Msaada wa kimawazo: Nahisi naanza kupata depression

Sasa huu ndio ushauri wa mwanaume. Mtoa mada kama ana akili inampasa kuchukua ushauri kwa watu wenye uzoefu kwenye suala kama lake.
 
Sasa wewe hufai kumshauri huyu mtoa mada ushafeli, tena ukute hapo kila mtoto na mama yake. Unadhani utakuwa na familia ya namna gani? Sahau familia bora hapo.
Poa uliyefaulu.

Endelea kufaulu mkuu.

#YNWA
 
Namuona new nyange in town
 
Furaha yako haipaswi kuibwa na yeyote yule


Kaa nae mbali mbali mok moyo utakaporidhia
 


Point nzuri Sana.

Mda anamkumbuka mda nao unakua haupo.
 
Dogo usioe kwanza. Komaa na na uamuzi wako huo huo. Huwezi jua kwanini huyo binti analizimisha sana mazingira ya kuolewa na wewe. Ukikaza na akajua uwezokano ndo wa ndoa ni mdogo ndo utaziona rangi zake vizuri.
Inawezekana alikua na mwamba mmoja kwa muda mrefu af mwamba kamzingua mwishoni, so now hataki kuchezewa tena, kakupata kaona upo fresh, una kipato kizuri, familia yako ipo straight hamna longo longo ndo kaamua alizimishe aolewe hapo.
Swali ni:
je anakupenda kweli?
Je akikuta hali ni tofauti na picha aliyonayo atavumilia?
Tabia zake unazijua kweli? Manake kaanza kutengeneza mazingira toka mnakutana, inawezekana anakuigizia, subiri uoe uone.

Ushauri wangu ni uendelee kukomaa na msimamo wako. Time will reveal everything.
Bro wangu kaoa mke wake baada ya mtoto kufikisha miaka mitano, na walikua mkoa mmoja lakini hakuwa akiishi na huyo mwanamke. Kapigiwa sana kelele lakini kakomaa na uamuzi wake. Siku alipokua tayari katoa taarifa tumefanya harusi mambo fresh tu mpaka leo.
 
Hao wanaokushauri uoe tu ndoa zao zinapumulia mashine. Wamejaza michepuko lukuki.
Namuelewa sana Mr. Liverpool, ingawa nimesoma kisa chake na mchungaji wake. Kweli mlango wa mbinguni mdogo sana.

Slogan yetu ni MITANO TENA
 
Another single mum....[emoji848][emoji848][emoji2827][emoji2827][emoji2827][emoji2827][emoji2827]
Single mum wa kujitakia lkn. A man came clean kwamba haitaji mke na asitegemee kama atamuoa, but akaamua kubeba ujauzito to keep him! Sasa hv bidada atajiona mshindi kweli kweli na hvyo wakwe wamemkubali! Ila atakuja kujuta baadae, ndoa itakuwa ndoano.

Usiombe uolewe na mwanaume hajakupenda, utaletewa michepuko nyumbani, atateseka sana kiakili na kihisia. Pole yake
 
Sikiliza moyo wako, masuala ya kuingia ndoani moyo haujaridhika utakuja kujuta na kuishia kumfanyia visa kwenye ndoa. Pia umri kama bado hivi angalau 30 ndio mzuri kuoa.

Sikiliza moyo wako, period. Maisha mafupi haya.
 
Nadhani thread ingefungwa hapa.
 
Ndugu, sio kila mara utaiendesha SITUATION, kuna muda SITUATION lazima ukubali ikuendeshe
 
Mwana kulitafuta, ukimwacha hyo mwanamke, kuna siku utajuta sana..ni suala la muda tu, Im telling.
Nina ndugu yangu kipindi ana mgogoro na mwanamke anayeishi naye baada ya kumfumania pia mke alikuwa mbinafsi hapendi ndugu wa mwanamme and blabla..
Jamaa akaja pata mwanamke mwingine mwalimu yupo simple wa kawaida tu sio mzuri kivile kama yule wa kwanza ila alikuwa anapendwa na kila mtu hasa upande wa jamaa. Akamzalisha kisha akaanza kumpotezea dada wa watu, akajaribu kubembeleza wee alivyokuja kugundua jamaa karudi kwa ex wake dada akaamua kumove on kimoja nakuendelea na mambo yake ya shule.
Yule dada leo hii ni proffessor pia alikuwa mtu mkubwa sana kwe serikali ya Kikwete, jamaa ni full kujuta full depression mambo yamemwendea vibaya mwanamke yuleyule wa mwanzo ni full kumsumbua, malaya ni malaya tu hadi huruma..
ANGALIZO
Hii ni kwa mwanamke na mwanaume..Huwa tunawachukulia poa sana wale tunaowaona wanatupenda sana na kuwafanyia visa huku tukiamini hawatatuacha bila kujua wao ndo wamebeba mustakabali mzima na maono na mafanikio ya maisha yetu..
 
Wahenga walisema...


Mkataa pema pabaya panamuita!!!



Ni hayo tu.

Alamsiki!
 
Mim nkafkir hata umepatwa na tatizo kubwa sana, au bidadada kakusngizia mimba. Kumbe unajaribu kuonesha vile hautaki kuchkua majukumu yako mpaka unapata depression,
Unataka uoe malaika au wa kwako ni special order
 
Kuna wakati wanaume sijui nini kinatupelekesha kwenye mioyo yetu, ukute huyo ndiye mke uliyepangiwa na Mungu lakini kwa kuwa huna utulivu wa moyo na nafsi unataka kufanya maamuzi ambayo baadae yatakugharimu...

Kumbuka mtoto wako wa kuzaa anauma sana, sasa unataka umuache yeye na mama yake bila kufikiria mara mbilimbili kwamba huko unakotaka kwenda ni kwa namna gani patakuwa salama kwako?
 
Mkuu nawaza hiyo depression uliyosema hapa labda ni ya furaha! Mwanamke ni wife material kabisa huyu sijui unataka wa Aina gani, mtoto umekiri unafanana naye unataka nini tena? Wazazi ni watu wazima na wanafahamu mengi sana hawajaona kasoro kwa huyu binti wamekwambia umchukue wewe unataka ushauri wa jamii forum kuliko wa wazazi wako? Mimi naona depression inajipatia mwenyewe. Nakushauri kwamba kama huna Mpango wa kuacha kuoa basi mchukue huyu binti haraka mtoto wako asiteseke.
 
Ukimuacha huyo mama wa mtoto wako hakika utamkumbuka sana... Take care bahati haibishi hodi inakuja nje ya mipango yako .. ndoa tamu sana acha uoga vaa ujasiri mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…