Hismastersvoice
JF-Expert Member
- Jan 26, 2013
- 24,523
- 30,084
Mtu muhimu sana kwenye uraia wako ni mama yako na bibi yako, taarifa za mama yako yaani jina lake kamili na aliko kuzalia, yaani yeye ni mtanzania alikuzalia Kenya ujue wewe si mtanzania ukishindwa hapo basi pasipoti utaisikia tu.Waheshimiwa, habari ya kazi na pole kwa majukumu.
Waheshimiwa, mwaka jana 2023, nilibahatika kupata ufadhili wa kwenda masomoni nje ya nchi hivyo nililazimika kutafuta passport. May 2023, nilifika ofisi za uhamiaji Kurasini na viambatanisho vyangu vyote kufanya ombi la passport. Nilifanikiwa kukamilisha ombi langu na kulipia gharama zote.
Waheshimiwa, toka May 2023, hadi sasa sijapata passport. Nilipojaribu kufatilia niliambiwa siwezi kupata passport kwa sababu mimi sio Mtanzania.
Waheshimiwa, mimi nimezaliwa, kukua na kusoma ndani ya mipaka ya Tanzania kama viambatanisho vyangu vinavyoonyesha. Wazazi pamoja na babu zangu ni watanzania.
Waheshimiwa, nimefanya jitihada zote pamoja na kuleta wazazi kutoka kijijini na kwenda nao uhamiaji bila mafanikio. Nimeingia gharama kubwa sana kufuatilia hili swala ukizingatia mimi ni kijana niliyemaliza chuo na bado sijabahatika kupata kazi. Kadhalika kuna uwezekano nikapoteza ufadhili niliobahatika kuupata kama sitapata passport kwa wakati; ndoto na maisha yangu kiujumla yataharibika kwani elimu ndio tegemeo langu kujikwamua kiuchumi.
Waheshimiwa nimekuwa ni MTU wa mawazo sana pamoja na misongo. Naombeni msaada wenu kutokomeza ukosefu wa haki katika nchi hii.
Ni mimi kijana mwenzenu Mwenyezi Mungu awabariki mnapoendelea na majukumu ya ujenzi wa taifa.
Nikweli wazazi wanatokea kigoma. Mimi nimezaliwa moroItakuwa umetokea Kigoma mkuu. Nina rafiki yangu yeye ni wa kigoma nae walimsumbua sana ila alipata baada ya kuhangaika sana
Huo mkoa ni changamoto sana uhamiaji kwa sababu ya wakimbizi. Pole sana mkuu Mungu akufanyie wepesi.Nikweli wazazi wanatokea kigoma. Mimi nimezaliwa moro
wanaangalia kwani unadhani hawaogopi fujoMbona mimi huu upuuzi sikumbani nao? Yaani mjinga mjinga fulani kwa upuuzi wake aniambie mimi sio mTz.
msaidie tuPole, Natamani ningekusaidia, ila nina uhakika utapata usaidizi wa haraka hapa hapa JF
1.MorogoroOh sawa twanzie hapo walipokwambia we si mtanzania
nataka kufahamu haya
Hebu jibu kwanza haya then tuone njia ipi itafunguka
- Umezaliwa mkoa gani
- Kabila lako
- Umesoma shule ya msingi ipi kwa jina na iliyopo mkoa gani na wilaya.
- Wazazi wako wapo wapi.
π π kwa kweli afanyiwe wepesiHuo mkoa ni changamoto sana uhamiaji kwa sababu ya wakimbizi. Pole sana mkuu Mungu akufanyie wepesi.
Uzi uishie hapa.Kuna mtu anataka Rushwa. Mtafute umjue.
Kuna jamaa tulikuwa naye jeshini alikoswa kazi kisa katoka kigoma,na lisura lake lilifananishwa na warundi,alirudi home kabisa hadi leo anasota uraiani.Nikweli wazazi wanatokea kigoma. Mimi nimezaliwa moro
Ulitaka kumpa asante ya kitu gani huyo Baba?Pole sana, mimi nilihangaika sana kupata hapa Mwanza nikaombwa hadi rushwa ya ngono nikakataa, nikasema kama kupata passport ni kazi hivi basi siitaki.
Nikapata kazi Dodoma nikaomba migration ya Dodoma nikaunganishwa na baba mmoja hivi hapo Migration hakuniomba chochote niliombwa Doc za sababu ya kusafiri, G akanitumia barua ya mwaliko na passport copy yake ndani ya wiki mbili nikapata passport, nikasema nimpe asante yule baba aliikataa kata kata akasema nimekusaidia tu.
Tafuta mtu akuunganishe utaipata haraka tu
ππππSasa ili wakuthibitishe Kuwa wewe ni Mtanzania unatakiwa uwapelekee Tunu kadhaa za Taifa ambazo ni currencies za kitanznia (Fedha halali) ili waamini kweli wewe ni mtanzania..
Vinginevyo hutaweza kupata unachokitaka