Msaada wa kisheria katika Ndoa

Msaada wa kisheria katika Ndoa

popo1986

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2014
Posts
1,120
Reaction score
372
Wakuu habari za kazi.kunamtu anaomba msaada juu jambo ambalo mwanandoa mwezi walieishi nae zaidi ya miaka 4.na kuzaa mtoto mmoja lkn hivi leo mumewe ameamua kumuacha na mume huyo ameiba hati ya nyumba na cheti cha kuzaliwa mtoto na amekimbia
Sasa huyo dada anataka kujua kwa kesi hii anashitaki wapi wakuu msaada. Au mwenye uelewa na hizi taasisi za kusaidia wanawake wanao onewa
 
Kama amepewa talaka anayo mkononi basi aende kufungua kesi mahakama ya wilaya adai mgawanyo wa mali, wala asihangaike na hati.
Kama kweli alikuwa mke mahakama italazimishwa ama kuuzwa mali au mmoja amlipe mwenzie stahiki yake endapo atahitaji kubaki na mali yoyote waliyochuma, hiyo ni baada ya kujua bei ya soko
 
Aende ustawi wa jamii au polisi siku hizi wanadawati la jinsia
 
aende TAWLA kule ilala-boma,hapa utapoteza mda wa kusubiria majibu,awaambie kule kuhusu hati ya nyumba ili waweke caveat mapema kabla mume wake hajaamua kuiuza nyumba
 
Wakuu habari za kazi.kunamtu anaomba msaada juu jambo ambalo mwanandoa mwezi walieishi nae zaidi ya miaka 4.na kuzaa mtoto mmoja lkn hivi leo mumewe ameamua kumuacha na mume huyo ameiba hati ya nyumba na cheti cha kuzaliwa mtoto na amekimbia
Sasa huyo dada anataka kujua kwa kesi hii anashitaki wapi wakuu msaada. Au mwenye uelewa na hizi taasisi za kusaidia wanawake wanao onewa

Sasa mkuu maelezo yako mbona hayajitoshelezi?sa tutajuaje ndoa hiyo ni ndoa ya namna gani?sisi sio malaika wakutoa majibu yasiyo na maelezo sahihi..haya lete maneno hapa.NDOA NI YA NAMNA GANI?
 
coxson, hiyo avatar yako ya dracula inatisha sana! Naomba uibadilishe!
 
Last edited by a moderator:
Sawa mkuu SHIEKA nitaibadili ola ndiyo sura yangu
 
Kabla hatujatoa msaada zaidi...kwanza inabidi utuweke wazi iyo ndoa yao ilifungwa kwa misingi ya imani ipi (ni aina gani ya ndoa)yaani ni je ilifungwa kwa misingi ya dini ya kiislam,kikristo au kiserikali?tuanzie apo kwanza.
 
Back
Top Bottom