Msaada TTCL Copper Internet

Hili u-enjoy yapasa kutokuzidi watu wangapi(device ngapi) wanaotumia kwa pamoja !?

Nataka kufungia familia.
Inategemea na matumizi na speed unayotumia, 4mbps watu wawili munaweza tumia kwa mpigo hata kama wote mna stream.
 
Njoo TTCL mzee baba. Inategemea unataka COPPER au FIBER?
Kama ni Fiber bei ni kama ifuatavyo;
20/10 Mbps ni 55k
40/20 Mbps ni 100k
60/30 Mbps ni 150k
100/50 Mbps ni 200k

COPPER Internet ni nafuu na gharama zake ni kama ifuatavyo;
4Mbps ni 25k
8Mbps ni 50k
12Mbps ni 80k

UFUNDI ni Bure na utafuatwa mpaka hapo ulipo.
Kuhusu vifaa inategemea kama una haraka nunua kwa pesa yako kama unasubiria tukuletee vifaa vya bure uvumilivu wako ni muhimu.
 
Kama wewe ni muhusika wa kampuni basi weka namba ya simu hapa tufanye mambo serious
 
Ndugu, maelezo uliyo yatia hapo juu ni kweli kabisa. Mimi huku naishi Sinza A opp na Mlimani City, nilikuwa natumia hiyo ya copper ambayo inaitwa Broadband tokea 2012 - 2013 baadaye nikaja tena kuitumia 2018 - 2019.

Hali ilikuwa vile vile inakuwa ON/OFF ilikuwa ina umiza sana unakuta unalipia inakata wiki 2 mpka 3 na nilikuwa nalipia ya BRONZE SILVER cha Tshs 66,500/ cha speed ya 2MBPS.

Nikiwa zangu nyumbani mwezi wa 8 tarehe 04 hivi majira ya mchana natoka nje, nikakutana na mafundi nje wa TTCL wanaweka nyaya za FIBRE nikawauliza mnaweka nn wakasema tunaweka nyaya za FIBRE nikawauliza si nasikia kuwekewa ni mpka uwe na 1Mil wakasema hiyo ilikuwa zamani lakin sasa Mama ameondoa hizo gharama sasa kuwekewa ni bure, na unawekewa popote pale ulipo.

Nikasema, OK basi naomba mnidondoshee basi huo waya kwangu, wakaniwekea tena hadi ndani nyumbani ni waya mnene na mgumu sana kukunjika, na wakaniambia nikalipe makao makuu yangu ambayo ni hapo tu Sayansi KijitoNyama waje mafundi wanifanyie connection nipate huduma.
 
Daah mimi nilifosi yani hata hiyo ya ON/OFF niliona poa tu kuliko daily shit ya mitandao ya simu

Lakini zoezi likashindikana wakanikomalia kuwa hawawezi kufunga huduma ambayo sio ya uhakika.
 

Umefanikiwa kupata huduma?
 
Kigamboni mpo mkuu
 
Manzese Midizini hapa Nimewatext jamaa zako uliosema ni wa Survey kwa zile no ulizonipa hata kujibu hawajibu
Wee jamaa nimekutafuta sana mpaka nilikata tamaa nikajua huduma umeshafungiwa kumbe upo kimya kabisa.

#RudiNyumbaniKumenoga
 
Mkuu, fiber hii nipo chamazi huku napata ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…