Msaada , ushauri wa eneo,mkoa wa kufanikisha huu mradi great thinkers!

Msaada , ushauri wa eneo,mkoa wa kufanikisha huu mradi great thinkers!

goodmother

Senior Member
Joined
Jul 21, 2012
Posts
108
Reaction score
78
Heshima kwenu wakuu! Nina wazo la kufungua mgahawa sio local sana wala wa kisasa sana, mradi huu nilikuwa na fikiri kuuanzisha morozgoro, au Mwanza na pia nataka nijihusishe na kilimo haswa cha mahema ( tomato, pepper and watermelon kwa njia ya greenhouse) na mazao mengine ya mboga mboga. Pamoja na ufugaji wa kuku kienyeji ili niweze kupata mbolea kwaajili ya kilimo hicho. Wakuu ni mkoa gani ambao mawazo yangu hayo yatafanikiwa utekelezaji wake yote kwa pamoja Pia upatikanaji wa eneo la mgahawa na shamba ekari tatu (3) ? Natanguliza shukurani kwenu.
 
Ili uweze kufanikisha vitu vyote, morogoro ni pazuri kuliko mwanza: hii nikwasababu ya initial cost yake ni ndogo kulinganisha na mikoa mingine, kama vile mashamba utapata kwa beindogo, malighafi kwa mgahawa ni nafuu sana, na uhitaji wa mghawa ni mkubwa maana wengi hapa morogoro ni wahamiaji wa muda kama vile wanavyuo, wafanyabiashara ambao wengi wao ni single hivyo hula kwenye migahawa.
kwaupande wa hotculture, udongo una rutuba sasa ukiongezea maarifa hapo hushikiki tena.Aidha kunafaida ktk mkoa huu maana nikituo cha vyuo vya kilimo ambapo unaweza ukashea mawazo.

"Economic for life"
 
Nashukuru kwa ushauri mr. Atufigwege ambao umezingatia matakwa yangu. Kama ni mkazi wa moro naomba nijulishe maeneo mahususi ambayo nitaweza kuwekeza haswa mgahawa kwanza. Wakati naendelea na mchakato wa mashamba. Mimi si mwenyeji huko.
 
Naam! mimi ni Mwanafunzi wa chuokikuu cha Jordan ambacho kipo hapa morogoro mtaa wa nanenane,original mimi natoka Rungwe~Mbeya, lakini ninapenda ujasiriamali ambao unanifanya kuwa mtafiti wa maswala hayo. Hata hivyo,niliokuambia, kwa kiasi nimeyafanyia utafiti kwa kuingia kwenye masoko pamoja na kuifahamu jiografia ya morogoro kwa kuwahusisha wakulima na wakaazi husika. nichoweza kukushauri: kama una ndugu au jamaa wa karibu njoo ukae wiki mbili kabla ya yote ukifanya doria ya migahawa na idadi ya walaji kwa manispaa ya morogoro. Hivyo uamuzi wa mwisho utauchukua sehemu ambapo idadi ya walaji nikubwa, idadi ya migahawa ni ndogo au hata kama ni kubwa wewe jiandae kwa kuleta mgahawa wenye usafi wa hali ya juu(hiki nimekiona huku, jiandae hivyo utavuta watu wengi).Aidha kabla ya kuajiri watendaji hakikisha umewafundisha namna ya kukarimu wateja na hii itakutofautisha.iIa kwa hapa maeneo mengi yanalipa maana walaji niwengi lakini tafuta penye faida zaidi.
"Economics for life"
0769882278
 
Back
Top Bottom