Msaada wa connection CRDB Bank kwa anayeweza nisaidia

maana CRDB hawa hawa wana Branch huko dhamana ilipo sasa najiuliza hawa wakisema n mbali je hao wenzao walioko huko je? nmewaza kama wewe mkuu nitafute bank ambapo dhamana ipo ila nawaza Biashara itakua mbali na wao Je hayatokua yale yale?? tupotezeane muda?

Unajua CRDB niliwategemea kwa kiasi kikubwa sana maana mimi ni WAKALA wao PIA, yani hii bank wamenikera mpaka sijui nisemeje, na laiti wangeniambia haya yote nisinge hangaika mimi.
 
valuation ikija 17m maana yake mkopo wako hupewi zaidi ya 50% asee huu ni ukuda mno.

Sasa mtu anamiliki nyumba ina range 15m to 17m ana biashara ya capital yakutosha unakuja umwambie umpe mil 7 si matusi haya?

wakati mil 7 ni hela unayoweza kupewa na ACCESS BANK hata bila dhamana yani biashara yako tu inakudhamini huna nyumba wala kiwanja 7m access wanakupa.. ila BANK hizi mpka nyumba aseee
 

Hadi leo unahangaikaje na benki moja kama unapewa hela bure?

Mambo mengine unajitakia mwenyewe, kuna benki ukienda leo siku 2 wameshakupa hela kutegemea na kiwango.

Wewe ni mfanyabiashara gani, napata mashaka hata kama unavyonunua mzigo usikute umeng’ang’ana na msambazaji mmoja bila kutazama masoko mengine.

Wake up comrade!!
 
Mfano wa hizo bank za chap chap n zipi mkuu,nipe mwanga boss wangu
 
kuna mtu alini tonya CRDB wako faster mkuu na alienipa hyo taarifa ni staff wa crdb ndiomana ila sio kwamba nawaganda sana CRDB.
 
Mfano wa hizo bank za chap chap n zipi mkuu,nipe mwanga boss wangu

Hiyo ni home work ndogo sana, sidhani kama kuna ulazima wa kuzitaja hapa nazo zaweza kuwa na changamoto zake.

Nilitaka ufanye kazi yako kwa usahihi ilifanye maamuzi. Kukopa kuna mambo mengi sana sio tu hilo la uharaka.

Fanya tathminikwa kutembelea sehemu ulipo na benki zilizopo, pata taarifa kwa wenzako hao staff baadae sana.
 
Ndo hivo mkuu, valuation yenyewe ni bei ghali nyumba ya kawaida labda wakufanyie kwa laki 5, na bado mkopo unaweza usipate

Bank hawataki hasara kabisa, ukishindwa Wanataka wakipiga mnada iwe rahisi wao kuuza ndo maana nyumba ya 15M watakupa kama 8M tu....

Na bado hapo utakatwa pesa ya bima ya mkopo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…