Msaada wa kisheria: Partnership kwenye biashara

Msaada wa kisheria: Partnership kwenye biashara

Hii inaitwa pika bomu. Kwamaelezo haya naona wewe ndio unalazimisha patnership yenu. Kifupi jamaa keshajua wewe ni dhaifu kiasi gani kwake hivyo anatumia kukutisha na wewe umetishika. Nakwambia utakuwa mtumwa wa hiyo biashara hadi ushangae.
Haswaaaaaa
 
Mm ni mpambanaji kama ww. Huyo jamaa kwa jicho la kuangalia maili 100 mbele na kuchungulia gizani hafai kua partner kwenye biashara. Kwa sababu mpaka hapo inaonekana ww ndo ulimuacha kwenye mapenzi. So kajidogoisha akiwa amekuja kishriki biashara lkn lengo lake ni kukuangamiza. Na ukimruhusu tegemea yafuatayo.

1. Kuandaa mkataba wenye lugha ngumu na mambo yaliyojificha. Unatakiwa utumie mwanasheria nguli tena zaidi ya mmoja kuchunguza lugha za mkataba husika.
2. Anataka ajue weakness yako ili a-take advantage na kuimiliki biashara.
3. Kuiangusha biashara yako kwa kuzusha mambo mengine kama vyesi, uchawi na uganga.

4. Kurudi ili mrudiane hatimae aimiliki biashara yeye kama yeye.

Muda ni hakimu mzuri. (Wanawake mkishauriwa mnasemaga mnaonewa wivu....yakiwakuta mnarudi kwa kuweka mikono nyuma mkiomba ushauri)
Kwa maelezo yake haitoshelezi kuonyesha kwamba yeye ndio alimuacha huyo jamaa. I can dump you and then help you, that's not a problem at all and that doesn't mean nataka njirudishe kwako. It is just that my heart is too soft and I am so humane.
 
Very unfortunate umeshaipokea hiyo hela.

Huyo jamaa anataka kurudi kwa ajili ya issue za mapenzi, na amejua udhaifu wako ulipo.

Pamoja na ushauri wote uliopewa, binafsi ningekushauri usifanye partnership na mtu ambaye ulishapita naye au unapita naye (labda kama ni mume).

Otherwise, vitu vingine viende kama wadau walivyoshauri.
Hahahahahahaah.

Ataliwa soon huyu dada. Yaani huyu mdogo wetu ametoa macho kwenye hela hajui kategwa tu.

Jamaa anamwambia yupo radhi a-inject more more ili tu yeye apate 50% profit na yeye anakubali tu.

Ngoja anijibu kwanza swali langu then ntamshauri vizuri
 
Habarini wana jamvi. Nimeamua kuja hapa kuomba ushauri kwa hili swala. Nimeona nije kwa watu wasionifahamu ili kuondoa "conflict of interest"

Straight kwenye mada, kuna biashara nimekua nikifanya kwa muda wa mwaka mmoja sasa. Nilianza from scratch mwenyewe bila msaada kutoka kwa mtu yeyote. Okay alhamdulilah one year down the line biashara imekua , na ina potential ya kukua zaidi. Yani inshort si meet demand ya wateja kwa sababu nna limited funds.

Unajua tena ukianza kufanya kitu watu huwa wanakucheki tu kuona how far you will go with it.

okay nisiwe muongo I want to bring all the facts ili mnipe ushauri mzuri, kuna jamaa nilikua natoka nae sawa, katika mapenzi yetu tulivyokua tuna share mambo yetu akawa intrested na biashara yangu, jinsi nnavyoifanya na faida nnayoitengeneza alivutiwa ku invest lkn katika mda ule alikua na mambo mengi hakuweza. Sasa tumeachana na huyu jamaa lakini karudi anataka ku invest . For my own safety nimemwambia a invest the same amount that my business is worth ili asinizidi kete.

