wakaangalia wakaona na wewe ukaangalia lakini hukuona. Kutazama (watch) ni tendo la kutulia na kuangalia ama mpira,hata Tv.

Maelezo ni mazuri lakini nadhani Kutazama sio ku-watch ni ku-look. Ukumbuke ku(watch) inahitajika kutilia maanani (pay attention) unachokiona. Unaweza kutazama kitu bila ya kutilia maanani unachokiona. Kwa maana hiyo mfano wa kuangalia ni vile unavyokaa mbele ya Tv.
 
Back
Top Bottom