Msaada ugonjwa wa kupungukiwa damu

Msaada ugonjwa wa kupungukiwa damu

Kuna dada alijifungua mtoto miezi mitano iliyo pita sasa ameshikwa na ugonjwa wa kupungukiwa damu sana kila akienda hospital anaingezewa damu lakini siku iyoiyo inakeisha tena na madaktari wamempima kila kitu haonekani na tatizo lolote sasa kwann damu inakauka tu??
Ni vema kama ungetuma majibu Maana kuishiwa damu siku hiyo hiyo haiwezi kuwa Parasitic Infection wala any infestation kama wengi wanavyodhani kuwa ni Nutrients deffiecient...

Haileti picha Ya Anaemia ya kawaida...
Anaemia yenye mlengo huo mara nyingi huwa ni
  • Leukemia
  • Internal Haemorrhage
  • Sickler case (Sickle cells Anaemia)
Cha msingi Wakupe majibu ya...
  • FBP/WBC
  • Bone marrow aspirate(kama walifanya biopsy) tuone structure na maturity ya blood cells
Bila kufanya hivyo wengi tutakuwa tunapiga ramli tu
 
Kuna dada alijifungua mtoto miezi mitano iliyo pita sasa ameshikwa na ugonjwa wa kupungukiwa damu sana kila akienda hospital anaingezewa damu lakini siku iyoiyo inakeisha tena na madaktari wamempima kila kitu haonekani na tatizo lolote sasa kwann damu inakauka tu??
Poleni.

Mwaka 2014 kuna dada alipata tatizo kama hilo la kupungukiwa damu kila inapoongezwa. Alipata na upofu pia, ikiwa ni miezi 6 baada ya kujifungua.

Huyo dada alifariki dunia. Sababu haikua ya kidaktari, ilisemwa kuwa alizaa na mume wa mtu (alimuiba huyo jamaa) ambae mkewe alikuwa amemsihi huyo dada amuache ili walau asomeshe hata watoto tu, lakini dada alikaza.

Awali dada (marehemu) na huyo jamaa walitaka kufunga ndoa Mbeya lakini makanisa yaliwakataa baada ya mke kuweka mapingamizi, basi wakaenda Morogoro na kufanikiwa kufunga ndoa. Waliporudi Mbeya yule dada akawa anamtambishia mke wa awali kuwa ndoa imefungwa, ndipo ghafla akaanza kuumwa na mpaka kufikia kufarikia. Wakazi wa Chunya wanaijua vyema habari hiyo 2014/2015.
 
Hospital anayotibiwa ni NSK hospital bora kabisa naya gharama haswa
Zaidi ya kuwa na vifaa bora vya maabara NSK haina ubora wowote. Haina madaktari wazuri wala wataalam wabobezi wa afya. Mtoe ndugu yako hapo kabla hajafariki.

Hao NSK wenyewe wakiona hali haieleweki watampa rufaa aende Mount Meru aua KCMC. Jiulize kwa nini wampe rufaa na siyo wakomae na mgonjwa wako hadi mwisho. Jiongeze kabla haujalia
 
Jamaa amesema wamekwenda hospitali zaidi ya 5 na kote wanapata jibu lilelile, maana yake ni kuwa, wameambiwa ana tatizo gani, sio kukisia tena.
Sometimes unaweza kuambiwa huna tatizo kwa kuangalia Hali yako wewe mwenyewe na utayari wa kupokea majibu inaitwa placebo hiyo ....
Na ndo maana kama angetuma majibu tungejua jinsi ya kumsaidia
 
Inabidi amkabidhi BWANA YESU shida zake, Yeye huwa hashindwi na jambo lolote.
Sijui kweli?
 
Zaidi ya kuwa na vifaa bora vya maabara NSK haina ubora wowote. Haina madaktari wazuri wala wataalam wabobezi wa afya. Mtoe ndugu yako hapo kabla hajafariki.

Hao NSK wenyewe wakiona hali haieleweki watampa rufaa aende Mount Meru aua KCMC. Jiulize kwa nini wampe rufaa na siyo wakomae na mgonjwa wako hadi mwisho. Jiongeze kabla haujalia
Rudi kasome post vizur
 
Hii haihitaji daktari bingwa kujua kuna tatizo kubwa huenda kuna vitu wanamficha
Ninaimani na wewe DR mambo AMP lkn hao madaktari wote kutoka hospital tano wanamficha👀?hata hivyo kama ulivyoshauri jamaa aweke majibu mezani watu washauri cha kufanya ikiwezekana twende upande wa pili chap
 
Yeah mkuu, Ethically (Wote wanafata Taratibu zote za Chronic illness Huenda kama anayo)
kuna baadhi ya Magonjwa kutoa majibu ya moja kwa moja kwa Relatives huwa ni mtihani ni mpaka uchunguze utayari wa Mpokeaji wa majibu unaweza ukampa Majibu badala ya kupunguza Tatiz ukawa ndo unachochea moto...

Kwa hiyo ni Jukumu la Daktri kuchunguza utayari na kujiridhisha kuwa Majibu hayo anayatoa sehemu salama..
Kwa mfano mtu mwenye HIV au cancer Kutoa majibu yake bila kuchunguza Hali ya mpokeaji huweza kusababisha matatizo makubwa sana...
(Na nahisi labda ndo maana anapewa sana Rufaa...)

Na ukimuuliza huenda kote anakoenda anaulizwa hili swali "kwani huko wamekuambiaje".....Rufaa yoyote huwa na maelezo kuhusu mgonjwa ,ugonjwa na maelezo ya ziada...

Kwahyo lazma uangalie signs za Ukubali wa majibu na baadhi ya Dodoso kuhusu Ugonjwa ukiona Inafaa unaweza kumpa majibu Relatives lakini ni kwa consents/Ruhusa ya mgonjwa...
Endapo mgonjwa atakataa au hataridhika na wewe kupewa majibu bado itakuwa ni mtihani kwako kupewa hata kama utaonyesha utayri wa kuyapokea majibu hayo...
 
Kuna dada alijifungua mtoto miezi mitano iliyopita sasa ameshikwa na ugonjwa wa kupungukiwa damu sana kila akienda hospitali anaingiziwa damu lakini siku hiyo hiyo inaisha tena na madaktari wamempima kila kitu haonekani na tatizo lolote sasa.

Kwanini damu inakauka tu?
atakuwa ana maradhi ya nguvu ya giza nione kwa wakati wako ili niweze kumtibia maradhi yake
 
Nashida ya moyo kwenda mbio sana nimepima Kila kitu Niko sawa shida nini jamani msaada wenu
 
Back
Top Bottom