Mulangila Mukuru
JF-Expert Member
- Feb 24, 2010
- 1,945
- 728
Kufunga vipi, fafanua mkuu kwa faida ya wengi.
Usidandie gari kwa mbele! Subiri umri usonge kidogo
Kufunga vipi, fafanua mkuu kwa faida ya wengi.
Muangila mpeleke kwa dr.wa watoto kuchelewa au kuwahi kufunga huwa haitakiwi lakini mi daktari alishawahi kunambia utosi huwa unafunga kabisa akifika mwaka. kwa utosi wa nyuma unafunga kuanzia mwezi na nusu wa mbele kuanzia mitatu na kuendelea lakini unakua haujafunga completely mpaka mwaka mmoja
Nimekusoma vyema mkuu, wajuvi watakuja kudadavua sote tuelimike.Ok mkuu sijui kama una watoto tayari au bado lakini ni kuwa kawaida mtoto anapozaliwa huwa utosini (katikati ya kichwa kwa juu) huwa mfupa wa kichwa haijaungana na ukingalia kwa makini utaona ubongo unachazacheza kama vile mapigo ya moyo na hali hii huisha muda mfupi baada ya eneo hilo mifupa kuungana na kuziba.
Sasa kinachotokea kwa kijana wangu mapaka sasa mwezi wa tano toka azaliwe sioni dalili za eneo hilo kuziba,nadhani umenielewa kaka nasubiria ushauri wako.
Muangila hapo unakuwa unampaka mafuta ya nazi pale utosini kwa wimgi hiyo ni tiba tosha
hakikisha mafuta hayakauki utosi utafunga tu
The secretary ur welcome,Asante Heaven on earth huwa nampaka mtoto mafuta ya nazi na ubuyu utosini bila kujua