Msaada wa haraka unahitajika

Msaada wa haraka unahitajika

Hyo mtoto n mdokozi by nature ,yan hata km sijamiadhibu mm ataadhibiwa na wengne
 
Mm ni mwanamke
Haaa pole je mshahara ulikuwa unamlipa vizuri,, je alikuwa Kesha pevuka, km Ndiyo unamtambua kijana aliyekuwa karibu naye maana yangu nikwamba usimuilize huyo kijana atakataa tafuta watu walio karibu na huyo kijana, ukijibu nitakuswalika maswali mengine
 
Haaa pole je mshahara ulikuwa unamlipa vizuri,, je alikuwa Kesha pevuka, km Ndiyo unamtambua kijana aliyekuwa karibu naye maana yangu nikwamba usimuilize huyo kijana atakataa tafuta watu walio karibu na huyo kijana, ukijibu nitakuswalika maswali mengine
Alilipwa jioni alfajiri akaondoka na pia amekaa mwezi mmoja ,na sijawah kumuona akiwa na mazoea na mtu hko nnje
 
Ajira ya watoto-Ulimchukua akiwa na umri sahihi?

Elimu kwa wote- Hukumkatisha masomo?

Usafirishaji binadamu- ulimpataje akafika kwako, una ushahidi wa hiari yake?

Sheria za kazi-Una ushahidi wa malipo ya mshahara wake, yalikuwa yanakidhi kima cha chini kwa wafanyakazi wa majumbani?

Angalia kibao kisije kukugeukia wewe.
She is above eighteen,kazi hajaanzia hapo kwa maelekezo yake kashafanya nyumba kadhaa.pia aliacha shule wazazi wakamsusa,mshahara sijui lkn ilikua 100k
 
She is above eighteen,kazi hajaanzia hapo kwa maelekezo yake kashafanya nyumba kadhaa.pia aliacha shule wazazi wakamsusa,mshahara sijui lkn ilikua 100k
Na kazi alitafuta mwenyewe hakulazimishwa
 
mpaka mtu anatoroka ujue kuna kaunyama mmemtendea

watu wa Dar mna roho mbaya sana
Hapana ,kama hujawahi kuishi na wafanyakazi huwezi jua.

Kiufupi wapo majirani huwarubuni wafanyakazi wa ndani na kuwaambia watoroke kwasababu ya kumkomoa au kuwapeleka kwa ndugu zao wengine.

Pili,Kuna watu hupewa pesa kutafuta wafanyakazi hivyo anapomuona yupo kwako anamlaghai Binti kuwa Kuna Kazi na mshahara wake ni mkubwa.

Binti akishakubali ,Yule jamaa anamtorpsha huyo binti na anampigia simu yule anayehitaji mfanyakazi kuwa Binti kapatikana yupo Mkoa Fulani labda Mwanza n.k hivyo yule anauetafuta mfanyakazi atamtumia huyu jamaa hiyo nauli ya mkoa ili hali mfanyakazi hakutoka Mkoa Bali kamwiba hapo hapo Dar nauri ni buku hizo zingine zinakuwa na manufaa kwake.
 
Habari wanajamvi
Naombeni msaada kuna mdada wa kazi nlikua naishi nae hapa nyumbani ametoroka usiku,na kaondoka na begi la ndugu yangu
Katokea ifakara kyelekea morogoro mjini
Kwanza huyo binti hakwenda huko Ifakara isipokuwa katoroshwa na inawezekana akawa jirani yako!!

Kinaxhofanyika ni kuwa ,Wewe unaweza ukawa unatafuta Binti wa kazi. Unawaulizia watu mbali mbali.

Anajitokeza mtu anakuambia msichana kapatikana sehemu Fulani lakini yupo Mkoa Fulani hivyo tuma pesa.

Ukimtumia pesa ya nauri ya mkoa huyo jamaa anamlubuni Binti wa mtaani na kumtorosha na kumpeleka anakohitajika.

Wewe unajua Binti katoka Mkoa kumbe alikuwa yupo Dar na nauri ni buku mbili tu ila wewe umeambiwa katoka kigoma na ulimpa jamaa nauri ya kutoka kigoma. Hivyo hiyo nauri anaitafuna.

Hata huyo binti yako hakwenda kwao yupo hapa hapa Dar na basdhi ya majirani zako wanajua alipopelekwa na watasikitika nawewe.

Mimi ilishanitokea jirani yangu alikuwa anatorosha wasichana wangu.

Wasichana watatu kwa nyakati mbali mbali alifanikiwa kuwatorosha.

Huyu wa mwisho ndipo alipokamatwa na wife .

Huyu jirani tunatoka Mkoa mmoja yeye na mkewe na Mimi na mke wangu wote Mkoa mmoja.!

Hivyo ilikuwa kama ndugu!

Jamaa alipata mgeni shemeji yake akaomba hifadhi sehemu ya kulala.

Kwakuwa wife hakuwepo nilimruhusu alale huyo shemeji yake na msichana wakazi na alikaa miezi miwili ilihali aliomba siku tatu tu.,!

Siku Binti anatoroka ,Huyo mdada hakuja kulala.

Halafu saa kumi na moja alfajiri yule mke wa jamaa akanpigia simu mke wangu kumuuliza et maji yanatoka!

Wife anaamka ndo anakuta na msichana hayupo ndani kamuacha mtoto peke yake.

Baadae jioni mke wangu alienda kwao akawakuta.huyo mke wa jamaa na yule dada aliyekuwa analala kwetu..

Wife aliomba simu ya huyo mdada akamwambia naomba nimpigie MTU simu yako ,

Yule dada akampa wife simu yake ila hawakujua nani anampigia.

Wife alipochukua simu akaipiga namba ya Mama wa yule msichana WA KAZI Cha ajabu likatokea jina la huyo mama yake na msichana WA KAZI.

Yule mama akijua anaongea na mwenye simu akaanza kuropoka vipi ameshafika mwanangu huko ulikompeleka?

Wife akawa anaitikia tu yeye hakugundua anaongea na wife.

Baadae yule mwenye simu akagundua anaongea na mama wa Binti hivyo akafanya varangati la kuitaka simu yake .

Mchezo ukaanzia hapo elezeni mlikompeleka Binti yangu wa kazi la sivyo polis.

Walipobanwa na kuitiwa polis walimfuata na kurudisha Binti.

Binti Alipofika alipoulizwa alieleza Kila kitu mbele ya mjumbe na mpango wa kumtorosha na Alipofika kule alielezwa na watoto wa huyo bosi wake mpya kuwa kwani wewe umekuja kufanya kazi badala ya dada AHADI aliyeonfoka juzi?

Na huyo AHADI alikuwa ni msichana wetu wa kazi.

Walipoulizwa kama kweli na huyo msichana wetu wa kwanza walimtorosha walikubali kufanya hivyo na wakaomba radhi mbele ya mjumbe na majirani.

Kipindi msichana ametoroka mke wa huyo jamaa alikuwa anasambaza taarifa kuwa wife anawatesa wasichana wa kazi ndo maana wanatoroka.

Sitori ni ndefu sana. Lakini just kuwa Kuna asilimia kubwa jirani kahusika na huyo msichana yupo hapa hapa Dar Wala huko kwao hayupo.Chunguza vizuri
 
Back
Top Bottom