Msaada wa "calculations" za mshahara, overtime, public holidays etc.

Msaada wa "calculations" za mshahara, overtime, public holidays etc.

Bin Kawambwa

JF-Expert Member
Joined
Oct 9, 2012
Posts
440
Reaction score
297
  • Habari wanajukwaa.

Naomba mnisaidie namna ya ku-calculate overtime kwa siku za kawaida na public holidays. Kwa ufahamu wangu, overtime ya kila saa ni mara moja na nusu ya mshahara wa kila saa (wa basic), na public holidays ni mara mbili ya malipo ya basic salary.

Swali 1,
Ni vipi huo mshahara (basic salary) wa kila siku au kila saa unapatikana?

Swali 2,
Ninapofanya kazi public holidays na kulipwa overtime yake, Je, inabidi kulipwa mara 3, i.e. mara moja ni ile basic na mara mbili ni zile za overtime? au Unalipwa mara 2, mara moja basic na nyingine overtime yako? Hapa namaanisha ni nini maana ya overtime kwa public holidays kulipwa mara?

Swali 3,
Kodi huwa ni asilimia ngapi? Na Ipi ndo hukatwa kodi, Basic Salary, Gross Income or another case?

Swali 4,
Je usipohudhuria kazini kwa siku moja au mbili, ni hatua gani au adhabu inayopaswa kwa mwajiriwa? Ni sahihi kukata mshahara wangu wa basic kama fidia kwa kutofika kazini siku hiyo?

Nitafurahi pia kupata vipengele vya kisheria kwa kila swali nililouliza, (kwa mwenye kumbukumbu sahihi ya vipengele hivyo).

Natanguliza shukrani zangu kwenu. Naomba kuwasilisha.
Ahsante.
 
Tuliojiajiri basi tunajua kitu juu hili yaani sisi nikufanya kazi kama punda. Mapumziko na malipo tunajipa wenyewe. Just joking- sijui lolote.
 
  • Habari wanajukwaa.

Naomba mnisaidie namna ya ku-calculate overtime kwa siku za kawaida na public holidays. Kwa ufahamu wangu, overtime ya kila saa ni mara moja na nusu ya mshahara wa kila saa (wa basic), na public holidays ni mara mbili ya malipo ya basic salary.

Swali 1,
Ni vipi huo mshahara (basic salary) wa kila siku au kila saa unapatikana?

Inategemea na mkataba wako, kawaida unapopewa mkataba mara nyingi mshahara unaweza kuandikwa kwa mwezi au kwa mwaka na mara nyingi hujumuisha gharama zote kwa kampuni hapa namaanisha gharama ambazo zinajulikana yaani mshahara wako, mchango wa mwajiri kwa pension fund pamoja na house allowance (hii ni kwa baadhi ya waajiri), sasa kama mshahara wako ni kwa mwaka say X wanachofanya ni kukadiria wastani wa siku 260 unazotakiwa kufanya kazi halafu saa nane kwa kila siku, hivyo mshahara wako kwa saa utakuwa X/(260*8) na kama ni kwa mwezi say Y mara nyingi huwa wanachukua wastani wa siku 21au 22 kwa mwezi au saa 168 au 176, kwa hiyo mshahara wako kwa saa utakuwa Y/168 au Y/176

Swali 2,
Ninapofanya kazi public holidays na kulipwa overtime yake, Je, inabidi kulipwa mara 3, i.e. mara moja ni ile basic na mara mbili ni zile za overtime? au Unalipwa mara 2, mara moja basic na nyingine overtime yako? Hapa namaanisha ni nini maana ya overtime kwa public holidays kulipwa mara?

Kwa kawaida overtime inalipwa baada ya kukokotoa kulingana na mshahara wako pamoja na saa za ziada ulizofanya kazi. Mfano umefanya kazi saa 30 kwa mwezi ambazo unatakiwa kulipwa mara mbili na saa 14 ambazo unatakiwa kulipwa mara moja na nusu, malipo yako itakuwa kama ifuatavyo.

  • Basic Salary -----------------Y
  • Overtime 1.5-----------------Y/168*1.5*14=Y1
  • Overtime 2.0 ----------------Y/168*2*30=Y2
  • Gross income --------------Y+Y1+Y2
NB: Idadi ya saa za ziada unazolipwa mara 1.5 ni zile siku za kawaida unapofanya kazi kuanzia 17h30 hadi saa 20h00 pamoja na jmosi, kama muda wako wa kutoka kazini ni saa 17h30, kwa kifupi ni baada ya muda wako wa kazi hadi saa mbili usiku baada ya hapo untakiwa ulipwe mara mbili pamoja na siku za sikukuu au jumapili.

Swali 3,
Kodi huwa ni asilimia ngapi? Na Ipi ndo hukatwa kodi, Basic Salary, Gross Income or another case?
Kodi hukatwa kutoka kwenye gross income, ingawa baadhi ya sehemu huficha overtime na hivyo kupelekea kodi kukatwa kwenye basic salary, lakini sheria ya kodi inataka mapato yote yanayotokana na kazi lazima yakatwe kodi hii ni pamoja na bonus.
Hakuna asilimia ya kodi ya moja kwa moja, inategemea na basic yako. Nenda website ya TRA utaona.

Swali 4,
Je usipohudhuria kazini kwa siku moja au mbili, ni hatua gani au adhabu inayopaswa kwa mwajiriwa? Ni sahihi kukata mshahara wangu wa basic kama fidia kwa kutofika kazini siku hiyo?

Mkataba wako wa kazi unahusika hapa.

Nitafurahi pia kupata vipengele vya kisheria kwa kila swali nililouliza, (kwa mwenye kumbukumbu sahihi ya vipengele hivyo).

Natanguliza shukrani zangu kwenu. Naomba kuwasilisha.
Ahsante.
Angalia nimejibu kwa kila swali.
 
Mkuu nashukuru sana, maelezo ni mazuri mno, ngoja nipige hizo calculations ulizonipa, then nitarudi kukuuliza tena swali la lile 2, maana kidogo nimeachwa njia panda. nashukuru sana mkuu.
 
Back
Top Bottom