Msaada wa Kisheria kuhusu mahusiano na Mwanafunzi

Msaada wa Kisheria kuhusu mahusiano na Mwanafunzi

Mnamkatili tu bwana mdogo ilitakiwa mumpe moyo aendelee kuwa na binti
 
Ndugu wa JF hapa kuna Mvulana ( Sio Mwanafunzi) alikamatwa na Msichana (Mwanafunzi).

Alipokamatwa akaitwa mtendaji wa kata pamoja na baba mzazi wa binti. Kesi ikapelekwa Polisi then mahakamani. Mahakama inataka ushahidi (Ambao tayari upo maana walipigwa picha na video wakiwa pamoja)

Mtendaji amekuwa akiwalazimisha wazazi wa binti hususani mwanamke (ambaye hakuwepo kwenye tukio) kufika mahakamani kutoa ushaidi na mama amegoma kwa madai ya kuwa hakuwepo kwenye tukio hivyo hana ushaidi wa kuiambia mahakama lakini pia na ugumu wa maisha hana nauli za kumpeleka mahakamani.

Swali langu: Je huo ushaidi wa picha hautoshi kumfunga huyo kijana?. Na je anayehitajika kutoa ushaidi ni upande wa wazazi au wale waliowakamata na kupeleka taarifa kwa mtendaji.

Naomba kuwasilisha.
Kijana ana miaka mingapi?

Sent from my SM-A6050 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom