Msaada ulevi unanitesa

Msaada ulevi unanitesa

ila usiongeze dawa mwishowe utatokwa jasho kama mtu aliefumaniwa

Habari zenu wakuu

Nimekua na mambo yananisumbua zaidi ya mwaka sasa, na nimeweza kuwa mnafki na kuyaweka moyoni tu bila kuongea kwa watu mambo hayo.

Kutokana na mambo mengimengi nilijikuta siwezi kulala usiku bila kumeza dawa(piriton)

Mwanzoni nilichukulia kawaida lakini sasa naona hali inazidi kuwa mbaya zaidi nilianza na vidonge viwili sasa nimefikia vitano.

Kila siku usiku ni lazima nimeze vidonge hivyo kama nahitaji kulala na vimekua msaada mkubwa kwangu

Lakini sasa vinanitesa, Mapigo ya moyo yanaenda mbio mda wote natoka jasho kama glass iliyotolewa kwenye jokofu, Nahisi kizunguzungu mara kwa mara na giza la gafla hata imefikia kuanguka anguka.

Ndugu wamekua wakiulizana nini tatizo nashindwa kuwaelezea tabia yangu ya kubwia mavidonge kila usiku, na nisingependa watu wafahamu napitia nini katika nafsi yangu.

Nifanyeje niweze kuacha matumizi ya dawa hizi??

Je nikiendelea na ulevi huu nini mwisho wangu??

MIMI NINAKUSHAURI ANZA KUFANYA MAZOEZI SANA YAANI ASUBUHI NENDA JOGGING KIMBIA NA MALIZIA KWA MAZOEZI YA VIUNGO NA MWILI UCHOKE SANA. PIA JIONI MAZOEZI TENA KWA JAPO SAA 1 HATA DK.30, HAPO UTACHOKA NA UTALALA USINGIZI FOFOFO BILA DAWA.
MIMI NILIKUWA MLEVI WA POMBE, USINGIZI HAUKUWA SHIDA HATA NISIPOKUNYWA ILA NILIWEKA RATIBA YA KUJICHOSHA, AISEE NIPO SAFI MAANA ULEVI HUMFANYA MTU KUBADILIKA HADI SURA KUWA MBAYA NA MWILI KUCHOKA CHOKA KUKOSA HAMU YA KULA. KWAHIYO KWASASA KWA ZOEZI INANIFANYA NILALE MAPEMA NA MWILI UMEKUWA MKAKAMAVU NA NINAUMBO LA KIUME YAANI MASCULAR. ILA KICHWANI KIAKILI NILIDHAMIRIA KUACHA POMBE.
NAWEWE HAYO UNAYOWAZA YAKATAE, KUWA MTU WA KUPUUZA SOMETIMES.

Unahitaji psychotherapy, Jaribu kupata watu unaowaamini wakushauri vzuri itakusaidia sana.

kula vizuri, fanya mazoezi, pata muda wa kupumzika ikibidi hata mchana.

Hizo dawa unaeza acha taratibu tu kwa kupunguza vidonge cku baada ya cku, maana ushautengenezea mwili dependency.

Habari zenu wakuu

Nimekua na mambo yananisumbua zaidi ya mwaka sasa, na nimeweza kuwa mnafki na kuyaweka moyoni tu bila kuongea kwa watu mambo hayo.

Kutokana na mambo mengimengi nilijikuta siwezi kulala usiku bila kumeza dawa(piriton)

Mwanzoni nilichukulia kawaida lakini sasa naona hali inazidi kuwa mbaya zaidi nilianza na vidonge viwili sasa nimefikia vitano.

Kila siku usiku ni lazima nimeze vidonge hivyo kama nahitaji kulala na vimekua msaada mkubwa kwangu

Lakini sasa vinanitesa, Mapigo ya moyo yanaenda mbio mda wote natoka jasho kama glass iliyotolewa kwenye jokofu, Nahisi kizunguzungu mara kwa mara na giza la gafla hata imefikia kuanguka anguka.

Ndugu wamekua wakiulizana nini tatizo nashindwa kuwaelezea tabia yangu ya kubwia mavidonge kila usiku, na nisingependa watu wafahamu napitia nini katika nafsi yangu.

Nifanyeje niweze kuacha matumizi ya dawa hizi??

Je nikiendelea na ulevi huu nini mwisho wangu??
Pole sana Dada !!.

Hiyi ni Drug Abuse, ndio madawa ya kulevya aisee.. yaani piriton tano ni nyingi... tafadhali sana, waone madaktari..

DAWA NI YESU....1.OKOKA 2. SOMA NENO 3. MAOMBI 4. ACHA DHAMBI NA MICHANGANYO.

rubii ni lini mara ya mwisho umepima blood pressure-BP yako?

Kama hujapima fanya hivyo haraka sana na umuone daktari. Naona ni kama dalili za severe high BP.

Kama unakaa mwenyewe rudi nyumbani kwenu kwa Muda kidogo... Hata Kama inawezekana uhame hapo unapokaa.... Pili usilale mwenyewe tafuta mtu hata Kama ni rafiki yako wa kawaida akupe company kwa usiku Wakati wa kulala....haya mambo yanatesa sana.

My dear, hii shida ni ya kiroho zaidi.
tatizo bila piritoni siwezi kulala kabisa akili yangu inakuwa busy kuwaza

pole my dear!kwanza kubali kuliweka hadharan au hata kwa dk umweleze unaweza kusaidika usipende kukaa na majanga moyon namna hyo funguka utahis umepona!au mtafte mama mtu mzima mfungukie!umenikumbusha mbali

Back
Top Bottom