Msaada wa connection CRDB Bank kwa anayeweza nisaidia

Hilo linashangaza... Sasa walikuwa wanakuja site kufanya nini? Valuation of asset inafanyika na valuer wao, ambaye anawapa report... Hayo yote ya distance nk.... yanakuwa covered kwenye valuation report ... Hapo sasa naona unadeal na unprofessional... Kwa mfano, NMB anaweza kukupa mkopo hata dhamana ipo mkoa mwingine , alimradi inakidhi vigezo vyao...

Nenda NMB, tengeneza valuation.
 
sidaiwi mkuu

Hawajaweka hiyo point mkuu,ingekua ivyo wangesema basi tunakupunguzia kiwango cha mkopo.

ila point yao ni 1 tu kwamba "UMBALI"

Umbalii..hiyo sababu haimake sense na Haina logic hapo nyumba Kwa upande wao hawajaona Iko valuable enough Kwa huo mkopo....wakatafuta sababu
 
Ukitoa percent mkopo utaulipaje? Hapo ndo mwanzo wa mkopo kutolipika maana pesa imeelekezwa kwingine
 
Unachokiandika hapa mkuu wengi sana tunao ongelea hili swala wananiuliza sasa hawa walikua wanakuja site kufanya nini? kuna namna natakiwa nianze na NMB tena siku deal nao sababu huwa siweki pesa kwao yani mizunguko yangu ya pesa natumia CRDB hvyo niliona niombe CRDB ila sasa itabidi nianze process mpya za Mkopo NMB,JAMBO litalochukua tena muda kwakweli ni habari za mwakani hizo.
 
Umbalii..hiyo sababu haimake sense na Haina logic hapo nyumba Kwa upande wao hawajaona Iko valuable enough Kwa huo mkopo....wakatafuta sababu
Ni kweli na bora hata wakwambie ukweli mtu uelewe unajua wangesema nyumba haiko valuable ungejua kweli hapa basi niwambie wanaweza kunipa kiasi gani.

maana swala la umbali watu wanakopa mikopo ya kilimo mashamba yapo maporini huko sembuse nyumba iliyopo mjini?
 
Hao walikua hawana Nia ya kukupa pesa kuanzia mwanzo, mi ni mzoefu wa mikopo crdb... Wanakupaje pesa bila ya kua na valuation report???
 
Nenda NMB
 
Ila kama biashara inaenda vizur usikope reinvest hiyo faida...mikopo ni pesa za nuksi na mabalaa ukingiza tu kwenye biashara zinaharibu
 
Yani hilo jambo limenishangaza sana,nikasema kwakua sijui acha ninyamaze ila matokeo ndio hayo
Valuation report lazima iwepo maana sio wao wanaidhinisha mikopo direct, wao watapitisha lakini lazima makao makuu wapelekewe wajadiliane ili kuidhinisha mkopo, sasa bila ya valuation report watajuaje dhamani halisi ya dhamana yako??

Kuna bank kama Azania wameanza ukuda, wanatoa si zaidi ya 50% ya thamani inayoonekana kwenye valuation report
 
Wakiangalia mzunguko, si lazima uwe kwenye benki unayoombea mkopo... Jipange vizuri... bank statement unazo, taarifa ya biashara unayo, leseni za biashara unayo, usajiri wa biashara ( Brela ) fanya mchanganuo wa biashara yako, ukiwa na document zote hizo , with confidence nenda uongee na meneja wa tawi la karibu na dhamana yako ilipo.... Usisikie wanakupa majibu gani... ....Mabenki wanatafuta sana watu wa kukopa.. Sijajua unachukua mkopo kwa ajili ya nini na unafanya biashara gani..

Kumbuka benki hawatoi mkopo kuanzisha biashara , wanatoa mikopo ya biashara kukuza mtaji, au uzalishaji unaoendelea...

Kama hayo yote , uko tayari nenda benki mbalimbali, lakini anza na NMB... halafu angalia benki walio karibu na dhamana yako ilipo.... Inamaanisha wilaya au kata ya karibu ... Ziangalie benki zenye muelekeo huo.
 
Hao wanataka RUSHWA jiongeze
 
Hao wanataka RUSHWA jiongeze
Nimeliona hili ila wengine hatujawahi kujiongeza unashindwa umuanzeje sasa... maana mtaka rushwa humjui na asietaka nae huwezi mjua hvyo n lazima akili ya ziada iwepo maana mwingine anaweza akawa hataki ukimuonyesha mazingira ya rushwa ndio unajikaanga kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…