Msaada: Ubora wa magari ya Be Forward

Msaada: Ubora wa magari ya Be Forward

The Tomorrow People

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2013
Posts
2,675
Reaction score
2,807
Wakuu,

Kwenye pita pita zangu, nimebahatika kupata pesa, nikaona sio mbaya na mimi ni ongeze foleni ya magari.

Kimsingi nimeshaanza mawasiliano na watu wa beforward, ila kuna mdau kanitonya hawa watu mara nyingi gari zao zinakuja zikiwa mbovu. Ni either shock up zimekufa au parts zingine.

Naombeni ushauri, Kama kuna ukweli katika hili.

Gari nyingi za be forward siyo mbovu ila watakuuzia gari kutokana na hali halisi ilivyo. Kama ni mbovu ni lazima utaonyeshwa ila kama ukiridhika basi ukinunua huwezi kulaumu be forward tena.

Mimi nilinunua kwao Suzuki Carry its was my first time lakini gari ilifika kama nilivyoiona kwenye mtandao.
Cha msingi hasa kama unataka saloon cars basi ukitafuta utaipata. Kingine na cha msingi unatakiwa kabla hujaamua kufanya maamuzi uwe na picha ya gari katika angle zote ili uweze kutoa maamuzi sahihi.
Kwa maelezo zaidi ni inbox tutawasiliana.
 
Rahisi ni aghali,

hizo kampuni zina Siri kubwa ila wa bongo uelewa mdogo,
 
Gari nyingi za be forward siyo mbovu ila watakuuzia gari kutokana na hali halisi ilivyo. Kama ni mbovu ni lazima utaonyeshwa ila kama ukiridhika basi ukinunua huwezi kulaumu be forward tena.

Mimi nilinunua kwao Suzuki Carry its was my first time lakini gari ilifika kama nilivyoiona kwenye mtandao.
Cha msingi hasa kama unataka saloon cars basi ukitafuta utaipata. Kingine na cha msingi unatakiwa kabla hujaamua kufanya maamuzi uwe na picha ya gari katika angle zote ili uweze kutoa maamuzi sahihi.
Kwa maelezo zaidi ni inbox tutawasiliana.

.Kuna kitu wanaita "as is condition" hivyo kama ulivyosema, utachukua kama ulivyoikuta/ilivyo, muhimu ni kuiangalia kwa makini picha za gari tarajiwa
 
....ukitaka kununua gari unatakiwa kufanya uchunguzi wa kina kabla ya kuchagua gari. `Unatakiwa kuwa na ufahamu mpana wa kuchunguza picha za hiyo gari kwa pande zote, pia picha za uvunguni mwa gari pande zote ni muhimu sana, husisahau kuangalia kilometers na mwaka.

NB;BF wanauza magari ya kila aina zote yenye ubora kufuatana na fedha yako, [ukiwa na pesa ya kutosha utapata gari iliyo nzuri na bora]
 
Vipi kuhusu kampuni ya autocom jp? Aliewahi kufanya nao biashara anipe ujuz
 
Vipi kuhusu kampuni ya autocom jp? Aliewahi kufanya nao biashara anipe ujuz

Autocom still ni kampuni mpya ambayo inajenga jina, Niko na rafiki zangu wamenunua Gari huko, and so far it's the best kuanzia wafanyakazi mpaka kupata Gari Yako, wajaribishe, 📞 0767328063 au tembelea office zao @ Quality Center, uliza jamaa anaitwa Msuya.
 
Nimejaribu kuangalia hii kampuni. Kwa ujumla magari yake mengi yametembea km nyingi sana mengi kuanzia km130000-270000. Hivyo ni vizuri kufanya market survey vizuri..
 
Habari yako,

Mimi kama mmoja ya watu niliyewahi kuagiza magari marakadhaa, nimepata pia kusikia malalamiko marakadhaa kutoka kwa mawakala kuwa magari mengi ya BFOWARD yanakuja yakiwa sio sawa. Ingawa watu wengine huchukua tu.

Nakushauri utumie TRADECARVIEW kwani hawa wanakitengo ambacho watakagua gari yako kabla hujatuma na kukupa feedback kuwa iko poa au lah. ingawa utalipia kama $150 kwa huduma hii.

TRADECAR VIEW sio maagent wa kuuza magari wao wanasimamia, wanakuunganisha na muuzaji kisha wanasimamia mpaka gari yako unaipata na hata malipo ukilipa huwa wanakaaa na hela zako mpaka umepata gari yako kisha ndo wanamlipa muuzaji.

Otherwise wanakurudishia hela yako.
 
habari yako,

mimi kama mmoja ya watu niliyewahi kuagiza magari marakadhaa, nimepata pia kusikia malalamiko marakadhaa kutoka kwa mawakala kuwa magari mengi ya BFOWARD yanakuja yakiwa sio sawa. ingawa watu wengine huchukua tu.

