Msaada wa kifedha wa China kwa Afrika "kupiga breki"?

Msaada wa kifedha wa China kwa Afrika "kupiga breki"?

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,116
Reaction score
1,121
fdsafafads.jpg

Hassan Zhou

Hivi majuzi, makala ya gazeti la Financial Times yenye kichwa "Mkopo wa China kwa Afrika Wapiga Breki" imenukuliwa na vyombo vya habari vya ndani na nje ya Afrika. Ikitaja hatari ya kushindwa kulipa madeni katika baadhi ya nchi za Afrika, makala hiyo ilisema China "imetuma ishara yenye uangalifu mkubwa" na "itapiga breki katika kutoa mkopo kwa Afrika". Makala hiyo pia ilirudia tena kashfa dhidi ya kile kinachoitwa "mtego wa madeni," ikidai kwamba "kukopa kwa China kwa asili ni uporaji."

Ikisimulia hadithi ya kubuni inayodai kwamba Uganda ilikuwa katika hatari ya kupoteza mali kuu kwa China kutokana na kushindwa kulipa madeni, makala hiyo iliwanukuu wale wanaojiita wachambuzi wakisema masharti ya kandarasi ya miradi inayofadhiliwa na China ni "sumu". Lakini imekubali kwamba licha ya shutuma kwamba China inaweza kunyakua mali ya kimkakati, "hii haijawahi kutokea". Jambo la kushangaza ni kwamba, kwa mujibu wa ripoti ya Deutsche Welle, wakopeshaji wa Ulaya wana historia zaidi ya kushtaki mali za serikali za nchi za Afrika kuliko China.

Mwelekeo ulio wazi siku hizi ni kwamba nchi za magharibi zitatumia hadithi zao za "mtego wa madeni" kuikosoa China, iwe China inaongeza au kupunguza kasi ya kutoa mikopo kwa Afrika. Nyuma ya maneno potofu ni unafiki wa nchi za magharibi na wivu wao na uhusiano wa kirafiki kati ya China na Afrika. Kimsingi, wana hofu juu ya uwepo wa China katika Afrika, na wanataka tu China ipotee, bila kujali hali hiyo itaathiri maendeleo ya Afrika au la. Lakini kutunga hadithi haina maana, na ni vibaya kuitumia kudhoofisha ushirikiano wa kunufaishana kati ya China na Afrika.

"Wachina wanaonekana kuona fursa za biashara na mustakabali wa Uganda kuwa bora kuliko kampuni za Magharibi," Rais wa Uganda Yoweri Museveni aliambia Reuters katika mahojiano ya hivi karibuni. Aliongeza kuwa "Uganda inajadiliana na kutia saini mikataba na wakopeshaji wa sekta binafsi wa China katika sekta ya kilimo na usindikaji wa mbolea, madini na nguo.

Ni wazi, kitu kinachoweza kuonekana tu vyombo vya habari vya Magharibi katika Afrika ni nchi mbalimbali kutokuwa na uwezo wa kurejesha mikopo iliyoombwa kwa ajili ya miradi muhimu ya miundombinu, na kutokuwa na uwezo wa kusaini mikataba ambayo inakidhi maslahi yao wenyewe. Kiwango hiki cha kiburi hakiwezi kuaminika hadi makala hii katika gazeti la Financial Times ilipoanza kuusema vibaya mustakabali wa kirafiki wa ushirikiano kati ya China na Afrika kwa upande mwingine. Hata hivyo, ni nchi za Kiafrika pekee ndizo zinazostahili kusema kama uwekezaji wa China una manufaa.

Tofauti na nchi za magharibi, ambazo zimekuwa zikipora malighafi kutoka Afrika na kujaribu kubadilisha mifumo yao ya kisiasa, China imekuwa ikiunga mkono kwa dhati maendeleo ya Afrika bila ya masharti ya kisiasa. Hiki ndicho kinachovutia nchi za Afrika. Kama Waraka wa "China na Afrika katika Enzi Mpya: uhusiano wa kiwenzi wenye usawa" unavyosema "Kuanzia 2000 hadi 2020, China imesaidia nchi za Afrika kujenga zaidi ya kilomita 13,000 za barabara na reli, zaidi ya vituo 80 vya nishati kubwa, na kufadhili vituo vya matibabu 130, kumbi 45 za michezo na zaidi ya shule 170."

Mbali na miradi ya miundombinu, ushirikiano wa China na nchi za Afrika umepanuka na kufikia nyanja mbalimbali kama vile kilimo, utamaduni, viwanda, fedha na uchumi wa kidijitali. Ili kusaidia bara la Afrika kupambana na janga la Covid-19, China imetoa dozi zaidi ya milioni 180 za chanjo kwa nchi 53 za Afrika na kamati ya Umoja wa Afrika hadi mwanzoni mwa mwaka huu, na mnamo Novemba 2021 iliahidi kutoa dozi nyingine bilioni 1 za chanjo ya Covid-19 kwa Afrika.

