Msaada wa kisheria tafadhali

Farolito

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2018
Posts
12,001
Reaction score
27,175
Habari wakuu,
Hivi ikitokea mti uliopo kwenye eneo lako(kwa maana ya ardhi) ukaangukia upande wa jirani mnae pakana nae na ukaleta madhara yawe makubwa kama kuua au madogo mfano kulalia bati likapinda au kuvunja sehem ya choo nk bila mti huo kusababishwa na mtu km kukatwa,ni kwamba umeanguka wenyewe tu au sehemu ya tawi limekatika labda kwa upepo,je mimi mmiliki wa mti huo(eneo) nitakua na kosa kisheria?,
Tusaidiane uelewa.
Ahsante.
 
Ndio utakuwa na kosa kwakadri ya ukubwa wa mti na adhari zake ukate tu
 
Ndio utakuwa na kosa kwakadri ya ukubwa wa mti na adhari zake ukate tu
Lakini mkuu wakati ananunua eneo aliukuta na aliuona na akaridhia kuuziwa eneo na mmiliki mimi nikiwa tayari naishi
 
Ndio.

Kama mmiliki wa mti ulichukua tahadhari zipi kuhakikishi mti hauleti madhara kwa jirani.

Negligence yako inavuka vipimo gani??

Ni upi utambuzi wako juu ya madhara ya mti?

Ulifanya uzembe?

Madhara yaliyotokea ni yapi na yanashabihiana vipi na kwa kiasi gani na negligence yako?

cc Malcom Lumumba
 
Utakuwa na kosa na utashtakiwa tu
 
Asante kwa maoni yako mkuu,
Inawezekana kabisa nilifanya kila jitihada kama vile kuupogoa matawi kadhaa ambayo mimi niliona yanahatari kama wajibu wangu lakin bado mimi pia nina uhitaji na mti kwa kivuli na faida zingine,pili huyu mtu wakati ananunua eneo aliukuta huo mti na pengine aliona kwamba upo karibu na atakapojengo je yeye kwanini hakuchukua tahadhari ya kuacha hilo eneo,je yeye wajibu wake ulikua upi?,mwisho kilichosababisha mti kukatika ni janga la kiasili kama vile upepo au radi nk kwanini niwajibike?
 
No case to answer.. Coz court will look your intention.. Kwani ulidhamila kupanda huo mti ili uje udamage huyo jirani yako na pia kuanguka kwa mti ni ni kama Act ya Mungu tu haipo within power ya human being.. KM amekupeleka mahakamani usiogope kabisa
 
Nadhani kwa mujibu wa sheria za torts unawajibika kulipa. Kwasababu mtu anajetunza kitu huku kwa uelewa wa kawaida "ordinary man" akijua kwamba kwa namna moja au nyingine kinweza kuleta madhara "does so at his own peril"

Hata kama it was due to the act of God, as at the ordinary understand you ought to have foreseen the consequences of you tree upon falling. (You are advised to seek a professional advice to stay on the safe side of the law.)
 
Kwenye sheria hiyo tunaita 'Negligence' meaning "breach of a duty of care which results in damage."

Ni kosa kisheria.

Huwezi kuacha kuchukua tahadhari kwa kutoukata mti au ku prune matawi ambayo kwa njia moja au nyingine yanaweza kuwa hatarishi kwa usalama wako na jirani yako.

Kumbuka kuwa hata kama mti huo ukiangukia kwako na kusababisha madhara kwa binadamu au mnyama yoyote bado utakuwa na kesi ya kujibu.
 
Ivi uko serious kweli?
 
Je wajibu wa mnunuzi wa eneo ni upi?,maana wakati ananunua alipaswa kuona hatari iliopo mbele yake
Sheria za tort zipo wazi. Kwa kifupi inaitwa strict liability. Mtu yeyote akiweka kitu kwenye ardhi basi kisilete madhara kwa mtu mwingine. That's why kupitia strict liability, bomba la serikali la mafuta lilipoungua na kuwaka moto na kusababisha madhara kwa watu wa hapa dar nadhani buguruni, walilipwa.

Nafikiri anaesema kuhusu ACT BY GOD kwa mtazamo wangu haiwezi kuwa defence katika sheria maana huwa inatumika kwenye tetemeko la ardhi, volcano, mvua kubwa, maji ya mito, chemchem, mafuriko nk. Kama kungekuweko na mvua kubwa au mmomonyoko wa ardhi au kimoja wapo hapo juu ndo kingesababisha kutokea ishu hyo, basi usingewajibika.

Zipo kesi za namna hizo na mahakama ilishaweka precedent kuhusu hyo ishu hvyo huo ndo ushauri wangu.

Kindly be advised
 
Je wajibu wa mnunuzi wa eneo ni upi?,maana wakati ananunua alipaswa kuona hatari iliopo mbele yake
Kuhusu wajibu wa mnunuzi ni kuwa kuna msemo unasema "customers beware" au kwa lugha ya kisheria katika mikataba basi kuna kitu kinaitwa "as is bases" yaani tafsiri yake ni kuwa ukinunua kitu chochote huwa una wajibu wa kufanya research, kupata ushauri na kisha kujua athari ya hicho kitu ili ukinunua basi UMENUNUA NA MAPUNGUFU YAKE. Iwapo umenunua gari kwa mfano then after two weeks likaharibika, km ni used utamrudishia? Hyo ndo tafsiri ya "As is bases" na wewe mnunuzi pia umo kwenye kundi Hilo.
 
Mkuu hii ni strict liability na si negligence. Ukishtaki kwa njia hii preliminary objection inakuhusu na unaweza shindwa kesi. Soma vizuri strict liability na negligence. Japokuwa unaweza tafsiri kama kuna uwiano lakini strict liability inahusu zaidi jambo lolote ulilosimika, panda, au kuweka chini ya ardhi ikasabisha hasara kwa mtu mwingine.

Inapaswa kuwapa darasa kwa watu wa sio na ujuzi wa sheria kuliko kila mwanasheria kuweka sheria tofauti tofauti zinawachanganya watu wanaomba ushaur
 
Asante kwa ufafanuzi
 
Swali lako linaendana na hii picha... ngoja wenye majibu waje..View attachment 875867

Ndo hii strict liability. Ili iwe strict liability ni lazima mtu awe amepanda au amesimika kitu, pili hicho kitu ni lazima kilete madhara kwa kupita hadi kwa mtu mwingine yaani property yake km nyumba, eneo, mtu au chochote kinachoweza leta hasara kwa mwingine
 
Asante kwa ufafanuzi
Ila mkuu defence zipo na ni kwa namna gani wakili anawez fika eneo na pia kuweza kung'amua kama anaweza convince the court kutoka strict liability to ACT BY GOD na mahakama ikamuelewa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…