Nakushauri utumie TRADECARVIEW kwani hawa wanakitengo ambacho watakagua gari yako kabla hujatuma na kukupa feedback kuwa iko poa au lah. ingawa utalipia kama $150 kwa huduma hii. TRADECAR VIEW sio maagent wa kuuza magari wao wanasimamia, wanakuunganisha na muuzaji kisha wanasimamia mpaka gari yako unaipata na hata malipo ukilipa huwa wanakaaa na hela zako mpaka umepata gari yako kisha ndo wanamlipa muuzaji. otherwise wanakurudishia hela yako.
Mkuu kutoka mwezi Mei 2015 huduma ya PayTrade ni bure, hivyo jamaa atakaguliwa gari lake na kupewa assurance mpaka linapofika na kukabidhiwa akiwa ameridhik nalo. Pia jamaa wameboresha site yao ambapo now CIF price ipo moja kwa moja ingawa mnunuzi bado amepewa nafasi ya kunegotiate na muuzaji kuhusu kupunguziwa bei tofauti na beforward ambako bei iliyopo ndio hiyohiyo unayotakiwa kulipa The Tomorrow People acheki CARVIEW corporation aone bei zao, akiridhika anunue hapo pia
 
Last edited by a moderator:
The Tomorrow People

Magari ya hawa jamaa hayana ubovu wowote zaidi ya ule wa vifaa kuisha muda wake..vitu kama betri au oil japo sio mara nyingi..cha msingi ni kuziangalia picha kwa makini na kukonsida vitu kama mwaka wa gari na umbali liliotembea
 
Last edited by a moderator:
Hongera kwa wazo zuri namna hyo gar ni gar tu hata iwe mbovu haiwezi kuitwa baskeli au pikipiki hata usiogope we nunua tu
 
Watz tuna mambo na kujitia wajuaji. eti chunguza sana kila upande wa gari hii inamaana gani, umejiandaa kununua gari au unanunua gari kwa majina ya wafanyabiashara ya magari kama una wacwac basi nunua ya hapahapa yaliyotumika na ukiambiwa kuwa hili ni zuri sana litakufaa nunua. magari yote yanayouzwa na makampuni toka nje yalishatumika, angaliua mwaka wa kutengenezwa na umbali uliotumika, vinginevyo wewe nunua matumizi ya ulaya ni tofauti na wabongo mtadanganyana kama yote hutaki bac nunua pkpkp foleni haitakusumbua DADA Mpendwa.
 
Mkuu kutoka mwezi Mei 2015 huduma ya PayTrade ni bure, hivyo jamaa atakaguliwa gari lake na kupewa assurance mpaka linapofika na kukabidhiwa akiwa ameridhik nalo. Pia jamaa wameboresha site yao ambapo now CIF price ipo moja kwa moja ingawa mnunuzi bado amepewa nafasi ya kunegotiate na muuzaji kuhusu kupunguziwa bei tofauti na beforward ambako bei iliyopo ndio hiyohiyo unayotakiwa kulipa The Tomorrow People acheki CARVIEW corporation aone bei zao, akiridhika anunue hapo pia

Umenena vyema mkuu... Mi nimenunua gar 2 noah na ist CARVIEW kwakwel hawajanilet down wakko poa sana
 
Last edited by a moderator:
Mkuu kutoka mwezi Mei 2015 huduma ya PayTrade ni bure, hivyo jamaa atakaguliwa gari lake na kupewa assurance mpaka linapofika na kukabidhiwa akiwa ameridhik nalo. Pia jamaa wameboresha site yao ambapo now CIF price ipo moja kwa moja ingawa mnunuzi bado amepewa nafasi ya kunegotiate na muuzaji kuhusu kupunguziwa bei tofauti na beforward ambako bei iliyopo ndio hiyohiyo unayotakiwa kulipa The Tomorrow People acheki CARVIEW corporation aone bei zao, akiridhika anunue hapo pia

Hata Beforward unaweza negotiate bei. Nilinunua gari huko kikafika December mwaka jana. Hadi sasa nabadili engine oil na engine coolant tu na check up ndogo ndogo. Ukitaka ku negotiate bei, unajaza details zako ikiwemo email address.Baada ya hapo makubaliano huhamia kwenye email address ambako negotiations hufanyika. Gari nililonunua walishusha kama $200.
 
Last edited by a moderator:
Nimejaribu kuangalia hii kampuni. Kwa ujumla magari yake mengi yametembea km nyingi sana mengi kuanzia km130000-270000. Hivyo ni vizuri kufanya market survey vizuri..

Hili suala lipo hata Beforward na SBT. Kwa Beforward ipo hivi: Kuna document fulani ya rangi ya blue ina maandishi ya kijapan na kiingereza. Ukiyasoma vzr utaona kwenye ile document wamelist watu wote waliomiliki hilo gari. Sasa unawekewa kwenye web limetembea 35000km, ukajipa moyo, angalia kwenye hiyo document baada ya gari kuwa njiani, utaona wa kwanza alitembea km laki na nusu, wa pili akatembea 35000 nae akaliuza, ww inakuja kuwa mmiliki wa 3. Nilisoma document ya gari fulani ambalo waliandika 96000km, ila mmiliki wa kwanza alitembea 92000, jumlisha hizo utapata jibu. Ila engine bado iko poa kbs.
 
Befoward. gari ina mwaka wa tatu
nakaa kimara. zaidi ya oil hakuna nilichobadilisha. uchaguzi wako na zali lako tu jombaaa.
 
Back
Top Bottom