Msaada wa kimawazo

Wanasemaga usiweke mayai yote kwenye kikapu kimoja
Ila kwa umri huo kama sio chai na unaogopa UTT basi kaweke hata fixed account for 10 yrs

Usisubutu kufanya biashara
Yaani usifanye biashara yoyote
 
Unamaanisha Fixed ni bora kuliko UTT, Kwanini?

#YNWA
 
Hongera sana ni wachache sana wenye bahati kama yako. Una pesa nzuri, umri mzuri, ukitulia vizuri baada ya miaka 10 utakuwa mbali sana. Kuwa makini sana mdogo wangu na kila la kheri.
 
Huu ushauri mzuri zaid
 
real hustler , msomi mwenzangu, nakushauri sana kwa vile hauna experience na biashara sana ila unataka kufanya biashara

Fanya hivi, Hio hela 50% iwekeze kwenye Ununuzi wa Ardhi.

Nunua viwanja Kwa Bei ndogo maeneo mazuri kama Goba, Kibaha kwa Matias huko ama Picha ya ndege (mimi niko Mwanza ila naona Mitandaoni wanauza viwanja huko)

Mfano ukinunua Kiwanja Tsh milioni 5, wewe anza kusaka wateja kwa Bei kubwapo kidogo.

Chunguza kwanza kabla hujanunua ardhi maana huko pia kuna seleka zake
 
Hongera sana kwa kupata mgao kutoka kwa mzee wako. UTT ni wazo jema sana. Nipo huko kwa zaidi ya miaka mitano sasa na hakuna ubabaishaji. Ukiweka hiyo mil 50 ndani ya miaka 30 una zaidi ya 700m. Ni vema kufanya hivyo na kuisahau hela. Naweza kukupa uzoefu wangu zaidi. Kila la kheri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…