Msaada wa kisheria: Partnership kwenye biashara

Hii inaitwa pika bomu. Kwamaelezo haya naona wewe ndio unalazimisha patnership yenu. Kifupi jamaa keshajua wewe ni dhaifu kiasi gani kwake hivyo anatumia kukutisha na wewe umetishika. Nakwambia utakuwa mtumwa wa hiyo biashara hadi ushangae.
Haswaaaaaa
 
Kwa maelezo yake haitoshelezi kuonyesha kwamba yeye ndio alimuacha huyo jamaa. I can dump you and then help you, that's not a problem at all and that doesn't mean nataka njirudishe kwako. It is just that my heart is too soft and I am so humane.
 
Hahahahahahaah.

Ataliwa soon huyu dada. Yaani huyu mdogo wetu ametoa macho kwenye hela hajui kategwa tu.

Jamaa anamwambia yupo radhi a-inject more more ili tu yeye apate 50% profit na yeye anakubali tu.

Ngoja anijibu kwanza swali langu then ntamshauri vizuri
 
Njoo inbox uniambie how much unataka mtu ainvest...hiyo pasu kwa pasu kwangu mie poa tuu
 
Sawa. Sasa twende sawa.
1. Biashara haina uhusiano wowote na mapenzi yenu wala na mmoja kati yenu. Inasimama kama yenyewe. Inaweza kumfungulia mtu mashtaka ama ikafunguliwa mashtaka. Hakikisha mnairasimisha kwa kuisajili brela.
2. Huyo jamaa aweke wazi kama anataka partnership ama anataka kuinvest. Ikiwa anataka partnership basi akichangia 50%–50% tafsiri yake kisheria ni kwamba mtagawana faida na/au hasara kwa uwiano sawa. Akichangia 70%, wewe ukaweka 30% (thamani ya biashara yako sasa hivi), basi mtagawana faida na/au hasara kwa uwiano huo huo (yeye 70%, wewe 30%) n.k Ila ikiwa anataka kuwekeza, basi utamlipa dividends kulingana na makubaliano. Mara nyingi hii hulipwa bila kujali biashara imetengeneza faida ama la. Na huwa kiwango constant kwa muda maalum mf. 12% kila mwaka.
3. Ikiwa wewe ndo unafanya kazi zote (kwa makubaliano yenu kama business partners) basi utalipwa mshahara kulingana na viwango vya soko. Maana yake kama kazi hiyo hiyo katika kampuni nyingi mtu analipwa laki 5 basi nawewe utalipwa laki 5 ikiwa ni sehemu ya operation expenses (pamoja na data, carriage outwards, inwards, etc).

NB: Mwandiko wako ni mbaya pia fanya upate thamani ya goodwill kabla hujakubaliana thamani halisi ya biashara yako.

For more business consultation and I.T solutions reach me kwa PM
 
Option ingine mwambie akukopeshe hiyo pesa utamlipa baada ya mda fulani sio hainvest then akileta mambo issue za kurudiana mkubalie endeleeni kutumiana huku unakuza biashara yako...hakikisha unampango wa kumlipa baada ya hicho kipindi ulichokubaliana then ukishamlipa chake utaamua kusuka au kunyoa kuhusu yeye...sometimes kutumiana sio mbaya sna[emoji12]
 

Nimejaribu kupitia ile convo ya SMS aliyoiweka kati yao, nimenote vitu kadhaa:-

Jamaa anajua udhaifu wa huyu dogo, kiasi kwamba anaweza ku-dictate kuandaa deeds na kusema eti Mwanasheria asihusike na dogo akakubali.

Zile short forms za sms anazozotumia jamaa sioni kama ni business brain, hapo kuna brain ya kichwa cha chini ndiyo inayofanya kazi

Lengo la jamaa kurudi ni kutaka mahusiano yarudi, ila pia anataka ku-manage business.

Hata kama tutakubaliana 50/50, kuna siku ataibuka kusema amepunjwa kwenye mahesabu ya "what is 100%". Na hapo ndo itaibuka ile ya nirudishie hela yangu. Na wakati huo cash hakuna, sijui nini kitafidia.

Mdogo wetu hajajua ukubwa wa biashara yake, naona kapiga hesabu tu za kifedha, kuna kitu Goodwill hajaihusisha, huyu jamaa anaweza kuja kuijaribu hiyo.

All in all, siyo lazima mawazo yetu yawe sawa. Yeye anamfahamu zaidi, aangalie uwezekano wa kuona kama anaweza kudili naye kwa haya aliyoambiwa humu.

Akili za kuambiwa changanya na zako. (Rais Mstaafu, Jakaya Mrisho Kikwete).
 
Yaani ile convo inatosha kabisa kukuonyesha kwamba jamaa is not in for the business. He is in for his own benefit!
 
Unapokuwa unafanya kazi then upigie mahesabu kiasi cha pesa unachopaswa kujilipa. Na iwe ni sehemu ya matumizi katika uendeshaji.

Kisha faida halisi ndiyo mgawane 50/50.
Yeah, this is it.
Mkubaliane kusajiri kampuni.
  • Wewe ulipwe mishahara.
  • Huo mishahara wako uwe sehemu ya matumizi(expenses).
  • Mugawane faida 50/50 baada ya kutoa matumizi na kodi za kaisari.
  • Wewe na yeye muwe wakurugenzi wenye maamuzi sawa, ingawa wewe utakuwa Managing Director (MD).
  • Hayo makubaliano yawe kwenye MOA.
  • Ulipofikia inabidi uondoke kwenye kufanya biashara kama sole proprietor, nenda hatua nyingine ya limited company ili ikitokea hasara usidaiwe na mtu au na yeyote wewe kama wewe Tuttyfruity bali idaiwe kampuni kama separate entity.
  • Uzuri wa hiyo limited company kila maamuzi huyo partner wako atashiriki hivyo hawezi kudai chochote mkipata hasara.
  • Mwisho angalia kama mwenzio siyo mbishi mbishi au mtu anayetaka kukuongoza zaidi wakati wewe ndiye una uzoefu na unajua zaidi kuhusu hiyo biashara, akiwa mbishi mtaanguka mapema tu.
  • Kila la heri na mapambano ma na jini nyonya fedha TII AARA EEII (TRA).
 
Tusifanye hivyo tumuokoe....dada ana wazo zuri basi tuwekeze sie wana jf...charity starts at home.

Tusimuache aangamie. Na vile amekuja hapa kuomba ushairi inaonyesha kabisa anajitambua na open minded
Hela kkashapokea na ukute kashaitumia. Kumuokoa tufanyeje, tumchangie?
 
I take a note here. thanks
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…