Tukirudi kwenye kile Financial Times ilikiita "breki ya mkopo", si vigumu kuelewa kuwa ni kawaida kwa mikopo ya kisoko inabadilika kufuatia mabadiliko ya mahitaji. Lakini Financial Times pia ilisema ukweli kwamba hakutakuwa na mabadiliko yoyote makubwa katika sera ya China kuhusu Afrika. Katika siku zijazo, China itazingatia zaidi ubora wa miradi ya uwekezaji barani Afrika, hasa miradi inayoweza kukuza uchumi na biashara ya Afrika kupitia mauzo ya nje. Urafiki wa kina kati ya China na Afrika haujengwi kwa siku moja. Hata kama vyombo vya habari vya Magharibi vinajaribu kuuangamiza, uungaji mkono wa China kwa Afrika unabakia kuwa thabiti.
 
Hawa waliodanganya kuhusu Sadam Hussein kua na silaha za maangamizi kisha wakaivuruga Iraq kwa kuua watu na wanaendelea kupora mafuta. Hawa walioivuruga Lybia kwa kuua watu na wanaendelea kupora mafuta na kufanya nchi isitawalike eti leo wanatahadharisha kuhusu China “kupora mali” za Africa!!!!!

Mbona hawasemi mipango yao kuigawa Iraq katika nchi tatu za Wakurd, Shia na Sunni ili wazidi kupora rasilimali zaidi? Njama kama hizo China imezifanya wapi zaidi ya propaganda chafu za magharibi???!!!
 
Ingawaje mahusiano kati ya China na Africa ni ya kuangalia kwa umakini shida ya nchi za Magharibi ni kama vile zimetoka usingizini na kungundua mchina ameshajikita na ananufaika sana Africa.
 
Ikisimulia hadithi ya kubuni inayodai kwamba Uganda ilikuwa katika hatari ya kupoteza mali kuu kwa China kutokana na kushindwa kulipa madeni, makala hiyo iliwanukuu wale wanaojiita wachambuzi wakisema masharti ya kandarasi ya miradi inayofadhiliwa na China ni "sumu"...
Acha waseme Wanaoongea Kiingereza manake tukisema sie Wamatumbi, akina macho_mdiliko, denooJ na Legacy Protectors wengine wanasema tunalipwa na China!!

And it's a matter of time kabla hajmanielewa pale nilipoandika "Wazalendo Fake Mnatumika na Mabeberu Bila Kujijua"!
 
Ingawaje mahusiano kati ya China na Africa ni ya kuangalia kwa umakini shida ya nchi za Magharibi ni kama vile zimetoka usingizini na kungundua mchina ameshajikita na ananufaika sana Africa.
Unaambiwa wanatapatapa kwa sasa...

Na washukuru, kama nilivyowahi kusema kwenye posts zangu za nyuma, Waafrika wenyewe, tena wale wale wanaojifanya wasomi, nao kila siku wamekuwa wakiziimba nyimbo za US bila kujijua!

Na pia washukuru, hata Wachina wenyewe (raia) wameanza kuhoji matumizi makubwa ya pesa yanayofanywa na serikali yao katika kujitanua wakati China kwenyewe mambo si mazuri kivile!

Na kama si hivyo, na ile BRI (Belt and Road Initiative) ya China, mataifa ya magharibi, hususani US wangeanza kutafutana!!

Na kama ulivyosema, hivi sasa Western Countries ndo zimetoka usingizini manake France tayari imeshaandaa mpango wa kukabiliana na China kwa staili zile zile za China, huku USA nao wakiwa wameanzisha Prosper Africa!!

Hapa ndipo pale nchi inapotakiwa kuwa na Wanadiplomasia aina ya JK ambae hawachukui upande!! Unakuta leo anaenda China, akirudi huko anapitiliza moja kwa moja hadi US na kote huko anagonga cheers na head of states!!

Anyway, najua Wazalendo wanadanganyana Tanzania tunao uwezo wa kujitegemea wenyewe huku wakisahau hata taifa kama Israeli tu, hadi kesho bado linategemea backup ya hazina za wakubwa!

Hadi kesho bado nchi za Americas zinakopa, lakini ka-nchi fulani hivi ambako hata kutengeneza toothpick hakajui, kanatamba kenyewe ni tajiri kanakoweza kujiendesha bila mikopo!

Hao hao wanaosema hivyo wape changamoto ya kutengeneza Strategic Development Plan... hawajui hata pa kuanzia!!

Uliza huo utajiri wako ni upi, watakuambia tuna madini kibao...

Yaani hata hawajui kwamba leo hii unaweza kuchimba madini yoooote kutoka kwenye migodi iliyopo na bado hata Mark Zuckerberg peke yake akawa na uwezo wa kuyanunua YOOOOTE na kuyatupa baharini na bado akabaki na utajiri mkubwa!!

Hapo zijamtaja Elon Musk wala Jeff Bezos!

Na utamu zaidi, waulize hivi kwa mfano tunataifisha migodi yetu YOOOOTE na kuwa 100% mali ya serikali! Halafu tukachimba madini yooote sisi wenyewe... yaani dhahabu, almasi, Tanzanite, you name it! Lakini pamoja na hayo, nchi ZOOOTE duniani ZIKAGOMA kununua hayo madini na products zinazotokana na madini!

TELL ME, hivi hii nchi tajiri ikikosa beberu wa kununua hayo madini, taifa hili tajiri litayatumia vipi madini hayo?! Kutengeneza vikuku, ama?!

Ukitafakari hayo ndipo mtakapojua nyie ni maskini tu!!
 
Back
Top Bottom