Msaada wa Imani

Msaada wa Imani

Mkuu haya maandiko hawapewi watu wanafiki wanapewa wajinga.

Usiwe mwepesi mara zote kutoa andiko.

Hawa wanajibiwa kwa kutumia vichwa vyao wenyewe.
[emoji1] [emoji1] [emoji1] nilijua yupo serious anahitaji msaada
 
Wakristo wenzangu, hebu acheni kubishana na hawa wana wa giza kwa kuwa walikwisha laaniwa kabla ya kuumbwa kwa ulimwengu huu.
Analeta mada hapa ili waonekane wao ndio wenye hekima zaidi na wamechagua fungu lililo jema kumbe ni baya.
Watu wanaoamini katika kusaidiwa na pepo wachafu(majini), kuuwana na kulipiza visasi.
 
Jaffar;
Nimeshakueleza mara kadhaa, unapo mlinganisha Mungu Muumba wa vyote na alichokiumba una shida. Mungu hakuja kuuhukumu ulimwengu bali kuuponya ulimwengu. Kulikuwa hakujawepo mpango mwingine ka huu hivyo mfano wako wa mwanagu James na labda nimwite jirani Yuda haviko hivyo!!
Ukombozi wa Mungu kwa ulimwengu ni tofauti. Tunasoma hivi; Yoh. 3 : 16 Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanaye pekee, ili kila mtua amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. 17 Maana Mungu hakumtuma Mwanaye ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe kwa yeye. 18 Amwaminiye yeye (Huyo Mwana) hahukumiwi; asiyemwamini (Huyo Mwana pekee) amekwisha hukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa Mungu.
Jaffar, Kwa nini tunataka kumfundisha Mungu?? Tulimkosea sisi, halafu tunataka atusamehe tunavyotaka sisi wala si kama atakavyo yeye. Huku tunajitia nguvu kuwa Mungu wetu aweza kufanya lolote. Kuna kasoro mahali fulani. Huenda tunajifanya vipofu na viziwi wenyewe.
Angalia Yoh. 3 : 19
Na hii ndiyo hukumu; ya kuwa nuru ilikuja ulimwenguni, na watu wakapenda giza kuliko nuru; kwa maana matendo yao yalikuwa maovu.

Amini kuwa ulimkosea Mungu na ni yeye Mungu tu awezaye kukusamehe. Tiyari kisha kusamehe, amini tu.

Hayo yote nimeshakuelewa Ndugu. Ni sawa na kusema Mungu pia anaweza akaamua sasa kua shetani na sisi kama wanadamu tujae kimya tuamini tu!! Tatizo linabaki kwanini awe Mungu wa KUUA? yaani kama mfano niliokupa hapo juu. Unao uwezo wa kusamehe halafu hutaki kusamehe mpaka amuue mwanae? Tena kipenzi? Mi nadhani sheria hizi tukianza kuzitumia wanadamu ndio italeta akili ya jambo la ajabu alilolifanya Mungu wenu!

Sasa hebu nikupe hukumu ya dhambi katika uislamu.
-Ukitenda dhambi ukatubia kwa dhati kwa Mungu na kutokurudia basi Mungu anasema Yeye ni mwingi wa msamaha. Atakusame.
-siku ya hukumu kila nafsi itahukumiwa kwa matendo yake hapa duniani. Yaani ule Mzigo ambao Yesu mwenyewe alisema kila mmoja ataubeba wake mwenyewe.(sio yeye kuubeba wako kama wengi mnavyoamini)
- mwisho kabisa wenye kufaulu watapata firdausi na wenye kufeli (wale ambao ukweli uliwafikia wakapuuza na kukanusha na kuendeleza uovu)watawekwa katika Jahhanam.

Sasa hebu linganisha maalezo hayo na uone kipi ni sahihi na cha haki.
 
Okay then. Kama unaamini biblia naomba nikuulize swali. Je unaamini biblia haijabadilishwa na wala haina makosa?
..makosa Gani unamaanisha mkuu,the whole logic au makosa ya uandishi katika harakati za kutafsiri??
 
Achana nae fanya mambo mengne. Utapasuka kichwa.
Uislam kaja nao mwarabu na sijui aliutoa wap???
Ukristo kaja nao mzungu. Sijui na yeye aliuokota wap.

Lakin yote hayo mapazia ya kubeba vito vya saman. Sasa wwe jichanganye kuuliza maswal ya kipuuz wakat hakuna aliyekufa akafufuka kuja kuleta aliyoyaona huko. AMIN MUNGU BASI
Niamini Mungu yupi?
 
..makosa Gani unamaanisha mkuu,the whole logic au makosa ya uandishi katika harakati za kutafsiri??
Makosa ya kimaandishi kama sehemu moja iseme jeshi la suleiman lilikua na wa tu 1010 na sehemu nyingine iseme 1100.
 
..naam ni errors ambazo haziepukiki Mkuu but nevertheLess LOGIC ni genuine!!
Boss, Kitabu cha Mungu hakitakiwi kua na Errors ! Unaamini Mungu anaweza kua na kitabu kama hicho?
Nikupe mfano wa kifo cha yuda Escariot
Matendo 1:18 alikua shambani akajikwaa na kuanguka na matumbo yake yakapasuka. hali yakua kinyume kabisa na maelezo hayo Matayo 27:5 alienda akajinyonga.

Hebu jaribu kutafakari. Biblia moja kifo cha mtu mmoja maelezo mawili tofauti kabisa.

Sasa tujue wazi Mungu si mwanadamu wa kufanya makosa kama haya na kitabu cha Mungu hakiwezi kua na kisa hata Moja.
 
Mkuu acha kujichanganya na vitu vyenye kutumia akili ya kawaida kufikiri.

