Habari wanajamvi
Naombeni msaada kuna mdada wa kazi nlikua naishi nae hapa nyumbani ametoroka usiku,na kaondoka na begi la ndugu yangu
Katokea ifakara kyelekea morogoro mjini
Kwanza huyo binti hakwenda huko Ifakara isipokuwa katoroshwa na inawezekana akawa jirani yako!!
Kinaxhofanyika ni kuwa ,Wewe unaweza ukawa unatafuta Binti wa kazi. Unawaulizia watu mbali mbali.
Anajitokeza mtu anakuambia msichana kapatikana sehemu Fulani lakini yupo Mkoa Fulani hivyo tuma pesa.
Ukimtumia pesa ya nauri ya mkoa huyo jamaa anamlubuni Binti wa mtaani na kumtorosha na kumpeleka anakohitajika.
Wewe unajua Binti katoka Mkoa kumbe alikuwa yupo Dar na nauri ni buku mbili tu ila wewe umeambiwa katoka kigoma na ulimpa jamaa nauri ya kutoka kigoma. Hivyo hiyo nauri anaitafuna.
Hata huyo binti yako hakwenda kwao yupo hapa hapa Dar na basdhi ya majirani zako wanajua alipopelekwa na watasikitika nawewe.
Mimi ilishanitokea jirani yangu alikuwa anatorosha wasichana wangu.
Wasichana watatu kwa nyakati mbali mbali alifanikiwa kuwatorosha.
Huyu wa mwisho ndipo alipokamatwa na wife .
Huyu jirani tunatoka Mkoa mmoja yeye na mkewe na Mimi na mke wangu wote Mkoa mmoja.!
Hivyo ilikuwa kama ndugu!
Jamaa alipata mgeni shemeji yake akaomba hifadhi sehemu ya kulala.
Kwakuwa wife hakuwepo nilimruhusu alale huyo shemeji yake na msichana wakazi na alikaa miezi miwili ilihali aliomba siku tatu tu.,!
Siku Binti anatoroka ,Huyo mdada hakuja kulala.
Halafu saa kumi na moja alfajiri yule mke wa jamaa akanpigia simu mke wangu kumuuliza et maji yanatoka!
Wife anaamka ndo anakuta na msichana hayupo ndani kamuacha mtoto peke yake.
Baadae jioni mke wangu alienda kwao akawakuta.huyo mke wa jamaa na yule dada aliyekuwa analala kwetu..
Wife aliomba simu ya huyo mdada akamwambia naomba nimpigie MTU simu yako ,
Yule dada akampa wife simu yake ila hawakujua nani anampigia.
Wife alipochukua simu akaipiga namba ya Mama wa yule msichana WA KAZI Cha ajabu likatokea jina la huyo mama yake na msichana WA KAZI.
Yule mama akijua anaongea na mwenye simu akaanza kuropoka vipi ameshafika mwanangu huko ulikompeleka?
Wife akawa anaitikia tu yeye hakugundua anaongea na wife.
Baadae yule mwenye simu akagundua anaongea na mama wa Binti hivyo akafanya varangati la kuitaka simu yake .
Mchezo ukaanzia hapo elezeni mlikompeleka Binti yangu wa kazi la sivyo polis.
Walipobanwa na kuitiwa polis walimfuata na kurudisha Binti.
Binti Alipofika alipoulizwa alieleza Kila kitu mbele ya mjumbe na mpango wa kumtorosha na Alipofika kule alielezwa na watoto wa huyo bosi wake mpya kuwa kwani wewe umekuja kufanya kazi badala ya dada AHADI aliyeonfoka juzi?
Na huyo AHADI alikuwa ni msichana wetu wa kazi.
Walipoulizwa kama kweli na huyo msichana wetu wa kwanza walimtorosha walikubali kufanya hivyo na wakaomba radhi mbele ya mjumbe na majirani.
Kipindi msichana ametoroka mke wa huyo jamaa alikuwa anasambaza taarifa kuwa wife anawatesa wasichana wa kazi ndo maana wanatoroka.
Sitori ni ndefu sana. Lakini just kuwa Kuna asilimia kubwa jirani kahusika na huyo msichana yupo hapa hapa Dar Wala huko kwao hayupo.Chunguza vizuri