tatizo liko hapa, although huyu jamaa ana invest fedha lakini management na operations zote ntakua nafanya mimi. It's an online business currently I run all social media, Facebook, Instagram, WhatsApp business etc. na kama mnavojua online business haina muda wa kufunga yani nakua online muda wote. Nashughulikia logistics kuorder, kusafirisha mpaka kupokea mzigo ni mimi. Sales na deliveries nafanya mimi na ntaendelea nafanya mimi cause this guy yeye anaishi mji mwingine.

shida inakuja hapa, huyu jamaa anataka tugawane profit 50,50. Nimefikiria mimi ndo ntakua ninafanya kazi zote muda wote it is unfair kugawana faida sawa bin sawa.

secondly kuna mtu nimemuuliza kaniambia kama mimi ndo ntakua nna run hiyo biashara full time ikitokea huko mbeleni tukapata hasara basi jamaa anaweza kunibana nimlipe pesa yake + profit. Sijajua hili lina ukweli kiasi gani. Lakini hiki kimenifanya niogope.

mimi nataka tugawane 60% by 40% profit kwa sababu nlizozitaja hapo.
Also jamaa anataka ku draft some kind of legal paper work which will legally bind me in the contract. Sitaki ku sign kitu kitakacho niweka matatizoni baadae au hata kupotezq biashara yangu kabisa cause this is all I got.

Guys nipeni ushauri unaoeleweka, ushauri ulioenda shule. Kama kuna lawyers humu ndani itakua vizuri zaidi.

msiuseme muandiko wangu hakuna alionilipia ada humu ndani.

Wsalaam.
Njoo inbox uniambie how much unataka mtu ainvest...hiyo pasu kwa pasu kwangu mie poa tuu
 
Sawa. Sasa twende sawa.
1. Biashara haina uhusiano wowote na mapenzi yenu wala na mmoja kati yenu. Inasimama kama yenyewe. Inaweza kumfungulia mtu mashtaka ama ikafunguliwa mashtaka. Hakikisha mnairasimisha kwa kuisajili brela.
2. Huyo jamaa aweke wazi kama anataka partnership ama anataka kuinvest. Ikiwa anataka partnership basi akichangia 50%–50% tafsiri yake kisheria ni kwamba mtagawana faida na/au hasara kwa uwiano sawa. Akichangia 70%, wewe ukaweka 30% (thamani ya biashara yako sasa hivi), basi mtagawana faida na/au hasara kwa uwiano huo huo (yeye 70%, wewe 30%) n.k Ila ikiwa anataka kuwekeza, basi utamlipa dividends kulingana na makubaliano. Mara nyingi hii hulipwa bila kujali biashara imetengeneza faida ama la. Na huwa kiwango constant kwa muda maalum mf. 12% kila mwaka.
3. Ikiwa wewe ndo unafanya kazi zote (kwa makubaliano yenu kama business partners) basi utalipwa mshahara kulingana na viwango vya soko. Maana yake kama kazi hiyo hiyo katika kampuni nyingi mtu analipwa laki 5 basi nawewe utalipwa laki 5 ikiwa ni sehemu ya operation expenses (pamoja na data, carriage outwards, inwards, etc).

NB: Mwandiko wako ni mbaya pia fanya upate thamani ya goodwill kabla hujakubaliana thamani halisi ya biashara yako.

For more business consultation and I.T solutions reach me kwa PM
 
Option ingine mwambie akukopeshe hiyo pesa utamlipa baada ya mda fulani sio hainvest then akileta mambo issue za kurudiana mkubalie endeleeni kutumiana huku unakuza biashara yako...hakikisha unampango wa kumlipa baada ya hicho kipindi ulichokubaliana then ukishamlipa chake utaamua kusuka au kunyoa kuhusu yeye...sometimes kutumiana sio mbaya sna[emoji12]
 
Hahahahahahaah.

Ataliwa soon huyu dada. Yaani huyu mdogo wetu ametoa macho kwenye hela hajui kategwa tu.

Jamaa anamwambia yupo radhi a-inject more more ili tu yeye apate 50% profit na yeye anakubali tu.

