Msaada wa haraka kuhusu tatizo la nyufa ukuta wa nyumba

UMUNYU

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2017
Posts
726
Reaction score
564
Wanajf ninaomba ushauri wa haraka wa nini kifanyike kwani kuta za kakibanda kangu kaliopo Katavi mahali ambapo matetemeko makubwa ya ardhi mithili ya mabomu yanapita Mara kwa Mara zimetoa nyufa nyingi!Nyufa zinaanzia chini na kuishia dirishani,zingine zimepitiliza!Nimeambatanisha na

16603834283003700171213819974784.jpg
16603834789678175556070831256357.jpg
16603835119138358122472337997349.jpg
16603835788994206757406927333929.jpg
 
Hiyo nyumba juu ya dirisha ulisuka lenta?
Lenta sikuweka!Lakini mbona hata walioweka lenta nyufa zimetokea chini ya dirisha!!!Pia kinachonichanganya hivyo ni viwanja vya kupimwa vya serikali
 
Sawa,sasa nini kifanyike?
Nimechunguza kwa haraka harska naona vitu hivi;
1. Hujaweka prince beam yaani nondo kwenye msingi.
2. Hujaweka beam/lenta tofali zimepanda hadi juu tu.

Huu ni ujenzi hafifu sana ulifaa uombe ushauri kabla ya kujenga.

Ungeweka beam ningekushauri uweke chicken wire then upige plasta upya ungekomesha hizo nyufa
 
Lenta sikuweka!Lakini mbona hata walioweka lenta nyufa zimetokea chini ya dirisha!!!Pia kinachonichanganya hivyo ni viwanja vya kupimwa vya serikali
Kitaalam unapaswa kuweka lenta juu ya msingi na juu ya ukuta yaani walling
 
Wanajf ninaomba ushauri wa haraka wa nini kifanyike kwani kuta za kakibanda kangu kaliopo Katavi mahali ambapo matetemeko makubwa ya ardhi mithili ya mabomu yanapita Mara kwa Mara zimetoa nyufa nyingi!Nyufa zinaanzia chini na kuishia dirishani,zingine zimepitiliza!Nimeambatanisha na

View attachment 2322864View attachment 2322866View attachment 2322867View attachment 2322869
Utagombana na atakaye rekebisha tu umejenga hovyo sana toka msingi mpaka lenta hakuna. Kama eneo lina matetemeko mengi bado unafanya mambo hovyo hovyo ? Bomoa jenga vizuri
 
Nimechunguza kwa haraka harska naona vitu hivi;
1. Hujaweka prince beam yaani nondo kwenye msingi.
2. Hujaweka beam/lenta tofali zimepanda hadi juu tu.

Huu ni ujenzi hafifu sana ulifaa uombe ushauri kabla ya kujenga.

Ungeweka beam ningekushauri uweke chicken wire then upige plasta upya ungekomesha hizo nyufa
Duh!Sasa nini kifanyike?Mbona nimechanganyikiwa
 
Nimechunguza kwa haraka harska naona vitu hivi;
1. Hujaweka prince beam yaani nondo kwenye msingi.
2. Hujaweka beam/lenta tofali zimepanda hadi juu tu.

Huu ni ujenzi hafifu sana ulifaa uombe ushauri kabla ya kujenga.

Ungeweka beam ningekushauri uweke chicken wire then upige plasta upya ungekomesha hizo nyufa
Hii ndio hasara ya Ujenzi wa JF wa kuulizana nina milioni 5 naweza kujenga nyumba ya vyumba vitatu? Na watu wanashabikia inawezekana.
 
Hapana Mimi nilijenga haraka haraka,nilisumbuliwa sana nilikokuwa nimekaa miaka ya 2014 nilipokuwa Katavi.Kinachonipata Mimi kimewapata hadi jirani zangu.Ninaomba mnisaidie cha kufanya kwani Nina hali ngumu hata kihisia mawazo ni mengi
 
Back
Top Bottom