Jane Msowoya
JF-Expert Member
- Aug 20, 2017
- 4,302
- 7,815
Wanasemaga usiweke mayai yote kwenye kikapu kimojaHabari yako mwana jf
Baba yangu alibahatika kuwa na mali nyingi sana na kwetu tumezaliwa wachache watu wa nne tu,
Sasa mzee ili kuondoka utata ameamua kugawa mali ingali yupo hai Mimi nimepata mgao wa nyumba ya kuishi pamoja na kiasi kama million 50
Kwa upane wa elimu nina degree ya agribusiness kutokea SUA
Pia binafsi sina background yoyote ya kufanya biashara maana mda mwingi nimetumia shuleni
Niliwaza hii pesa niiweke UTT baada ya kuisoma na kuifatilia Sana lakini changamoto inakuja nahofia usalama wa pesa yangu huko UTT hasa hasa kwenye nchi yetu hii ambayo kiongozi anaweza amua chochote mda wowote.
Naombeni ushauri je naweza anzia wapi katika uwekezaji.
Na je UTT ni salama mathalani kwa miaka 30 ijayo. Umri wangu ni miaka 25.
Pia ningeomba Kwa wenye kujua zaidi ni mkoa gani au eneo gani Tanzania ni zuri Kwa mtu mwenye mtaji kuanza biashara na biashara ipi inaweza kuwa na rejesho zuri.
Asanteni
Ila kwa umri huo kama sio chai na unaogopa UTT basi kaweke hata fixed account for 10 yrs
Usisubutu kufanya biashara
Yaani usifanye biashara yoyote