Msaada: Ufahamu kuhusu madini

Msaada: Ufahamu kuhusu madini

mkuu sio kweli kuwa red garnet ndio ina bei kuliko gemstone zote, green garnet iko juu mara nyingi sana ya hiyo red garnet,,,,,,,,,,, hizo red garnet ziko nyingi sana kule ruangwa-lindi na zinauzwa kwa kilo tu
acha masihara mkuu!kilo!
 
red garnet ipi hiyo mzee? Red garnet ninayoijua mimi kwa jina jingine inaitwa "almandite" ndugu yake na pyrope bei yake iko chini sana, na unaweza ukauziwa kilo 1 kwa bei ndogo sana-hata million 4 haifiki. Angalau rose/pink garnet in bei lakini bado siyo ya kutisha

aina ya garnet iliyo ghali sana inaitwa green garnet ambayo inapatika landanai na msitu wa tembo kule arusha.

abaakana! Mimi nilichokoza mada tu.sikuwa na uhakika wa kutosha.ila hata hivyo nilidhani madini haya ya red garnette yana thamani kubwa sana kumbe....!
 
acha masihara mkuu!kilo!

Mkuu unashangaa, hayo yanuzwa kwa kilo na sio jiwe mojamoja, hayana hiyo thamani uliyoambiwa au uliyonunulia,

Biashara ya madini hasa Gemstone, ni biashara hatari sana, kama hauna ujuzi nayo acha kabisa kuingia, hiyo biashara siku moja unaweza kujikuta ni tajiri sana na kesho ukawa ni maskini kabisa
 
mkuu unashangaa, hayo yanuzwa kwa kilo na sio jiwe mojamoja, hayana hiyo thamani uliyoambiwa au uliyonunulia,

biashara ya madini hasa gemstone, ni biashara hatari sana, kama hauna ujuzi nayo acha kabisa kuingia, hiyo biashara siku moja unaweza kujikuta ni tajiri sana na kesho ukawa ni maskini kabisa
hivi hizi germstones zinatakiwa ziwe na thamani kiubwa kuliko madini kama almasi shaba na kadhalika au inakuwa je?
 
Habarini wana jf wote:

Wana jf ninataka kujiajiri kwenye secta ya madini lakini hasa kwenye dhahabu na hata aina nyingine ya madini ya vito...

Kwa sasa siyajui maeneo wanapouza,hivyo ninaomba ushauri wenu kwa walio na ufaham na hata waliofanya na wanaoendelea kufanya shughuli hizi.Ninaomba ushauri katika mambo yafuatayo:

1:changamoto za biashara yenyewe
2:sehemu ninapoweza kupata madini hayo na aina yenyewe
3:usalama wa eneo unaloshauri nifike
4:Upatikanaji wa usafiri na barabara
5:maeneo yenye madini ambayo bado hayajamilikishwa ili ikiwezekana ninunue eneo na kuwa na machimbo yangu
na mengineyo unaweza ongeza

Aliye na taarifa sahihi tunaweza wasiliana kwa kuni-pm,nitawashukuru kwa ushauri mzuri mtakaonipa
 
Bei ya Tanzanite navyo uzagaa na kununua IMG-20140926-WA0000.jpg mimi 1 gram single laki mbili mpaka 3 na nusu na inategemea na rangi na shape..kama unagram kuwanzia gram 5 na kuendelea ilioshikana rangi nzuri na shape nzuri bila tatizo kama viwembe yani mikatiko ndani ya jiwe(Tanzanite) bie yake ni nzuri sana kuwanzia 1.8m mpaka 2m per 1 gram
 
Bei ya Tanzanite navyo uzagaa na kununuaView attachment 213871 mimi 1 gram single laki mbili mpaka 3 na nusu na inategemea na rangi na shape..kama unagram kuwanzia gram 5 na kuendelea ilioshikana rangi nzuri na shape nzuri bila tatizo kama viwembe yani mikatiko ndani ya jiwe(Tanzanite) bie yake ni nzuri sana kuwanzia 1.8m mpaka 2m per 1 gram

Whaaaaatt!!! Tanzanite iko na bei hivo?
 