Wewe unaamini asilimia mia moja quran haina error yoyote ile????
 
Imani ni kitu ambacho kupingana nacho ni kazi.
Wakritu tunaamini kuwa Yesu ni Mungu. Nikiwa na maana ya kwamba Mungu ni mmoja lakini katika nafsi tatu, yaani Mungu baba, Mungu mwana (Yesu) na Mungu roho mtakatifu.
Kwa mfano rahisi ni sawa na kusema gari ni moja lakni lina matair, milango taa n.k.
Hivyo ndivyo tunavyo amini, kwa hyo Yesu ni Mungu. Na tunazidi kuamini maana kila tumuombapo anajibu sala zetu kwa kutufanikishia yale tunayo yaomba. Pia tume kuwa tukishuhidia watu wakiponywa na wachungaji kwa msaada wa jina la Yesu (yaani Mungu anawaponya watu).
Kama una swali uliza
 
Mkuu acha kujichanganya na vitu vyenye kutumia akili ya kawaida kufikiri.

Wewe unaamini asilimia mia moja quran haina error yoyote ile????
Kuna maandiko hapo nimeweka boss. Kama unaweza kujibu naomba ujibu. Halafu ndio twende kwenye Quran. tusiwe tunaruka ruka kama panzi. Kama unaamini Quran in errors utaleta maandiko unayohisi yana tatizo tuyajadili. Hakuna haja ya POVU.
sasa nipe maelezo kuhusu maandiko hayo ndio tuendelee.
 
Wapi povu,, unaamini quran iko perfect 100%???? jibu hapa.
 
Imani ni kitu ambacho kupingana nacho ni kazi.
Wakritu tunaamini kuwa Yesu ni Mungu. Nikiwa na maana ya kwamba Mungu ni mmoja lakini katika nafsi tatu, yaani Mungu baba, Mungu mwana (Yesu) na Mungu roho mtakatifu.
Kwa mfano rahisi ni sawa na kusema gari ni moja lakni lina matair, milango taa n.k.
Hivyo ndivyo tunavyo amini, kwa hyo Yesu ni Mungu. Na tunazidi kuamini maana kila tumuombapo anajibu sala zetu kwa kutufanikishia yale tunayo yaomba. Pia tume kuwa tukishuhidia watu wakiponywa na wachungaji kwa msaada wa jina la Yesu (yaani Mungu anawaponya watu).
Kama una swali uliza
Kwa maana hiyo unataka kusema wasabato sio wakristo maana wao hawaamini kama Yesu ni Mungu.
Na kama Yesu ni Mungu tukubali basi Mungu huyo nae ana Mungu wake. Na yule Mungu wa Yesu ndio sisi tunamuabudu.

-Hivi hujui hata baniani anaomba sanamu la ng'ombe na anajibiwa anachokiomba? Sasa kwa mantiki hiyo je naye akisema Ngombe ni Mungu wa Kweli utamuelewa?

-Umeleta mfano wa Gari kua moja na mfano wa taa. Hivi Taa peke yake unaweza kuuita Gari? Hapana huwezi. Lakini gari inaweza kutembea bila taa.

Fahamu kua Nafsi ya Baba ndio kuu kuliko nafsi hizo zingine.
 
Imani ni kitu ambacho kupingana nacho ni kazi.
Wakritu tunaamini kuwa Yesu ni Mungu. Nikiwa na maana ya kwamba Mungu ni mmoja lakini katika nafsi tatu, yaani Mungu baba, Mungu mwana (Yesu) na Mungu roho mtakatifu.
Kwa mfano rahisi ni sawa na kusema gari ni moja lakni lina matair, milango taa n.k.
Hivyo ndivyo tunavyo amini, kwa hyo Yesu ni Mungu. Na tunazidi kuamini maana kila tumuombapo anajibu sala zetu kwa kutufanikishia yale tunayo yaomba. Pia tume kuwa tukishuhidia watu wakiponywa na wachungaji kwa msaada wa jina la Yesu (yaani Mungu anawaponya watu).
Kama una swali uliza
Hao wenye kupona kwa kutumia jina la Yesu ni pamoja na mitume wa uongo? tunajua kuwa kuna wengine ni matapeli ila hatuoni tofauti ya hao matapeli na wasio matapeli wote hutumia jina la Yesu kuponya.

Je,tuamini kuwa ni jina la Yesu ndiyo huponya?
 
Mungu baba...mungu mwana...mungu roho mtakatifu.....!!amani ya bwana iwe nanyi. ...asiejua mAana haambiwi mAana hapa mtabishana mpaka...ni vema Kila mtu aheshimu imani ya mwenzie tu
 
Wapi povu,, unaamini quran iko perfect 100%???? jibu hapa.
Mie naamini iko correct. Labda uelewa wako ndio unaweza kua hauko correct. So kabla hatujahamia huko nipe jibu kwanza je wewe unaamini biblia iko correct au imevurugwa? Na kama unaamini iko correct nipe maelezo hayo ya kifo cha yuda.
 
Mungu baba...mungu mwana...mungu roho mtakatifu.....!!amani ya bwana iwe nanyi. ...asiejua mAana haambiwi mAana hapa mtabishana mpaka...ni vema Kila mtu aheshimu imani ya mwenzie tu
Amani ya bwana iwe nasi. Kwa kiarabu ndio hua tunasema Asalaam aleykum.
Na jibu lake hua waaleykum Salaam yaaani Amani ya Mungu iwe nawe pia!
Vyema. Sasa hapo sijaelewa unamaana gani yaani ni miungu mitatu? Ama Mungu Mmoja? Na kama ni Mungu mmoja je nafsi ipi katika hizo tatu ina mamlaka zaidi ya zingine?
 
Back
Top Bottom