Msaada wa Kisheria kuhusu mahusiano na Mwanafunzi

Ndugu wa JF hapa kuna Mvulana ( Sio Mwanafunzi) alikamatwa na Msichana (Mwanafunzi).

Alipokamatwa akaitwa mtendaji wa kata pamoja na baba mzazi wa binti. Kesi ikapelekwa Polisi then mahakamani. Mahakama inataka ushahidi (Ambao tayari upo maana walipigwa picha na video wakiwa pamoja)

Mtendaji amekuwa akiwalazimisha wazazi wa binti hususani mwanamke (ambaye hakuwepo kwenye tukio) kufika mahakamani kutoa ushaidi na mama amegoma kwa madai ya kuwa hakuwepo kwenye tukio hivyo hana ushaidi wa kuiambia mahakama lakini pia na ugumu wa maisha hana nauli za kumpeleka mahakamani.

Swali langu: Je huo ushaidi wa picha hautoshi kumfunga huyo kijana?. Na je anayehitajika kutoa ushaidi ni upande wa wazazi au wale waliowakamata na kupeleka taarifa kwa mtendaji.

Naomba kuwasilisha.
Ushahidi wa kubaka mwanafunzi hutomewa na daktari na ikibidi hupimwa dna kuthibitisha aliyemwingilia ni yeue kwwli

Sent from my V2111 using JamiiForums mobile app
 
Kesipo mahakama ya Wilaya na kijana amewekwa mahabusu kwa mujibu wa taarifa ya mtendaji
Ok, mtafutieni dogo wakili msisubiri hadi apigwe mvua ndio muanze kuhangaika. Hiyo kesi kwa maelezo yako tu akipata wakili anaweza kutoboa sababu ya aina ya ushahidi uliopo.

Narudia msisubiri hadi kesi ikasikilizwa, itakuwa haina maana kuweka wakili tena.
 
Ushahidi wa kubaka mwanafunzi hutomewa na daktari na ikibidi hupimwa dna kuthibitisha aliyemwingilia ni yeue kwwli

Sent from my V2111 using JamiiForums mobile app
Hapo hakuna ubakaji bali kuwa na mahusiano na mwanafunzi, hili ni kosa jipya chini ya sheria ya elimu. Yaani hata bila kujamiiana na huyo mwanafunzi, akiwa demu wako tu tayari ni kosa la jinai kwa mujibu wa sheria ya sasa hivi elimu.
 
Ndugu wa JF hapa kuna Mvulana ( Sio Mwanafunzi) alikamatwa na Msichana (Mwanafunzi).

Alipokamatwa akaitwa mtendaji wa kata pamoja na baba mzazi wa binti. Kesi ikapelekwa Polisi then mahakamani. Mahakama inataka ushahidi (Ambao tayari upo maana walipigwa picha na video wakiwa pamoja)

Mtendaji amekuwa akiwalazimisha wazazi wa binti hususani mwanamke (ambaye hakuwepo kwenye tukio) kufika mahakamani kutoa ushaidi na mama amegoma kwa madai ya kuwa hakuwepo kwenye tukio hivyo hana ushaidi wa kuiambia mahakama lakini pia na ugumu wa maisha hana nauli za kumpeleka mahakamani.

Swali langu: Je huo ushaidi wa picha hautoshi kumfunga huyo kijana?. Na je anayehitajika kutoa ushaidi ni upande wa wazazi au wale waliowakamata na kupeleka taarifa kwa mtendaji.

Naomba kuwasilisha.
Picha/,video wakiwa pamoja sio ushahidi USIOTIA SHAKA bado. Kajipange upya
 
Hapo hakuna ubakaji bali kuwa na mahusiano na mwanafunzi, hili ni kosa jipya chini ya sheria ya elimu. Yaani hata bila kujamiiana na huyo mwanafunzi, akiwa demu wako tu tayari ni kosa la jinai kwa mujibu wa sheria ya sasa hivi elimu.
Sheria mpya ya Elimu namba ngapi? Ya mwaka gani? Ile ya 1978 imefutwa?
 
Kilichonifanya nije kuulizia sheria ni baada ya mtendaji kumtumia sms za kumtishia dada yangu kuwa atamfunga nikasema nijue kama anaweza kufungwa kweli.
sasa hii hela kabisa. Mpigie simu huyo mtendaji, mwambie uko mwanza, unafunga safari kuja bukoba, kumshitaki mahakamani na kumreport kwa DED, DAS, RAS ili achuliwe hatua za kinidhamu kwa kosa la kutumia madaraka yake vibaya, ushahidi ni hizo message alizomtumia dada yako. Atakupigia magoti huyo jamaa.

Changamka, bukoba to mwanza hapo ni Chap tu.
 
Naam mkuu, mimi nina majukumu yangu hapa, sema nimemdhibiti kwa asilimia kadhaa baada ya kupewa mawazo na wana JF
 
Ok, mtafutieni dogo wakili msisubiri hadi apigwe mvua ndio muanze kuhangaika. Hiyo kesi kwa maelezo yako tu akipata wakili anaweza kutoboa sababu ya aina ya ushahidi uliopo.

Narudia msisubiri hadi kesi ikasikilizwa, itakuwa haina maana kuweka wakili tena.
Kesi ishasikilizwa jana na wamepangiwa tarehe moja mwezi ujao. Mimi concern yangu ilikuwa ni kujua uhusiano wa hii kesi na wazazi wa binti ambao hawakuwa kwenye tukio
 
Hapo hakuna ubakaji bali kuwa na mahusiano na mwanafunzi, hili ni kosa jipya chini ya sheria ya elimu. Yaani hata bila kujamiiana na huyo mwanafunzi, akiwa demu wako tu tayari ni kosa la jinai kwa mujibu wa sheria ya sasa hivi elimu.
Ndiyo, lakini si inaendeshwa na Jamuhuri?
 
Kesi imeendeleaje?? Kwa sasa nipo bukoba..nitumie no yako nataka nikajifunze kitu kwenye kesi hii ya mpango
 
Hawawezi kufungwa bila makosa. Akili ya kawaida tu..
wawaache vijana na mapenzi yao wanahitaji muongozo na si mambo ya mahakamani. Binti hajalazimishwa ni mihemko yake mwenyewe.
Kuna watu wanasahau kua nao kuna kipindi walipitia foolish age Kama za hao vijana na balehe zao za awali!!
 
Usijibu sichokielewa kurupukaji kubwa

Kwahiyo Mimi nikikutwa na mwanafunzi nimesimama nikipigwa picha niushahidi tayari mahakamani na unanifunga !
Picha haimfungi Mtu, labda Kama ni picha na video za ngono, Kama zile zilizo mponza Ambaruti!!
 
Back
Top Bottom