Msaada wa engine ya Nadia D-4

Mkuu unamaanisha ninunue sehemu kama autorec...befoward nk
 
hakuna kitu kinachonikera kwa mafundi na madereva wa kibongo kama kutojua majina ya vifaa wanavyo viongelea....

Fundi kakwambia ubadilishe pampu, a wewe ukabadilisha pampu.... Na wataalam wa hapa wanasema tatizo kweli ni pampu

Fuel pump, water pump, oil pump, power steering pump, injector pump, vacuum pump, air ride pump (Range Rover, Cadillacs n.k.).... pampu, pampu ganiiiiii? ?????? ??????

Jesus!
 
Kuna jamaa yangu aliweka engine ya 3s mpaka leo mwendo mdundo
 
Mpigie huyu bwana 0754 371 392 yupo Kirumba police kwa juu anaitwa kachemu
shukrani mkuu sasa hivi mfuko hausomi ...ngoja nivute pumzi..maana nimetoboka mpaka akili imenikaa sawa
 

Direc injection pump.. ipo kwenye engine za d4 ndio zinazoonekana kuleta usumbufu kwa gari hizi tatizo ni kwamba mafundi wengi wa mtaani hawazijui. Nilishakuwa na tatizo hilo kwenye gari yangu toyota opa d4 nikaenda pale toyota wakatatua. Ila zilinitoka karibu mil 2 so wanaomshauri anunue 3s ambayo mafundi wote wanazijua kwa 1.6 mil naona hoja yao ina mashiko
 

Ok, mafundi wa Toyota waliifanya nini hiyo direct injection pump, waliibadilisha?

Kwa milioni mbili?
 
Acheni kumwingiza mwenzenu chaka.hapo tatizo ni d4 pump.so kama akiweka nyingine nzuri ugonjwa umekwisha.

Hivi kweli unamshauri mtu atoe engine ya d4 aweke ya 3s tuache masihara jamani.

Ni sawa na kusema smartphone hazifai kwa kuwa ikidondoka tuu kidogo touch inakufa hivyo usinunue smartphone nunua nokia torch.

Hahahahahahaha
 
Huyo fundi ni katili sana, kaa nae mbali.

Ameshakuingiza hasara.

Hio gari inatakiwa kufanyiwa diagnosis kupata faults codes ilikujua sababu ya tatizo na sio kukisia kisia tu.

Hao mafundi wa namna hio, wameharibu magari ya watu mno.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…