Msaada wa haraka pesa ipo akaunti ya mahakama

Msaada wa haraka pesa ipo akaunti ya mahakama

Uncle Mabiki

Member
Joined
Sep 22, 2018
Posts
77
Reaction score
77
Wadau wa Sheria,Iko hivi Mimi kama msimamizi wa mirathi,nilifatilia mpaka Hela zikawa zimetumwa kwenye akaunti ya mahakama, warithi wakajaza zile form za mgao,tukambiwa tusuburi Hela zitaingia kwenye hizo akaunti za warithi
Swali? Je inachukua muda gani mpaka mahakama kuingiza hizo pesa kwa walengwa? Miezi miwili sasa
 
Mambo ya mirathi hayanaga uharaka, sijui kwa nini!...Hata miye ndugu yangu kafuatilia kakwamia hapo; wakasema mfumo haufanyi kazi mpaka mwaka mpya wa fedha wa serikali. Leo tunakaribia kumaliza robo mwaka!
 
Duh Kweli Bongo Nyoso,yaani taratibu zote zimeisha imebaki muhasibu kuclick tu button ya Laptop ndani ya dakika 3 muhamala usome watu wanangojea mwaka😮‍💨
 
Wafungulie kesi hapohapo mahakamani kwa kuchelewesha malipo yako na uwadai fidia ya usumbufu, siku nyingine hawatarudia ujinga wao!!

sio rahisi kama unavyosema, mara nyingi wenye power ya kuprocess na kulipa hizo pesa wanakuwa ni mahakama za juu, tofauti na mirathi iliposikilizwa,

mfano sisi mirathi ilikuwa mahakama ya wilaya ya kinondoni, ila malipo ya pesa yakalipwa na mahakama ya rufaa ya kule kivukoni
 
Mambo ya mirathi hayanaga uharaka, sijui kwa nini!...Hata miye ndugu yangu kafuatilia kakwamia hapo; wakasema mfumo haufanyi kazi mpaka mwaka mpya wa fedha wa serikali. Leo tunakaribia kumaliza robo mwaka!
Mwaka mpya wa fedha umeanza tarehe Moja mwezi wa saba
 
Mazingira ya rushwa hayo, wanasubiri ujiongeze. Mahakama zetu zinatia aibu Kuna wakati wanaomba waziwazi kabisa. Kama hutaki usumbufu wape kitu kidogo mambo yatakamilika.
 
Back
Top Bottom