Msaada wa final year project title kwa bachelor degrees

Yote Tisa kumi umeniongezea ufikiri nashukuru mkuu nadhan ngoja nijikite katika hii game na bila Shaka kwakuwa Ni ya kujifunzia inaeza hata ikawa 2D
 
Namna ya kuwasilisha suluhisho pia labda ni changamoto. Maana hata mimi project hiyo niliyofanya kuna ugumu ulikuwepo mwanzo lakini baada ya kuiwasilisha na kuonyesha uhalisia wa tatizo lenyewe na ukosefu wa suluhisho na pia namna tatizo linavyoongezeka mwaka kwa mwaka, kila mmoja alikuwa sold. Ni tatizo halisi na suluhisho ni halisia sio tu kwa ajili ya kupata degree.

Nashauri kuangalia katika upande wa elimu, na haswa watoto. But hey, that's me.

I'm glad if some of these gave you light.
 
Sasa Kama mtaalam anashindwaje kujua kuwa management systems kwa nchi yetu Ni Bora kuliko gadgets na nyinginezo,...anashindwaje kujua kuwa anavyovitaka yeye vipo ila vinapigwa chini, hamuoni kipanya
Management Information Systems ambazo zinafanya CRUD zimeshafanyika mara nyingi sana toka late 2000s, hakuna kipya utakachokuwa unafanya ndio maana mtaalamu happ amekuambia hivyo.

Kama unafanya dissertation kwa ajili ya kupata Degree lazima utapitia wakati mgumu sana.

Njia sahihi ya kutengeneza title yako ni kuangalia hali halisi ya mazingira yako, kusoma tafiti zilizofanywa kwenye tatizo uliloliona kwenye mazingira yako na kulitetea kupitia maandiko ya tafiti nyingine.

Lazima uangalie kama eneo unalotaka kufanyia utafiti limekuwa na tafiti za kutosha hivi karibuni na umuhimu wa hizo tafiti (recency / relevance).

Huyo lecturer anachotaka mfanye ni sahihi kutokana na maelezo yako kwamba tayari kuna mfumo unaotumika locally, bila shaka hata hospitali nyingine zina mifumo yake inayotumika, na si rahisi kuiondoa hiyo mifumo ili uwekwe mfumo mmoja. Kinachokosekana sasa ni njia ya kufanya hiyo mifumo iweze kubadilishana taarifa za mgonjwa kwa usalama. Kuna taratibu za kuhifadhi na kutuma taarifa za mgonjwa unaweza ukasoma HIPPA kwa kuanzia. Keywords za title yako bila shaka zitakuwa kwenye cloud computing, health data sharing, APIs etc.


Kama ungefanya huo utafiti na kuja na njia ya kufanya hiyo mifumo iongee na kubadilishana taarifa ( data synchronization) ingekuwa na mchango mkubwa sana kuliko kutengeneza tu mfumo mwingine wa kuhifadhi na kuchakata taarifa za mgonjwa ambayo imekuwa ikitengenezwa kwa kipindi kirefu.
 

Kwa kias kikubwa umensaidia na ntatoa mrejesho
 
Umepita mule mule ...kuintergrate Ni kitu Cha kawaida ila Ni ghali kwa mtu kusucrifice pesa na muda kisa degree , inawezeka kuintergrate na NHIF, au nyingine yyte Ile ,

Shida Ni kuwa title ilisha pita na tukawa tunawaza system requirement ,design na implementation , ila wakatuchomolea ....nnakuelewa Sana mkuu tatzo muda uliopo na gharama zake ...now najikita katka gaming Kama nilivosaidiwa na chiz hapo juu
 
Hakuna gharama ya ziada katika kuonyesha jinsi ambavyo hiyo mifumo inaweza kubadilishana taarifa, ingewezekana hata kutengeneza prototype ndogo tu kuonyesha jinsi ambavyo taarifa zingekuwa zinatumwa kati ya mifumo miwili au zaidi iliyopo katika network tofauti.

Kama una muda ungesoma kidogo hii kazi niliyo-attach hapa.
 

Attachments

Na hapo ukifanya mchezo unarudi mwakani.


Mfanye supervisor Kama rafiki.

Lasivyo jiandae kurudi mwakani :-😀
 
File corrupted ,inaeza ituma tena
 
Hiki chuo x kwa hizi descriptions kitakuwa tu Mtakatifu Yusufu...
 
Fanya system ambayo auto traffic control kulingana na foleni za barabara kadhaa. Kusanya data kutoka multiple road then fanya traffic control toka kwenye server

Nyingine ni system ya watu kuita mwendokasi na automatically inafanya aggregation na kumpa controller wapi watu wengi wanahitaji gari.

Simple enough
 
Zote mbili zilifanyika mwaka Jana
 
Zote mbili zilifanyika mwaka Jana
Project mpya kabisa haipo duniani. Chukua hizo zilizofanyika, angalia mapungufu then perfect ndio iwe project yako. Unless yout instructors are total morons which I doubt, they can't refuse it.

Project inapoma ufahamu na uwezo wa kutumia ufahamu huo. Ukijazia significant part ambayo ita demonstrate matumizi ya ufahamu utapita tu...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…