Bei za Ruby : Ruby zote zisizopitisha mwanga (cabochon), ruby nuts, Ruby in Zoisite, Tsavorite etc bei inaanzia dola 10 mpaka dola 500 kwa gram. Ruby yenye kuona, haina chenga, rangi nzuri (pigeon blood ) imekatwa au bado bei inaanzia dola 5,000 mpaka 25,000 kwa jiwe lisiozidi karati mbili. Kwa rough bei inaanzia $ 25000 kwa gram. Bei halisi inategemea na shape ya jiwe, colour, clearity na grade. Wewe una Ruby za aina gani?

Mkuu haya makitu yanapatikana wapi tukajitoe umaskini? Na vipi kuhusu diamond bei yake kwa gram.
 
Duuuuuuuu hadi inakua raha sana kwa dondoo kama hizi wakuu niulize SEMIKI ipo wapi?
 
Tanzania ina madini mengi na ya thamani kama: Ruby, saphire, emarald, diamond, alexandrite, Tanzanite, etc
bei ya madini inategemea na :hardness, size, colour, clearity, na kama yamekatwa na aina ya mkato e.g. brilliant, cushion, oval, table cut etc. Madini yenye bei kubwa kwa Tanzania ni Diamond ikifuatiwa na ruby, emarald, saphire, alexandrite na Tanzanite.
NB. Ruby zipo za aina tatu: red, rose na pink ruby. red ruby ndiyo ya ghali zaidi.

We mshenzi unajua hayo madude hadi raha!Unavyoyachambua kama umezaliwa nayo kwenye udongo.
 
Hi!
ndugu wana jamvi hili
Naomba nitoeni kwenye kashimo haka, hivi ni madini gani Duniani yenye gharama kubwa
Ni madini gani yana bei kubwa yanayopatikana Tanzania
Madini aina ya Ruby ni madini ya aina gani na je ghalama yake ikoje kwa gram moja?

Msisahu kuniambia wapi kwa Dar maduka ya kununua madini?

Nenda STAMICO au ni PM nikutonye
 
Madini ghali ni alexandrite itakuwa...Nakumbuka nikiwa na miaka 15 enzi hizo tunduru inawika nilikuwa huko na mjomba wangu mmoja, ilisemekana kuna jamaa aliyapata na kuna mnunuzi mthailand wakati huo alikuwa hapa tz anaitwa tom mine alikuwa ga na ofisi Upanga ali shindwa fika offer mpaka kuna mzungu mmoja maarufu kama john almasi alikuja na private jet tz akaja linunua...na akatambaa
 
Madini ghali ni alexandrite itakuwa...Nakumbuka nikiwa na miaka 15 enzi hizo tunduru inawika nilikuwa huko na mjomba wangu mmoja, ilisemekana kuna jamaa aliyapata na kuna mnunuzi mthailand wakati huo alikuwa hapa tz anaitwa tom mine alikuwa ga na ofisi Upanga ali shindwa fika offer mpaka kuna mzungu mmoja maarufu kama john almasi alikuja na private jet tz akaja linunua...na akatambaa

Mkuu unataka sema hii jiwe inazidi hata bei ya diamond?
 
Wadau, kwa anaefahamu thamani ya madini
ya Rubi.
vilevile ni madini gani kwa jina yana sura zifuatazo.
1. rangi ya njano.
2. rangi ya chupa ya sprite
3. rangi ya blue
4. rangi nyeusi kama mkaa ila inayomeremeta
5. rangi nyeusi iinayong'aa ila inanata kwenye sumaku
6. rangi nyeupe ila ni transparency kama kioo.

Naombeni mwenye uelewa wa mambo haya ya madini. Nipo makini kwa kua nikienda kichwa kichwa ntapoteza pesa na hayo madini kwa kutapeliwa. anayefahamu naomba msaada wa mawazo
 
Mkuu vema kama ungeambatanisha na picha ili upate majibu kutoka kwa watu yenye uhakika (ni ushauri tu)
 
Madini yana properties zake pamoja na color texture grain size inner structure n.k hiyo rangi siyo kigezo cha kusema ni aina gani ya madini. Ngoja wataalam waje nishasahau
 
Back
Top Bottom