Msaada wa haraka unahitajika

Msaada wa haraka unahitajika

Cha-phile

Member
Joined
Sep 20, 2012
Posts
66
Reaction score
9
Habari za asubuhi wana jukwaa. Mimi ni mwanafunzi katika chuo kikuu cha Mtakatifu Agustino cha Tanzania, Mwanza mwaka wa tatu 'BAED' na nimepanga kufanya utafiti (Research) juu ya mtazamo wa walimu juu ya madaraja mapya ya ufaulu yaliyotolewa mwaka jana.

Naombeni msaada kwa yeyote anaejua chapisho, utafiti uliofanywa au hotuba iliyotolewa kuhusiana na madaraja mapya, kama vile tarehe, aliyetangaza, sababu za mabadiliko na maoni ya wadau wa elimu.

AHSANTENI NA KARIBUNI KWA MAWAZO YANAYOJENGA
 
Ndugu yangu,

Kutafuta vyanzo vya utafiti ni sehemu ya utafiti wenyewe....

Usipende kutafuniwa sababu ni mara chache sana kujifunza kwa kutumia njia hii.

Tafakari.
 
Habari za asubuhi wana jukwaa. Mimi ni mwanafunzi katika chuo kikuu cha Mtakatifu Agustino cha Tanzania,Mwanza mwaka wa tatu 'BAED' na nimepanga kufanya utafiti (Research) juu ya mtazamo wa walimu juu ya madaraja mapya ya ufaulu yaliyotolewa mwaka jana. Naombeni msaada kwa yeyote anaejua chapisho, utafiti uliofanywa au hotuba iliyotolewa kuhusiana na madaraja mapya, kama vile tarehe, aliyetangaza, sababu za mabadiliko na maoni ya wadau wa elimu. AHSANTENI NA KARIBUNI KWA MAWAZO YANAYOJENGA
mm nakushauri ungebadilisha topic mana inaweza kuwa ngumu sana kwako kupata secondary data ukizingatia kitu chenyewe hakina hata mwaka mmoja toka kifanyike pia, kupata data kwa wahusika yaani primary data inaweza kukusumbua sana mana wengi wanaweza kuogopa kukupa data kuhofia kibarua chao,yote kwa yote muamuzi wa mwisho ni wewe mwenyewe
 
Back
Top Bottom