Msaada, Ugonjwa wa ngozi unaotesa Wanangu

Hapa ndio umesaidia nini?
 
Mwanangu aliwahi kupata tatizo kama hili nilizunguka hospitali zote hapa dar, kuna dr mmoja anaitwa massawe pale morocco akasema akifikisha miaka mitano itaisha na ni kweli sasa ni kijana mkubwa hana shida tena.
 
Chukuwa hii lakini badae usifanye kama unauza kwa watu yaani waambie bure kabisa kama mimi ninavyokwambie.

Tafuta mti wa mwarobaini mizizi yake

Tafuta mti wa mjohoro mizizi yake

Tafuta mbaazi mizizi yake huu unachimba mzizi asubuhi saa kumi na moja hakikisha usemezani na mtu au haupo katika siku zako kama ni kwanamke, vile vile hupaswi kuwa na jasho la kufanya mapenzi.

Tafuta mzugwa majani yake.


Chemsha kisha muogeshe mtoto/watoto asubuhi na jioni changanya na chumvi ya mawe.

usichanganye na maji mengine kabisa.

mwarobaini
Mjohoro
Mbaazi
Mzugwa

mpatie kikombe nusu kimoja kila siku usichanganye na chumvi ya mawe katika kuvywa.

Matumizi ni siku saba za mwanzo kisha unaacha siku saba nyingine haumpi.

Siku saba nyingine unampa siku saba nyingine unaacha

Siku saba nyingine unampa,hapo atakuwa kamaliza dozi.

Mana hiyo hutumika kwa mara tatu katika mfumo huo.

HIVYO NDIO NIJUAVYO TIBA HIYO.

Onyo😡 mimi sio mganga usinifate pm tafadhali 😂
 
Habari ..
Angalia vitu hivi ni lini mara ya mwisho umewapa dawa ya minyoo?,chunguza hiyo shida inatokea hasa baada ya kula au kunywa nini? Kwa maana kwamba wanaweza kuwa na allergy na baadhi ya vyakula pia kapime ujue kama wanamchafuko wa damu..
 
Pole sana, huo unaitwa ukurutu, scabies kitaalamu.. Ni bora uende hosp nyengine wawaangalie vizuri ili wote waanze matibabu ikiwezekana na wewe mwenyewe kama umekupata pia.
Umetumia kigezo Gani kusema ni ukurutu.
 
#Mrejesho#

Habari za Mida wakuu, napenda kutoa mrejesho wa Ugonjwa huu unaosumbua watoto wangu.

Nashukuru Kwa wote mliotoa ushauri juu ya hili tatizo asanteni sn

Shida ni Maziwa fresh ya ng'ombe , nilikuwa nawanunulia mtindi maeneo ya Mbezi, sasa nikaja kununua Maziwa fresh ya ng'ombe katika kabisa moja hapa mtaani. Hapo ndipo tatizo lilipoanza Kwa Kasi Ila baada ya kuacha kuwapa naona vinaanza kupungua na wanaacha kujikuna.

Nimepanga kuendelea kufatilia vitu vingine vinavyoweza kuwapa allergy pia nimembiwa hata mayai ya kuku yanaweza changia.

Ila Dr kaniambia wakifikisha miaka 5 kuna possibly ya ugonjwa huu kuisha

Asanteni
 
Nitafute WASSAP 0779427472 Kila kitu kinaenda kuisha kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…