Msaada wa kisheria kwa makosa ya jinai kwenye ushahidi

Msaada wa kisheria kwa makosa ya jinai kwenye ushahidi

mbapa

Member
Joined
Feb 4, 2014
Posts
63
Reaction score
18
Habari
wanaJf?.

Kuna ndugu yangu ambae ni mtuhumiwa kwa wizi wa mifugo!. Ushahidi unaomweka hatiani hauna kidhibiti wala hajakamatwa kwenye eneo la tukio badala yake amekamatwa kwenye shughuli zake na kuambiwa ameiba siku zilizopita. Shahidi wa mlalamikaji ni askari ambae anasema "nliambiwa na msiri wangu kua mtuhumiwa ameiba sehemu husika tarehe flan saa flan". Naomba ushauri wa kisheria kwa pande hizo mbili. Je, atahukumiwa jela au faini?, au ataachiwa huru?. Na kwanin ahukumiwe au aachiwe huru?. Shauri lipo mahakama ya mwanzo
 
Mashauri ya jinai yanafunguliwa polisi. Inategemea upepelezi wa polisi utakavyojitosheleza.
 
Sheria hairuhusu kuzungumzia shauri ambalo liko Mahakamani. Lakini Kama atahukumiwa jela au kutofaini njoo huku tena tutakushauri
 
Sheria hairuhusu kuzungumzia shauri ambalo liko Mahakamani. Lakini Kama atahukumiwa jela au kutofaini njoo huku tena tutakushauri

Ok!. Nashkuru mkuu kwa kunijuza kitu nisichokijuaga!.
 
ila mara zote kwenye sheria mahakama haikubali ushaidi wa kusikia tu kutoka kwa mtu i mean 'hearsay evidence is not admissible in the court unless supported by colloborative evidence" kwenye swala lako shahidi anasema yee aliambiwa kuwa mtuhumiwa aliiba siku fulani na msiri wake, ushahidi wake haukubaliki mpaka amlete huyo msiri athibitishe kuwa kwa macho yake alimuona mtuhumiwa akiiba siku ya tukio. Upande wa mashtaka ndo unatakiwa uthibitishe kuwa ni kweli mshtakiwa aliiba ila ndugu yako ana haki ya kujitetea kuwa hajahusika na tukio hilo kwa kutoa defense kama ya "alibi" kwamba hakuwa eneo la tukio siku ya wizi. Zaidi achia mahakama itaamua.
 
Afande akiambiwa mlete huyo msiri wako aje kuithibitishia mahakama kua ameona tukia anasema msiri analindwa kisheria. Kwa hyo ni ushahidi wa kuambiwa na msiri ambae analindwa kisheria. Mlalamikaji yeye anasema "mimi sikujua kua huyu ndie mwizi ila tu nlijua baada ya kuambiwa na afande ambae aliambiwa na msiri wake.
 
Hukumu imetolewa leo mtuhumiwa aachiwa huru!. Mlalamikaji alalamika na kusema atakata rufaa na mshitakiwa nae ataka kukata rufaa ya kudai fidia. Je ni nani mwenye nafasi nzuri ya kukata rufaa?. Na kwanini?
 
Back
Top Bottom