Msaada wa Kisheria kuhusu mahusiano na Mwanafunzi

Msaada wa Kisheria kuhusu mahusiano na Mwanafunzi

Bukoba Finest

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2023
Posts
250
Reaction score
315
Ndugu wa JF hapa kuna Mvulana ( Sio Mwanafunzi) alikamatwa na Msichana (Mwanafunzi).

Alipokamatwa akaitwa mtendaji wa kata pamoja na baba mzazi wa binti. Kesi ikapelekwa Polisi then mahakamani. Mahakama inataka ushahidi (Ambao tayari upo maana walipigwa picha na video wakiwa pamoja)

Mtendaji amekuwa akiwalazimisha wazazi wa binti hususani mwanamke (ambaye hakuwepo kwenye tukio) kufika mahakamani kutoa ushaidi na mama amegoma kwa madai ya kuwa hakuwepo kwenye tukio hivyo hana ushaidi wa kuiambia mahakama lakini pia na ugumu wa maisha hana nauli za kumpeleka mahakamani.

Swali langu: Je huo ushaidi wa picha hautoshi kumfunga huyo kijana?. Na je anayehitajika kutoa ushaidi ni upande wa wazazi au wale waliowakamata na kupeleka taarifa kwa mtendaji.

Naomba kuwasilisha.
 
Hakulazimishwa na wazazi wenyewe wamesema hawana uthibitisho maana hawakuwakamata. Ila Mtendaji anawapa vitishio kwamba watafungwa.
Hawawezi kufungwa bila makosa. Akili ya kawaida tu..
wawaache vijana na mapenzi yao wanahitaji muongozo na si mambo ya mahakamani. Binti hajalazimishwa ni mihemko yake mwenyewe.
 
Hawawezi kufungwa bila makosa. Akili ya kawaida tu..
wawaache vijana na mapenzi yao wanahitaji muongozo na si mambo ya mahakamani. Binti hajalazimishwa ni mihemko yake mwemyewe.
Kwa taarifa nilizopewa kesi imefikishwa mahakamani na mtendaji bila ridhaa ya wazazi na anawalazimisha waende mahakamani kutoa ushaidi ila wamegoma kwenda. Unanishauri niwaambie wafanye nini?
 
Kwa taarifa nilizopewa kesi imefikishwa mahakamani na mtendaji bila ridhaa ya wazazi na anawalazimisha waende mahakamani kutoa ushaidi ila wamegoma kwenda. Unanishauri niwaambie wafanye nini?
Waende mahakamani wakampe moyo mtoto wao. Hakuna sheria yoyote ya kuwakamata wazazi ama kuwalazimisha watoe ushahidi.
 
Ushahidi wa picha inatosha pia wale waliomkamata kama mgambo na yale MAELEZO ya polis baada ya watuhumiwa kuhojiwa!!i!!

Japo inaonyesha wazazi wa binti hawapo TAYARI kumfunga kumfunga kijana!!
Usijibu sichokielewa kurupukaji kubwa

Kwahiyo Mimi nikikutwa na mwanafunzi nimesimama nikipigwa picha niushahidi tayari mahakamani na unanifunga !
 
Kama ni minor haijalishi alikubali, ulimkuta bikra au si bikra au vyovyote wanasema umembaka maana hana maamuzi.
Sawa, lkn wote ni vijana.
Kuwapeleka mahakamani na hadi jela ni kuharibu maisha yao na si kujenga.
Hao ni vijana na wengi tumepita hiyo stage.
Kwani binti ana umri gani?
Huyo mtendaji nini kinamuuma? Nani kafungua kesi? Sijaelewa vizuri labda.

Kesi ilitakiwa iishie kwa mtendaji kwa vijana kupewa onyo.
 
Back
Top Bottom