Msaada; Utosi wa mtoto kuchelewa kufunga

Msaada; Utosi wa mtoto kuchelewa kufunga

Mulangila Mukuru

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2010
Posts
1,945
Reaction score
728
Wakuu heshima kwenu
Nina mtoto wa miezi mitano lakini mpaka sasa utosi wake bado haujafunga na umeachia eneo kubwa,ingawa mtoto mwenyewe ana afya nzuri lakini tatizo hili linanipa wasiwasi
Naomba kwa mwenye kujua naweza kumsaidia vipi mwanangu ili utosi ufunge mapema anisaidie
Shukrani.
 
Kufunga vipi, fafanua mkuu kwa faida ya wengi.

Ok mkuu sijui kama una watoto tayari au bado lakini ni kuwa kawaida mtoto anapozaliwa huwa utosini (katikati ya kichwa kwa juu) huwa mfupa wa kichwa haijaungana na ukingalia kwa makini utaona ubongo unachazacheza kama vile mapigo ya moyo na hali hii huisha muda mfupi baada ya eneo hilo mifupa kuungana na kuziba.
Sasa kinachotokea kwa kijana wangu mapaka sasa mwezi wa tano toka azaliwe sioni dalili za eneo hilo kuziba,nadhani umenielewa kaka nasubiria ushauri wako.
 
Muangila mpeleke kwa dr.wa watoto kuchelewa au kuwahi kufunga huwa haitakiwi lakini mi daktari alishawahi kunambia utosi huwa unafunga kabisa akifika mwaka. kwa utosi wa nyuma unafunga kuanzia mwezi na nusu wa mbele kuanzia mitatu na kuendelea lakini unakua haujafunga completely mpaka mwaka mmoja
 
Last edited by a moderator:

Nakushukuru sana mkuu nitafanya hivyo.
 
Last edited by a moderator:
Ok mkuu sijui kama una watoto tayari au bado lakini ni kuwa kawaida mtoto anapozaliwa huwa utosini (katikati ya kichwa kwa juu) huwa mfupa wa kichwa haijaungana na ukingalia kwa makini utaona ubongo unachazacheza kama vile mapigo ya moyo na hali hii huisha muda mfupi baada ya eneo hilo mifupa kuungana na kuziba.
Sasa kinachotokea kwa kijana wangu mapaka sasa mwezi wa tano toka azaliwe sioni dalili za eneo hilo kuziba,nadhani umenielewa kaka nasubiria ushauri wako.
Nimekusoma vyema mkuu, wajuvi watakuja kudadavua sote tuelimike.
 
Muangila hapo unakuwa unampaka mafuta ya nazi pale utosini kwa wimgi hiyo ni tiba tosha

hakikisha mafuta hayakauki utosi utafunga tu
 
Last edited by a moderator:
The secretary usiwe na wasi wasi sio ugonjwa wa kwangu ana mwaka na miezi mitatu sasa haujafunga bado, ingawa alivyokua na miezi mitano hata mimi nilishangaa sana maana utosi ulikua unadunda mpaka naogopa, wakubwa waliniambia kwamba niliruka makaburi wakati mjamzito (huwa siamini local believes na pia huwa sibishi huwezi jua) Ila siku zinavyoendelea unaanza kupungua ila bado kufunga kabisa so usiwe na wasi wasi utafunga tu
 
Last edited by a moderator:
Za leo, mi mtoto wangu ana wiki tatu ila cha kushanhaza ni utosi wake haudundi. Sasa sijui tatizo ni nini. Naombeni msaada kwa yeyote anaefahamu hili swala
 
Back
Top Bottom