Msaada wa hili, miguu inakufa ganzi

Msaada wa hili, miguu inakufa ganzi

Pole,
Kuna mambo zaidi Zaidi nahitajji kujua:
1: Ganzi ilianzia wapi, na mpaka sasa iko sehemu gani mguu/miguu?
2: Ilianza miguu yote kwa pamoja?
3: Una maumivu yoyote kwenye uti wa mgongo?
4: Unafanya kazi zote nzito za kuinama?
Ilianzia mguu wa kushoto, ila mguu wa kulia pia ipo kwa mbali na inasogea mpaka mapajani kuelekea kiunoni

Mguu mmoja mwingine ukafuata ila mguu wa kulia ipo kidogo sana

Sometimes nikiwa job nikikaa sana maumivu ya mgongo yanakuwepo kwa mbali amabyo yanaisha baada ya muda mfupi

Kazi zakuinama sio sana , mara nying ni kukaa
 
Tiba je au ni mpaka leo tatizo bado lipo
Kuhusu Tiba walimwambia hakuna maana alikuwa amechelewa sana, maana alianza kulalamika miguu inakufa ganzi kama miaka 5 hivi upande wakushoto ndio alikuwa analalamika zaidi. Ila kuna dawa walimwandikia za kuwa anaenda kuchukua kila mwezi now tatizo limepungua.

pia pressure alikutwa nayo ila daktari alisema haina uhusiano na hilo tatizo. Jaribu kwenda hospital ufanyiwe uchunguzi.

Usipende kufanya kazi nzito,.kusimama muda mrefu,.kusafiri safiri safari za mbali inaongeza tatizo maradufu
 
Kama sio mshipa wa ngiri, unadalili kama sukari, pressure, je kiu ya maji haikupati usiku? Unakojoa mara kwa mara?
 
Ilianzia mguu wa kushoto, ila mguu wa kulia pia ipo kwa mbali na inasogea mpaka mapajani kuelekea kiunoni

Mguu mmoja mwingine ukafuata ila mguu wa kulia ipo kidogo sana

Sometimes nikiwa job nikikaa sana maumivu ya mgongo yanakuwepo kwa mbali amabyo yanaisha baada ya muda mfupi

Kazi zakuinama sio sana , mara nying ni kukaa
Tatizo linaweza kuwa mgandamizo/ nerve intrapment/radiculopathy kwenye mshipa wa fahamu, kuanzia/kwenye usawa wa kiuno kwenda juu kidogo.

Sababu: Itatafutwa kwa vipimo zaidi, kulingana na maoni ya mtaalamu.

NB: Mwone Neurophysician/daktari bingwa wa mishipa ya fahamu au internal medicine physician/daktari bingwa wa magonjwa ya ndani kwa hospitali tajwa hapo juu.
 
Mkuu Fanya mazoezi ya jogging kwa wiki Moja ukiwa na viatu na tracksuit toka jasho la kutosha halafu wiki ijayo lete majibu. Utanishukuru badae
Hivi mtu anaganzi halafu afanye jogging kweli kila mtu na,zake kama hawezi simama vizuri ndio jogging anaweza fanya
 
Tatizo linaweza kuwa mgandamizo kwenye mshipa wa fahamu, kuanzia usawa wa kiuno.

NB: Mwone Neurophysician/daktari bingwa wa mishipa ya fahamu au internal medicine physician/daktari bingwa wa magonjwa ya ndani kwa hospitali tajwa hapo juu.
Thanks
 
Habarini wadau,

Kama wiki sasa nimepata hili tatizo la miguu kufa ganzi, wa kushoto ndio sana mpaka sasa nakuwa siu feel kwa kiasi kikubwa, nikajua itaenda ikipungua ila naona ipo same au kama inapungu basi taratibu sanaaa kiasi chja kwamba siwezi jua,

Kama kuna yoyote mwenye ujuzi au alishawahi kukumbana na hili akapona msaada wako unahitajika

Hospital nimeenda mara mbili mara ya mwisho leo, mara ya kwanza niliambiwa inaweza kuwa ni upungufu wa Vitamin b12 maana dalili pia zinaambatana na ngozi kuwa kavu sana uchovu n.k nikachoma sindano kadhaa za vitamin b12 pamoja na vidonge ila mpaka leo maendeleo ni hafifu tu, leo nikaenda kucheki sukari pamoja na syphilis kwa mujibu wa dokta maana niliambiwa asilimia kubwa itakuwa ni sukari ila majibu yote hayo yamekuwa negative

Msaada kwenye hili tafadhali maana nahisi ni nerve damage somewhere ila sijui cause ndio inaniogopesha nahofia isije ikawa permanent hii feeling which is bad sana kwa upande wangu.
Pole Mkuu kwa maradhi yako Nitafute kwa wakati wako ili niweze kukutibia maradhi yako uguwa pole.
 
Maybe, sijataka kuanza na haya kwanza ngoja nihangaike na menngine ila ntawachek wazee nao
Tafuta majani ya mlonge, ask me hapa hapa nikuambie namna ya kukausha.

But kama unao huu mti kwako anza kwa kupurura na kutafuna majani yake
 
Back
Top Bottom