KERO Msaada: Tuliotoka Diploma kwenda Degree tukiomba mkopo tunakutana na "No Applications Found" kwenye mfumo

KERO Msaada: Tuliotoka Diploma kwenda Degree tukiomba mkopo tunakutana na "No Applications Found" kwenye mfumo

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Naomba kuwasilisha changamoto inayowakabili waombaji wengi wa mkopo wa HESLB, hasa sisi tuliotoka Diploma kwenda Degree.

Kutokana na kuchelewa kwa matokeo ya Diploma, tuliopo kwenye kundi hili tulipewa siku 14 za ziada ili kukamilisha maombi yetu ya mkopo. Muda huo ulikuwa unatosha, na hatuombi kuongezewa muda.

Tatizo limeanza Ijumaa, tarehe 11 Septemba 2026, ambapo mfumo wa OLAMS umeanza kuleta changamoto kwa waombaji wengi. Baadhi yetu tukiingia kwenye akaunti tunaoneshwa “No Applications Found”, hivyo tunashindwa kuendelea na kukamilisha maombi. Mimi binafsi nilikuwa nimefika hatua za mwisho kabisa za maombi kabla ya kukutana na tatizo hili.

Kinachotia wasiwasi zaidi ni kwamba muda wa mwisho wa maombi unaendelea kukaribia. Tovuti rasmi ya HESLB imeonyesha deadline ni 14 Septemba 2026, huku countdown ikiendelea kuhesabu muda uliobaki.
Kwa waombaji wengi, hasa wanaotoka kwenye familia zenye uwezo mdogo, mkopo wa HESLB ndiyo tumaini la kuweza kuendelea na Degree. Ni jambo linaloumiza kuona nafasi ya kukamilisha maombi inaweza kupotea kutokana na tatizo la mfumo ambalo si kosa la mwombaji.

Tunaomba HESLB itoe ufafanuzi na kurekebisha mfumo wa OLAMS haraka, ili waombaji waliokwama waweze kutumia muda ambao tayari wamepewa kukamilisha maombi yao.

Hatuombi kuongezewa muda; tunaomba mfumo ufanye kazi ili tutumie muda tuliopewa.

markup_1000118323.png

Saver Error.jpg


Saver Error.jpg

Save 11.jpg
 
Mimi mwanzo ilikuwa inasema maombi yako yamepokelewa ila sasa inaonesha click to appeal.
 

Attachments

  • Screenshot_20260914-222725_Chrome.jpg
    Screenshot_20260914-222725_Chrome.jpg
    21.6 KB · Views: 12
You know, sisi binadamu mara nyingi hatuna shukrani hata kidogo. Kwa kidogo tunachopata, hatujawahi kushukuru wala kupongeza.

Hivi unajua kwamba tarehe ya mwisho ya maombi ilikuwa 31 Agosti? Hizo siku 14 zilizoongezwa zilikuwa ni favor—yaani nafasi ya ziada ambayo mtu hakuwa na uhakika wa kupewa.

Sasa unataka kuilaumu Bodi kwa hizo siku tatu ambazo walifungua tena dirisha, wakati awali walitoa muda wa miezi mitatu, sawa na siku 90, na wakaongeza tena siku 14? Bado unaona ni sahihi kuwalaumu kwa changamoto zilizojitokeza katika hizo siku tatu za ziada?

Embu tuwe na shukrani kwanza. Kama mtu ameshindwa kuomba ndani ya siku 100, basi hizo siku tatu za ziada zisiwe sababu ya kuipuuza au kuondoa thamani ya kazi iliyofanywa na Bodi. Ndiyo maana wamewapa nafasi pia wale ambao maombi yao yalikuwa tayari kwenye hatua ya progress.

Anyway, tunaweza kuwa na maoni tofauti. Endelea kuwalaumu kama unaona inafaa. Uzuri wa nchi huru ni kwamba kila mtu ana haki ya kuwa na maoni yake. Muhimu ni kwamba hoja zenye uzito zisikilizwe na, pale inapobidi, zifanyiwe kazi.
 
Back
Top Bottom