Pole sana,hlo tatzo unalozungumzia hata mimi lilinipata nilipokuwa namsaidia rafiki yangu kujaza hizo programs.
Nilijaribu kwenye simu ikanizingua.
Nikaenda internet cafe(wanatumia internet explorer) ikagoma.
Kwa hiyo mtindo ndo ukawa kama huo unaokukumba wewe.Ukitazama lile tangazo lenye maandishi mekundu,baada ya kulogin,wamekuambia ujaribu kutumia browser nyingine kama Operamini,Firefox,Google Chrome nk.
Kwa hyo kama wewe ulikuwa unatumia browser tofauti,jarbu kutumia hzo walizosema.
Pia,jaribu kufanya application zako kwenye computer nyingine,sanasana yenye Firefox ndo haizingui. Hivi ndo nilivyofanikiwa kumjazia yule rafiki yangu.