Bin Kawambwa
JF-Expert Member
- Oct 9, 2012
- 440
- 297
- Habari wanajukwaa.
Naomba mnisaidie namna ya ku-calculate overtime kwa siku za kawaida na public holidays. Kwa ufahamu wangu, overtime ya kila saa ni mara moja na nusu ya mshahara wa kila saa (wa basic), na public holidays ni mara mbili ya malipo ya basic salary.
Swali 1,
Ni vipi huo mshahara (basic salary) wa kila siku au kila saa unapatikana?
Swali 2,
Ninapofanya kazi public holidays na kulipwa overtime yake, Je, inabidi kulipwa mara 3, i.e. mara moja ni ile basic na mara mbili ni zile za overtime? au Unalipwa mara 2, mara moja basic na nyingine overtime yako? Hapa namaanisha ni nini maana ya overtime kwa public holidays kulipwa mara?
Swali 3,
Kodi huwa ni asilimia ngapi? Na Ipi ndo hukatwa kodi, Basic Salary, Gross Income or another case?
Swali 4,
Je usipohudhuria kazini kwa siku moja au mbili, ni hatua gani au adhabu inayopaswa kwa mwajiriwa? Ni sahihi kukata mshahara wangu wa basic kama fidia kwa kutofika kazini siku hiyo?
Nitafurahi pia kupata vipengele vya kisheria kwa kila swali nililouliza, (kwa mwenye kumbukumbu sahihi ya vipengele hivyo).
Natanguliza shukrani zangu kwenu. Naomba kuwasilisha.
Ahsante.