Msaada wa engine ya Nadia D-4

Msaada wa engine ya Nadia D-4

Mkuu, tulizana akili ndiyo uchukue maamuzi. LEGE ametuita mabashite, lakini mimi nimezungumzia experience.

Baada ya gari ya jamaa yangu kuwa na tatizo kama lako, tulimshauri aweke engine ya 3s.

Alipoenda garage, fundi akamshauri anunue engine nyingine ya D4 kwa sababu ni rahisi. Alinunua na gari ikawa fresh. Baada ya miezi kama saba hivi, issue ikaibuka tena.

Mwisho wa siku jamaa yangu aliweka engine ya 3s. Mpaka leo gari ipo fresh.

Gharama alizotumia kutengeneza, ukijumlisha kununua engine ya D4, ambayo ilifaa kwa muda, ilikuwa ni hasara tupu.

Kama ukijikunja ukanunua engine ya D4 au 3s hakikisha unanunua ya kutoka nje ya nchi. Ni sawa sawa hiyo engine yako uivue halafu ifanyiwe marekebisho kidogo na iuzwe kama used.
Mkuu unamaanisha ninunue sehemu kama autorec...befoward nk
 
ef21a3f8759bb8791ddfdc5a3bbdb9f1.jpg
 
hakuna kitu kinachonikera kwa mafundi na madereva wa kibongo kama kutojua majina ya vifaa wanavyo viongelea....

Fundi kakwambia ubadilishe pampu, a wewe ukabadilisha pampu.... Na wataalam wa hapa wanasema tatizo kweli ni pampu

Fuel pump, water pump, oil pump, power steering pump, injector pump, vacuum pump, air ride pump (Range Rover, Cadillacs n.k.).... pampu, pampu ganiiiiii? ?????? ??????

Jesus!
 
Habari wana jamvi wenzangu...nilikua naomva msaada wa kiufundi katika engine ya gari aina ya Nadia. Inachanganya sana oil na petrol yaani naweka lita 3 za engine oil ila baada ya wiki moja namwaga lita 6 mpaka 7 (maelekezo ya fundi nimwage kila baada ya wiki)...fundi kasema tatizo ni pump..nimebadili pump nikaweka mpya bado tatizo ni lile lile. Inawaka kwa siku moja siku ya pili haiwaki..inatoa moshi mweusi ajili ya kuchanganya oil na mafuta.sasa fundi kaniambia nibadili kabisa engine niweke 3-S , kiukweli simuamini tena fundi maana nimeumia vya kutosha na tatizo haliishi..msaada tafadhali je ni kweli kubadili engine ndio suluhisho au..Nawasilisha
Kuna jamaa yangu aliweka engine ya 3s mpaka leo mwendo mdundo
 
Mpigie huyu bwana 0754 371 392 yupo Kirumba police kwa juu anaitwa kachemu
shukrani mkuu sasa hivi mfuko hausomi ...ngoja nivute pumzi..maana nimetoboka mpaka akili imenikaa sawa
 
hakuna kitu kinachonikera kwa mafundi na madereva wa kibongo kama kutojua majina ya vifaa wanavyo viongelea....

Fundi kakwambia ubadilishe pampu, a wewe ukabadilisha pampu.... Na wataalam wa hapa wanasema tatizo kweli ni pampu

Fuel pump, water pump, oil pump, power steering pump, injector pump, vacuum pump, air ride pump (Range Rover, Cadillacs n.k.).... pampu, pampu ganiiiiii? ?????? ??????

Jesus!

Direc injection pump.. ipo kwenye engine za d4 ndio zinazoonekana kuleta usumbufu kwa gari hizi tatizo ni kwamba mafundi wengi wa mtaani hawazijui. Nilishakuwa na tatizo hilo kwenye gari yangu toyota opa d4 nikaenda pale toyota wakatatua. Ila zilinitoka karibu mil 2 so wanaomshauri anunue 3s ambayo mafundi wote wanazijua kwa 1.6 mil naona hoja yao ina mashiko
 
Ok, mafundi wa Toyota waliifanya nini hiyo direct injection pump, waliibadilisha?

Kwa milioni mbili?
 
Direc injection pump.. ipo kwenye engine za d4 ndio zinazoonekana kuleta usumbufu kwa gari hizi tatizo ni kwamba mafundi wengi wa mtaani hawazijui. Nilishakuwa na tatizo hilo kwenye gari yangu toyota opa d4 nikaenda pale toyota wakatatua. Ila zilinitoka karibu mil 2 so wanaomshauri anunue 3s ambayo mafundi wote wanazijua kwa 1.6 mil naona hoja yao ina mashiko
Acheni kumwingiza mwenzenu chaka.hapo tatizo ni d4 pump.so kama akiweka nyingine nzuri ugonjwa umekwisha.

Hivi kweli unamshauri mtu atoe engine ya d4 aweke ya 3s tuache masihara jamani.

Ni sawa na kusema smartphone hazifai kwa kuwa ikidondoka tuu kidogo touch inakufa hivyo usinunue smartphone nunua nokia torch.

Hahahahahahaha
 
Habari wana jamvi wenzangu...nilikua naomva msaada wa kiufundi katika engine ya gari aina ya Nadia. Inachanganya sana oil na petrol yaani naweka lita 3 za engine oil ila baada ya wiki moja namwaga lita 6 mpaka 7 (maelekezo ya fundi nimwage kila baada ya wiki)...fundi kasema tatizo ni pump..nimebadili pump nikaweka mpya bado tatizo ni lile lile. Inawaka kwa siku moja siku ya pili haiwaki..inatoa moshi mweusi ajili ya kuchanganya oil na mafuta.sasa fundi kaniambia nibadili kabisa engine niweke 3-S , kiukweli simuamini tena fundi maana nimeumia vya kutosha na tatizo haliishi..msaada tafadhali je ni kweli kubadili engine ndio suluhisho au..Nawasilisha
Huyo fundi ni katili sana, kaa nae mbali.

Ameshakuingiza hasara.

Hio gari inatakiwa kufanyiwa diagnosis kupata faults codes ilikujua sababu ya tatizo na sio kukisia kisia tu.

Hao mafundi wa namna hio, wameharibu magari ya watu mno.
 
Back
Top Bottom