Msaada: Ukipewa Mkopo wa kusoma Diploma ukahitimu. Je, utapewa na mkopo wa kusoma Degree (Elimu ya Juu)?

Acha kueneza uongo,
Leta uthibitisho kuwa riba ni zaidi ya 15%
Wewe kama ni mtumishi wa umma nchini sidhani kama ungepingana na Mimi. Ila kwakua upon njee ya mchezo basi tuishie hapo
 
Hakuna hisabati za namna hiyo. Deni la mkopo wa elimu halina riba. Hivyo utakachopewa ndiyo utakacho rudisha.
 
Mkuu hiyo tuition fee ya around 5M kwa government University ni ya chuo gani?
Tuition kwa MD naona inachezea kwenye 1.8M kwa mwaka.
Hiyo riba ya bodi si ilishafutwa? Hiyo interest unayoisema inatoka wapi mkuu?

Ukiwa vizuri kiuchumi hakuna haja ya kuomba bodi.
 
Sio wote watafadhiliwa kama ilivyo medicine ambayo wengine wanafadhiliwa na wengine ni mikopo.
 
Kanuni ya loan board ni lazima angalau ulipe asilimia 25 ya mkopo uliosomea ili upate mwingine.
Kama una uwezo jisomeshe dip uombe mkopo degree sababu deni litakuwa kubwa sana ukianza kukopa diploma.
 
Kilichofutwa ni value retention fee yaani Ile riba baada ya kuchelewa kulipia ukisha hitimu.
 
Kilichofutwa ni value retention fee yaani Ile riba baada ya kuchelewa kulipia ukisha hitimu.
Kama ulikopeshwa milioni 9 utarudisha 9 hakuna zaidi ya hapo tusipotoshe umma. Huu si mkopo wa bank ni elimu na upo kwaajili ya kusaidia siyo kutengeneza faida
 
Kama ulikopeshwa milioni 9 utarudisha 9 hakuna zaidi ya hapo tusipotoshe umma. Huu si mkopo wa bank ni elimu na upo kwaajili ya kusaidia siyo kutengeneza faida
Hata processing fee siku hizi haipo?
 
Kanuni ya loan board ni lazima angalau ulipe asilimia 25 ya mkopo uliosomea ili upate mwingine.
Kama una uwezo jisomeshe dip uombe mkopo degree sababu deni litakuwa kubwa sana ukianza kukopa diploma.
Mkuu shukurani sana Huu ushauri wako Ngoja niufanyie kazi. Maana Sina mzigo Mrefu mwaka huu tu ndo nahitimu Dip so ngoja nikomae tu nimalizie mwakani Mungu akijalia nitaomba
 
Ni kweli HESLB kwa sasa inamdai mnufaika kiasi kile tu ulichoandikiwa kwenye loan statement (kiasi halisi ulichokopeshwa/principal loan) bila riba yoyote.
Kuhusu utaratibu wa kulipa deni kwa watumishi/waajiriwa ni kwamba kila mwezi unakatwa 15% ( asilimia 15) ya basic salary hadi deni litakapoisha.
Kwa aliyejiajiri anatakiwa kulipa kiasi kisichopungua 100,000(laki 1) kwa kila mwezi hadi deni litakapoisha.
Kuhusu kupata mkopo wa degree ni hadi umalize deni lote la nyuma (la diploma).
Wanaoruhusiwa kuomba mkopo japo hawajamaliza deni lote ni wale ambao walikuwa wanufaika wa HESLB ila walikatisha masomo yao. Hao wanatakiwa kulipa angalau asilimia 25 (25%) ya deni lote ili waombe mkopo mwingine.
 
Utapewa ndio ila kwa ushaur jitahidi sana kuepuka hii mikopo kama uwezo wa kujisomesha upo hata kwa shida maana baadae ukimaliza na ukapata ajira utafuraia maisha kupita kiasi
 
Mzee, Hii hesabu ni ya mwaka gani? Hakuna kitu cha hivi aiseeee
 
Interest imeondolewa muda sana mbona hakuna cha 6% wala 15% unalipa ulichokopeshwa .
 
Nashangazwa sana ni kwamba watu huwa hamfuatilii taarifa za habari ? Mkopo wa degree kwa sasa hakuna riba yeyote ile yaani utalipia kile ulichokopeshwa na hii imeanza mwaka 2020 rais samia suluhu alipoingia madarakani alifuta 6% ya value retension fee na heslb wakaondoa 15% ya penalty na hata wahitimu wa nyuma walifutiwa madeni ya riba .

Jaribu kuangalia videos zipo nyingi na hata articles za heslb pia zipo zinazoelezea riba kuondolewa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…