Ngoja anijibu kwanza swali langu then ntamshauri vizuri

Nimejaribu kupitia ile convo ya SMS aliyoiweka kati yao, nimenote vitu kadhaa:-

Jamaa anajua udhaifu wa huyu dogo, kiasi kwamba anaweza ku-dictate kuandaa deeds na kusema eti Mwanasheria asihusike na dogo akakubali.

Zile short forms za sms anazozotumia jamaa sioni kama ni business brain, hapo kuna brain ya kichwa cha chini ndiyo inayofanya kazi

Lengo la jamaa kurudi ni kutaka mahusiano yarudi, ila pia anataka ku-manage business.

Hata kama tutakubaliana 50/50, kuna siku ataibuka kusema amepunjwa kwenye mahesabu ya "what is 100%". Na hapo ndo itaibuka ile ya nirudishie hela yangu. Na wakati huo cash hakuna, sijui nini kitafidia.

Mdogo wetu hajajua ukubwa wa biashara yake, naona kapiga hesabu tu za kifedha, kuna kitu Goodwill hajaihusisha, huyu jamaa anaweza kuja kuijaribu hiyo.

All in all, siyo lazima mawazo yetu yawe sawa. Yeye anamfahamu zaidi, aangalie uwezekano wa kuona kama anaweza kudili naye kwa haya aliyoambiwa humu.

Akili za kuambiwa changanya na zako. (Rais Mstaafu, Jakaya Mrisho Kikwete).
 
Yaani ile convo inatosha kabisa kukuonyesha kwamba jamaa is not in for the business. He is in for his own benefit!
 
Unapokuwa unafanya kazi then upigie mahesabu kiasi cha pesa unachopaswa kujilipa. Na iwe ni sehemu ya matumizi katika uendeshaji.

Kisha faida halisi ndiyo mgawane 50/50.
Yeah, this is it.
Mkubaliane kusajiri kampuni.
  • Wewe ulipwe mishahara.
  • Huo mishahara wako uwe sehemu ya matumizi(expenses).
  • Mugawane faida 50/50 baada ya kutoa matumizi na kodi za kaisari.
  • Wewe na yeye muwe wakurugenzi wenye maamuzi sawa, ingawa wewe utakuwa Managing Director (MD).
  • Hayo makubaliano yawe kwenye MOA.
  • Ulipofikia inabidi uondoke kwenye kufanya biashara kama sole proprietor, nenda hatua nyingine ya limited company ili ikitokea hasara usidaiwe na mtu au na yeyote wewe kama wewe Tuttyfruity bali idaiwe kampuni kama separate entity.
  • Uzuri wa hiyo limited company kila maamuzi huyo partner wako atashiriki hivyo hawezi kudai chochote mkipata hasara.
  • Mwisho angalia kama mwenzio siyo mbishi mbishi au mtu anayetaka kukuongoza zaidi wakati wewe ndiye una uzoefu na unajua zaidi kuhusu hiyo biashara, akiwa mbishi mtaanguka mapema tu.
  • Kila la heri na mapambano ma na jini nyonya fedha TII AARA EEII (TRA).
 
Tusifanye hivyo tumuokoe....dada ana wazo zuri basi tuwekeze sie wana jf...charity starts at home.

Tusimuache aangamie. Na vile amekuja hapa kuomba ushairi inaonyesha kabisa anajitambua na open minded
Hela kkashapokea na ukute kashaitumia. Kumuokoa tufanyeje, tumchangie?
 
Tumia mfano ufuatao. Assume hiyo biashara ingekuwa ni yangu kwa 100%, na kwa status hiyo hiyo uliyonayo sasa hivi, naamua kukuajiri unifanyie yale yote unayofanya sasa kwenye hiyo biashara, kwa muda wote ambao unafanya sasa!

Je, ungependa nikulipe Sh. ngapi kwa mwezi?

Baada ya hapo, tutaende sehemu ya pili kwa sababu suala sio tu ku-finance hiyo biashara ni lazima mkubaliane rasmi na sio kimapenzi namna ya ku-share Profit and Loss ili asije akawa anadai faida tu kwa sababu anaona biashara inatengeneza faida. Kwa kifupi, kuna mengi ya kuangalia!
I take a note here. thanks
 
Back
Top Bottom